Tafuta

2024.05.20 Papa Francisko alizungumza na maaskofu 200 wa Baraza la Maaskofu Italia wanaofanya mkutano wao hadi 23 Mei 2024. 2024.05.20 Papa Francisko alizungumza na maaskofu 200 wa Baraza la Maaskofu Italia wanaofanya mkutano wao hadi 23 Mei 2024.  (Vatican Media)

Papa Francisko azungumza na CEI juu ya: Uhamiaji, Kupungua kwa miito na Kuunganisha majimbo

Saa moja na nusu ya maswali na majibu kati ya Baraza la Maaskofu Katoliki wa Italia na Papa Francisko wakati wa ufunguzi wa Mkutano wao Mkuu wa 79 mjini Vatican. Katika mazungumzo hayo matatizo mbalimbali ya Kanisa na dunia yalijitokeza:kuanzia kukusindikiza mapadre hadi itikadi za leo hii,kuanzia vijana kuondoka nchini hadi miito iliyopungua, kuunganisha majimbo,utaratibu unaoweza kuingiliwa.

Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.

Matatizo ya dunia ya leo, yakiwemo itikadi, matukio ya uhamaji na maandamano dhidi ya Wayahudi, na yale ya Kanisa, kama vile kuunganisha majimbo au kusindikiza mapadre, yalikuwa kiini cha mazungumzo kati ya Papa Francisko na Maaskofu wa Kanisa la Italia. Kwa njia hiyo Baraz la Maaskofu katoliki nchini Italia  (CEI)  Jumatatu tarehe 20 Mei 2024 mchana katika Ukumbi mpya wa Sinodi mjini Vatican wamefungua kikao chao ambacho kitafungwa tarehe 23 Mei  2024. Muda mfupi kabla ya saa kumi jioni, Papa alifungua Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Maaskofu wa Italia. Akiwa na takriban maaskofu 200 wa Kiitaliano, Papa Francisko alisali masifu ya  Mchana, kisha akawasalimu na hatimaye akawasilisha maandishi yaliyotayarishwa.

Mahojiano ya saa moja na nusu

Kama mwanzoni mwa upapa, Papa alitaka kufanya mazungumzo kwa faragha na wakuu wa  Kanisa la Italia - ambao tayari walikutana katika ziara kumi na sita za miezi ya hivi karibuni - walioalikwa kuzungumza kwa uhuru na kwa uwazi. Kwa muda wa saa moja na nusu, hadi saa 11.30, jioni  Papa Francisko alisikiliza maswali yao na kutoa majibu na kwa tafakari ya kufikiria. Mada nyingi ziliibuka wakati wa mazungumzo: vijana, wale waliosalia na wale wanaoondoka Italia, “kuifanya kuwa masikini", wasiwasi wa sasa na maisha yao ya baadaye, itikadi zinazojiingiza katika utamaduni na jamii, kupungua kwa miito ya vijana katika seminari na utunzaji wa waliopo, kukaribishwa kwa wahamiaji kama wajibu wa kimaadili, wasiwasi juu ya kurudi kwa misemo ya chuki dhidi ya Wayahudi, sinodi, kusindikiza wachungaji mapadre.

Kuunganisha majimbo

Moja ya mada kuu ilikuwa umoja wa majimbo ya Italia, suala  ambalo Francisko tayari katika mkutano wake wa kwanza na CEI mnamo 2013 alihimiza tafakari ya kina na suluhisho la vitendo, kila wakati akizingatia mashaka ya baadhi ya maaskofu wenyewe, kuhusu vitambulisho mbalimbali vya kiutamaduni vya kila eneo na hatari ya ongezeko ambalo linaweza kuleta matatizo katika ukaribu wa wachungaji. Hali pia ziliwakilishwa kwa Papa katika ziara mbalimbali za ad limina za Mabaraza ya Maaskofu ya kieneo ambayo yaliruhusu Papa kuwa na habari ambayo hapo awali haikuwa wazi. Pendekezo moja ambalo limeibuka ni lile la kuunganisha miundo zaidi kuliko kitu kingine chochote, ikiwa ni pamoja na seminari za kikanda zenyewe (mara nyingi zinazokaliwa na kikundi kidogo cha mapadre), kama alivyohimiza Papa mwenyewe mara kadhaa huko nyuma.

Mgogoro wa miito

Suala hilo linahusishwa kwa karibu na mada nyingine, ambayo imejitokeza mara kadhaa, ya kupungua kwa miito. Baadhi ya Maaskofu walieleza kupunguzwa kwa jumuiya, mapadre na watawa na Papa Fransisko akakumbuka mfano wa Makanisa mbali mbali hasa yale ya Amerika ya Kusini ambapo shughuli za jumuiya hiyo husimamiwa na walei na watawa.

Kusindikiza, sinodi, sala

Kwa kuzingatia katika mazungumzo pia juu ya sinodi na dalili ya kuwasindikiza mapadre wenye upendo wa kibaba, wanaohitaji kuambatanishwa katika mabadiliko na mabadiliko ya kitamaduni ya nyakati hizi. Mbele ya matatizo, Papa alihimiza wasisimamishe shauku yao , kwa uhakika kwamba Mungu kamwe hatawatupa na pia kwa nguvu za Roho Mtakatifu ambaye husaidia kukabiliana na matatizo kwa fikra na mtazamo mpya. Kanisa la “Watakatifu, sio la kidunia,” tafakari mbili za Bergoglio alizowapatiawashiriki wa Sinodi kama kitabu ambacho kinatolewa katika Jumba la Uchapishaji la Vatican na kinakusanya hatua zake mbili, kifungu kutoka '91 “Ufisadi  na dhambi.”

Kama zawadi kitabu:“Watakatifu na wasio wa kidunia”

Mwaliko mkubwa wa Papa Franciskowa kuishi Kanisa la kisinodi na pia kupata mafunzo thabiti kwa mapadre na walei, ili wasitumbukie katika majaribu mabaya ya ukasisi. Katika suala hilo, zawadi iliyotolewa na Papa kwa Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) ilikuwa ya mfano: kitabu “Watakatifu na wasio wa ulimwengu,” kilichochapishwa na LEV. Ni mkusanyo wa michango ya Jorge Mario Bergoglio kutoka enzi tofauti: maandishi kutoka 1991, yenye kichwa Ufisadi  na dhambi, Barua kwa mapadre wa Jimbo la Roma kuanzia majira ya kiangazi 2023, utangulizi ambao haujachapishwa na Papa mwenyewe. Maandiko yote yameunganishwa na kushutumu "ulimwengu wa kiroho" kama pigo la kweli la imani.

Salamu kwa vijana wahudumu wa upishi

Baada kusalimiama kwa  mkono salamu kibinafsi kwa maaskofu ambao jioni ya tarehe 202 Mei  walipata muda wa sala na Rozari kwa ajili ya amani katika KanisaKkuu la Mtakatifu Petro, na  karibu saa 12.15 Jioni, Papa Francis aliondoka kwenye ukumbi wa Vatican kurejea nyumba ya Mtakatifu Marta. Kwanza, hata hivyo, akiwa na rais wa CEI,  Kardinali Matteo Maria Zuppi, alitaka kusalimiana na kikundi cha wahudumu wa upishi wa “La locanda dei girasoli”, wa  Roma, ambao wanaleta pamoja na kuajiri vijana wenye ulemavu au ugonjwa wa Utindio wa Ubongo. Kila mmoja alijipanga na sare zake jioni hii walifurahi sana kwa kuweza kumsalimia Mrithi wa Petro.

Papa na Baraza la Maaskofu Italia (CEI)
21 May 2024, 17:40