Tafuta

2024.05.23 Papa amekutana na Washiriki wa Mikutano Mkuu ya Watawa wa Hospitali na Mabiti wa Mtakatifu Camillus. 2024.05.23 Papa amekutana na Washiriki wa Mikutano Mkuu ya Watawa wa Hospitali na Mabiti wa Mtakatifu Camillus.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko kwa mashirika mawili ya kitawa wajitume na ujasiri na uthubutu

Baba Mtakatifu Francisko akikutana na washiriki wa Mikutano mikuu ya Watawa 40 wa Hospitali na Mabinti 60 wa Mtakatifu Camillus,amejikita kueleza juu ya historia ya mashirika hayo ya kitawa huku akiwaalika kuendelea na utume wa waanzilishi karibu na wagonjwa,waliobaguliwa na kuthubutu bila kuogopa wajiulize juu ya umaskini wa nyakati zetu.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Alhamis tarehe 23 Mei 2024 amekutana na washiriki wa Mikutano mikuu ya Watawa 40 wa wOspitali na Mabinti 60 wa Mtakatifu Camillus, kwamba, nkipindi hiki ni cha mikutano miwili hadi Julai na kwa namna hiyo ilibidi afanye mikutano kwa mashirika mawili kwa sababu hakuna muda, kwani ni wengi na hivyo amewatia moyo. Baba  Mtakatifu akiendelea ameonesha furaha yake ya kuwapoke akatika muda huu mzuri wa neema kwa ajili yao na kwa watawa wote wanaowawakilisha na kwa ajili ya Kanisa zima!. Mwanzoni mwa safari zao kuna historia mbili za kusisimua, ambazo tunaona jinsi ya ujasiri wa waanzilishi chini ya hatua ya uweza wa Roho Mtakatifu, ambapo wameweza kufikia kazi kubwa, huku wakijizindua wenyewe  wito wa upendo, bila kufanya mahesabu mengi, na 'ukichaa' mtakatifu wa upendo." Na ikiwa upendo haupo, Papa amesisitiza "hakuna kitu!"

Papa amekutana masisita wa Hosptalini na wale wa Mtakatifu Camillus
Papa amekutana masisita wa Hosptalini na wale wa Mtakatifu Camillus

Hiki ndicho kisa cha Maria Angustias Gimenez, Maria Josefa Recio na Mtakatufu Benedetto Menni, ambao mnamo mwaka 1881, wakiongozwa na ari ya Mtakatifu Yohane wa Mungu, katika nchi ya Uhispania yenye matatizo na migawanyiko, walianza kazi ya awali kwa wale. mara, katika huduma ya wa mwisho wa mwisho: wagonjwa wa akili.  Hili ni jambo zuri, lisilo na maslahi ya kibinadamu. Hivyo Masista wa Hospitali ya Moyo Mtakatifu walizaliwa. Na tangu wakati huo mmeendelea na utume wao, wakitoa msaada kwa mateso na umaskini mpya daima, ili kufanya huruma ya Mungu ionekane katika utendaji wa ukarimu, kwa kuzingatia hasa ufufuko na ukarabati wa watu. Na wanafanya hivyo kwa kujaribu kuhusisha kila mtu: wagonjwa, familia, madaktari, watawa, watu wa kujitolea na wengine, katika hali nzuri ya  kijumuiya ambayo kila mtu anashiriki na kuchangia kwa manufaa ya wengine. Hii ni nzuri, kwa sababu kwa njia hii kila mtu huponya pamoja, kila mmoja kulingana na hitaji lake na majeraha aliyobeba. Papa amewao,ba wasisahau kamwe kuwa “sote tunahitaji uponyaji, kila mtu, na kuwajali wengine ni nzuri kwetu.”

Shirika la Mtakatifu Camillus

Papa ameema kuwa haikuwa  miaka mingi baada ya kuanzishwa kwa Masista wa Hospitali mnamo 1892, jijini  Roma, pia mwanamke mwingine, Mtakatifu Giuseppina Vannini, aliongoza wakati huu na Mtakatifu Camillus de Lellis, pamoja na Mwenyeheri Luigi Tezza,  ambaye alizikwa huko Buenos Aires nchini Argentina ambalo Papa alisema alivyotembelea kaburi lake,  alitoa uhai kwa Shirika la Mabinti wa Mtakatifu Camillus, pia waliojitolea kutunza wagonjwa. Papa alisema kuwa “Nililazwa katika  hospitali yao  waliponifanyia upasuaji.” Kwa njia hiyo Papa aliongeza kuwa  Mwanamke huyo alijua vizuri nini maana ya maumivu kwani katika maisha yake alikuwa ameteseka sana kutokana na afya mbaya na kwa sababu nyingine nyingi. Ni kwa msaada wa Mungu na watu wema tu aliweza kufanya hivyo, na kwa hiyo alipenda kurudia: “mateso yanashindwa na upendo tu.” Hivyo, aliwakabidhi wagonjwa kwa upendo wako, dawa ya kwanza na ya lazima ya kila mahali pa matibabu; hakika, kwa nadhiri ya nne ya msaada kwa wagonjwa, aliwaweka katika moyo wa wakfu wao.

Watawa wa Mtakatifu Camillus
Watawa wa Mtakatifu Camillus

Papa Francisko akiendela alisema Padre ambaye alikuwa amelazwa hospitalini pamoja nami aliniambia: “Watawa hawa wanaamini, wanaamini!” Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza kuwa, haya yote ni ishara, ni mwaliko, katika kupambanua kwa Sura zao na wasiogope, waache wasukumwe na uthubutu uleule wa waanzilishi wao, kuthubutu, kujihatarisha kwani uthubutu ni hatari! kwa ajili ya kaka na dada ambao Mungu anawaweka katika njia yao. Kuthubutu, bila hofu, na wajiruhusu kuhojiwa na aina mpya za umaskini wa wakati wetu: kuna mengi! Kwa hivyo watatumia vyema urithi mkubwa na tajiri walioupokea, na watauweka hai kila wakati. Papa amewashukuru sana kwa kazi yao. Tafadhali wasipoteze furaha yao, wasipoteze tabasamu lao na furaha ya moyo. Amewabariki kutoka ndani ya moyo wake. Na tafadhali ameomba wamwombee.

 

 

 

23 May 2024, 16:46