Tafuta

Upendo kwa Mungu na jirani, maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu kiini na kilele cha maisha na utume wa Kanisa; unyenyekevu katika maisha ya sala ni mambo msingi katika maisha na utume wa Mapadre. Upendo kwa Mungu na jirani, maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu kiini na kilele cha maisha na utume wa Kanisa; unyenyekevu katika maisha ya sala ni mambo msingi katika maisha na utume wa Mapadre.  (Vatican Media)

Maisha na Utume wa Kipadre Unasimikwa Katika: Upendo, Ekaristi na Sala

Upendo kwa Mungu na jirani, maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu kiini na kilele cha maisha na utume wa Kanisa; unyenyekevu katika maisha ya sala ni mambo msingi katika maisha na utume wa Mapadre na kwamba, chimbuko la wito wowote ule ni upendo. Mwenyezi Mungu anawaita wote kuwa ni watoto wake wapendwa na kati yao, kuna wateule wachache wanao kabidhiwa dhamana na utume maalum, wa kuwa karibu zaidi na Mungu kwa njia ya huduma makini

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Upendo kwa Mungu na jirani, maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu kiini na kilele cha maisha na utume wa Kanisa; unyenyekevu katika maisha ya sala ni mambo msingi katika maisha na utume wa Mapadre na kwamba, chimbuko la wito wowote ule ni upendo. Mwenyezi Mungu anawaita wote kuwa ni watoto wake wapendwa na kati yao, kuna wateule wachache wanao kabidhiwa dhamana na utume maalum, wa kuwa karibu zaidi na Mungu kwa ajili ya huduma kwa Mungu na watu wake. Kumbe, changamoto kubwa kwa watu wenye wito maalum ni kutenda kama Kristo Yesu katika maisha na utume wao “Agire in persona Christi” kwa kujitahidi kuwa ni kielelezo cha Sura ya Kristo Yesu, iliyochapswa kwenye kitambaa cha Veronika, tayari kupangusa na kukausha machozi ya watu wanaoteseka kutokana na sababu mbalimbali katika maisha yao. Jambo hili litendeke katika sala kama ilivyokuwa kwa Maria na Martha walivyomwambia Kristo Yesu kwamba, “Bwana, yeye umpendaye hawezi.” Rej. Yn 11:3.

Wito na Maisha ya Kipadre: Upendo, Ekaristi na Sala
Wito na Maisha ya Kipadre: Upendo, Ekaristi na Sala

Hii ni sehemu ya tafakari iliyotolewa na Baba Mtakatifu Francisko kwa Jumuiya za Vyuo vikuu vitatu vya Kipapa kutoka Amerika ya Kusini yaani: Chuo cha Kipapa cha Pio cha Amerika ya Kusini, Chuo Kikuu cha Pio cha Brazili na Chuo cha Kipapa cha Mexico. Baba Mtakatifu Francisko anasema, maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu liwe ni kielelezo cha sadaka ya wao kujitoa bila ya kujibakiza, kwa kukinywea kikombe cha Kristo Yesu katika maisha na utume wao. “Je, mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Hapa kinachofichwa katika kikombe cha mateso ni ushuhuda wa kifodini, yaani watambue kwamba, wamewekwa wakfu ili kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha na utume wao na kuyaweka kando matakwa yao binafsi. Baba Mtakatifu anawakumbusha mapadre kwamba, masomo, kazi na utume wao, mapumziko, maamuzi mbalimbali wanayoyafanya katika maisha ya kila siku, watambue kwamba, yanapaswa kuelekezwa katika huduma ya kipadre.

Unyenyekevu katika maisha na utume wa Mapadre ni muhimu
Unyenyekevu katika maisha na utume wa Mapadre ni muhimu

Mapadre watambue kwamba, hapa duniani wao ni wapita njia, ni wasafiri, kumbe wanapaswa kumwilisha unyenyekevu katika maisha ya sala, faraja katika huduma yao kwa watu wa Mungu. Kristo Yesu alikuwa ni mtu wa sala, lakini hii inajionesha kwa namna ya pekee kabla ya kukamatwa na hatimaye kuhukumiwa kufa Msalabani, alisali sana pale kwenye Mlima wa Mizeituni na akapata faraja kutoka kwa Malaika. Rej. Lk 22:43. Baba Mtakatifu anawaalika Mapadre kuwa ni watu wa sala, daima wajitahidi kuwakumbuka na kuwaombea watu ambao wako katika maisha na utume wao: Walezi wao, Mapadre wenzao pamoja na watu wanaowazunguka. Kwa maneno machache wawe ni waombezi wa watu waaminifu wa Mungu katika shida na mahitaji yao msingi. Kamwe wasisahau kuwakumbuka na kuwaombea viongozi wao na kwa namna ya pekee Baba Mtakatifu mwenyewe. Amewabariki wote hawa na kuwaweka chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria wa Guadalupe, Mlinzi na Mwombezi wa Amerika ya Kusini.

Wito na Maisha ya Kipadre
04 April 2024, 14:33