Tafuta

Papa Francisko:Unyenyekevu ni lango la fadhila na chimbuko la amani duniani na Kanisani

Katika katekesi ya mwisho wa Mzunguko kuhusu Fadhila na dhambi,Papa amejikita juu ya adui mkuu kiburi kuwa danganyifu wa uweza wa yote mara nyingi hutokea katika moyo wa mwanadamu.Ni hatari sana.Na kuwa maskini wa roho hutufanya tuelewe kuwa sisi ni viumbe wa ajabu lakini wenye mipaka,nguvu na udhaifu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika Katkesi yake, Jumatano tarehe 22 Mei 2024 ilikuwa ni mwisho wa  Katekesi kuhusu Mzunguko wa Fadhilia na dambi ambapo akianza tafakari hiyo amesema kuwa: “Tunahitimisha mzunguko huu wa katekesi kwa kuzingatia fadhila ambayo si sehemu ya fadhila saba kuu  au kitaalimungu, bali ambayo ni msingi wa maisha ya Kikristo, na fadhila hii ni unyenyekevu. Huu ni mpinzani mkuu wa maovu mabaya zaidi, yaani kiburi. Ingawa kiburi na majivuno huvimbisha moyo wa mwanadamu, na kutufanya tuonekane zaidi kuliko tulivyo, unyenyekevu unarudisha kila kitu katika mwelekeo sahihi: sisi ni viumbe wa ajabu lakini wenye mipaka, wenye nguvu na udhaifu. Tangu mwanzo, Biblia inatukumbusha kwamba sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi (taz Mwa 3:19), "Mnyenyekevu" kiukweli hutokana na humus, yaani udongo. Hata hivyo udanganyifu wa uweza wa yote mara nyingi hutokea katika moyo wa mwanadamu na ni hatari sana! Na hii inatuumiza sana.

Papa akisalimia makundi wakati wa katekesi
Papa akisalimia makundi wakati wa katekesi

Ili kujikomboa na kiburi, inatoshi kidogo sana, yaanui ingetosha kutafakari anga lenye nyota ili kupata kipimo sahihi, kama Zaburi inavyosema: “Nizionapo mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota uliloweka, mwanadamu ni kitu gani hata umkumbuke, au mwanadamu ni kitu gani hata umwangalie?” (8,4-5).  Sayansi ya kisasa huturuhusu kupanua upeo zaidi, mbali zaidi, na kuhisi hata zaidi fumbo ambalo linatuzunguka na kuishi ndani yetu. Heri watu wanaoweka mtazamo huu wa udogo wao ndani ya mioyo yao: watu hawa wanalindwa kutokana na tabia mbaya, ya  kiburi. Katika Heri zake, Yesu alianza kutoka kwao kwamba: “Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao” (Mt 5:3). Ni Heri ya kwanza kwa sababu ndiyo msingi wa zile zinazofua: kwa hakika upole, huruma, usafi wa moyo hutokana na hisia hiyo ya ndani ya udogo. Unyenyekevu ni lango la fadhila zote.

Papa akimbariki wenye ndoa wapya
Papa akimbariki wenye ndoa wapya

Katika kurasa za kwanza za Injili, unyenyekevu na umaskini wa roho daima huonekana kuwa chanzo cha kila kitu. Tangazo la malaika halifanyiki kwenye malango ya Yerusalemu, bali katika kijiji cha mbali huko Galilaya, kisicho na maana sana na hivi kwamba watu walisema: Je, kitu kizuri kinaweza kutoka Nazareti?”( Yoh 1.46 ). Lakini ni kutoka hapo ndipo ulimwengu ulizaliwa upya. Mwanamke mwenye fadhila za kipekee na nguvu isiyo ya kawaida ya akili aliyechaguliwa sio malkia ambaye alikulia katika pamba, lakini ni msichana asiyejulikana: Maria. Wa kwanza kustaajabu ni yeye mwenyewe, wakati Malaika alipomletea tangazo la Mungu. Na katika wimbo wake wa sifa, mshangao huu unajionesha: “Nafsi yangu yamtukuza Bwana, na roho yangu inashangilia katika Mungu, mwokozi wangu, kwa sababu ameutazama unyenyekevu wa mtumishi wake” (Lk 1:46-48). Mungu - kwa kusema - anavutiwa na udogo wa Maria, ambao ni juu ya udogo wa mambo ya ndani. Na pia, anavutiwa na udogo wetu tunapokubali udogo huu,” Papa alisisitiza. Yeye kwa aalikuwa na hali halisi nyingine ambayo ilionekana kidogo kidogo katika simulizi ya Injili, lakini ya kipepee uliyotanhwa ni hii “Unyenyekevu”. Kuanzia hapo na kuendelea, Maria atakuwa mwangalifu asipande jukwaani. Uamuzi wake wa kwanza baada ya tangazo la kiinjili ni kwenda kusaidia, kwenda kumtumikia binamu yake. Watu wanyenyekevu hawataki kamwe kutoka katika maficho yao.

Kila mmoja anajaribu kutoa kile alicho nacho kwa Papa
Kila mmoja anajaribu kutoa kile alicho nacho kwa Papa

“Kwenda kuelekea milina ya Yofa ili kumtembelea Elizabeti. Alimsaidia katika miezi ya mwisho ya ujauzito. Lakini ni nani anaona ishara hiyo? Hakuna, ikiwa siyo Mungu. Kutoka hapo kwenye maficho, Bikira utafikiri hataki kutoka kamwe. Kama vile katika umati  sauti ya mwanamke alipasa zaudi ya heri na kusema “ Heri tumbo lililosanaa na maziwa yaliyokunyonyesha” (Lk 11,27). Lakini Yesu kwa haraka  alijibu kuwa daima wenye heri ni walio wa mwisho.” Zaidi ni wale ambao wanasikiliza Neno la Mungu na kuliweka katika matendo (Lk 11,28). Hata ukweli mtakatifu zaidi wa maisha yake - kuwa Mama wa Mungu - haukuwa kitu cha kujivunia kuwa chanzo cha kiburi mbele ya watu. Katika Ulimwengu ambao mbio za kuonekana, ili kujidhihirisha, kuwa bora kuliko wengine, kinyume chake, Maria alitembea kwa uamuzi, kwa nguvu pekee ya neema ya Mungu.”

Papa akiasalimia waamini katika uwanja
Papa akiasalimia waamini katika uwanja

Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo alisisitiza kuwa “ Tunaweza kuwazia kwamba Maria pia alipatwa na nyakati ngumu, siku ambazo imani yake ilizidi kuwa gizani. Lakini hii haikufanya unyenyekevu wake utikisike, ambao ulikuwa kama fadhila ya chembe: Ninataka kusisitiza hili. Unyenyekevu ni fadhila ya chembe. Udogo ambao tunaupata katika unyenyekevu  na pia tunamfikiria Maria.” Yeye daima ni mdogo, hujivua na daima yuko huru na hana tamaa. Udogo wake huu. Ni nguvu zake zisizoshindwa: ni yeye ambaye anabaki chini ya msalaba, wakati udanganyifu wa Masiha mwenye ushindi unavunjwa.” Atakuwa Maria katika siku zilizotangulia Pentekoste, ambaye atakusanya kundi la wanafunzi, ambao hawakuweza kukesha pamoja na Yesu kwa muda wa saa moja tu, na walikuwa wamemwacha dhoruba ilipowasili.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kusisitiza zaidi amebainisha kuwa “ unyenyekevu ndio kila kitu. Ndilo linalotuokoa kutoka kwa yule Mwovu, na kutoka katia hatari ya kuwa washirika wake. Na unyenyekevu ndio chimbuko la amani duniani na katika Kanisa. Mahali ambapo hakuna unyenyekevu kuna vita, na kukosa maelewano, kuna migawanyiko. Mungu alitupatia mfano wa hili katika Yesu na Maria, kwa sababu wao nini? ni wokovu wetu na furaha yetu. Na unyenyekevu ndio njia hasa, njia ya wokovu. Amehitimisha kwa kushukuru.

Katekesi ya Papa Francisko
22 May 2024, 16:30