Tafuta

Baba Mtakatifu anawaalika Waisraeli na Wapalestina kusitisha mara moja mashambulizi huko Ukanda wa Gaza na kuanza kujizatiti katika majadiliano. Baba Mtakatifu anawaalika Waisraeli na Wapalestina kusitisha mara moja mashambulizi huko Ukanda wa Gaza na kuanza kujizatiti katika majadiliano. 

Mashambulizi ya Iran Dhidi ya Israeli: Shikamaneni Kutafuta Amani Mashariki ya Kati

Baba Mtakatifu alitoa wito kwa pande zinazohusika kusitisha mara moja mashambulizi haya kwani yanaweza kupelekea kuibuka kwa vita kubwa ya kikanda huko Mashariki ya Kati. Hakuna taifa linaloweza kutishia uwepo wa Taifa jingine. Nchi zote zina haki ya kuwepo; hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko anasema, nchi zote zishikamane kulinda, kutetea na kudumisha amani sanjari na kuzisaidia nchi za Israel na Palestina kuweza kuishi bega kwa bega, kwa usalama na amani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Israeli na washirika wake wanasema wamezuia ndege zisizo na rubani na makombora zaidi 300 yaliyorushwa na Iran, na kwamba makombora machache tu yaliweza kutua ardhini na kusababisha madhara kidogo. Iran inalipiza kisasi kwa kile inachodai kwamba, Israeli tarehe Mosi Aprili 2024 iliushambulia Ubalozi wa Iran ulioko mjini Damasko nchini Siria na kupelekea watu kumi na tatu kupoteza maisha. Kati yao alikuwemo Brigedia Jenerali Mohammad Reza Zahedi, Kamanda mkuu katika kikosi cha Quds, tawi la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC). Taarifa zinabainisha kwamba, Iran imeunda mtandao wa washirika Mashariki ya Kati ambayo inasema ni sehemu ya mhimili wa upinzani unaopinga maslahi ya Marekani na Israel huko Mashariki ya Kati.

Ndege zisizo na rubani 300 zimeishambulia Israeli
Ndege zisizo na rubani 300 zimeishambulia Israeli

Ni katika muktadha wa mashambulizi ya Iran dhidi ya Israeli, Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 14 Aprili 2024, mara baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu, amesema kwamba, anafuatilia kwa wasiwasi na uchungu mkubwa taarifa za mahusiano kati ya Israeli na Iran kufuatia shambulizi lililofanywa na Iran dhidi ya Israeli. Baba Mtakatifu alitoa wito kwa pande zinazohusika kusitisha mara moja mashambulizi haya kwani yanaweza kupelekea kuibuka kwa vita kubwa ya kikanda huko Mashariki ya Kati. Hakuna taifa linaloweza kutishia uwepo wa Taifa jingine. Nchi zote zina haki ya kuwepo; hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko anasema, nchi zote zishikamane kulinda, kutetea na kudumisha amani sanjari na kuzisaidia nchi za Israel na Palestina kuweza kuishi bega kwa bega kwa usalama na amani kama Mataifa mawili huru.

UN: Mashambulizi ya Iran dhidi ya Israeli ni hatari sana
UN: Mashambulizi ya Iran dhidi ya Israeli ni hatari sana

Baba Mtakatifu anawaalika Waisraeli na Wapalestina kusitisha mara moja mashambulizi huko Ukanda wa Gaza na kuanza kujizatiti katika majadiliano. Wapalestina waendelee kupewa msaada wa kiutu, ili wasitumbukie katika janga. Mateka na wafungwa wa kivita waachiliwe mara moja, ili kupunguza mateso ya watu hawa. Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wotre wenye mapenzi mema kuendelea kusali kwa ajili ya kuombea amani, kwa kuachana na mashambulizi na hatimaye kuanza kujielekeza katika majadiliano na amani.

Vita Kati ya Iran na Israel

 

16 April 2024, 16:21