Tafuta

Baba Mtakatifu amewakumbusha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kwamba, Kristo Yesu ndiye tumaini la maisha yao. Baba Mtakatifu amewakumbusha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kwamba, Kristo Yesu ndiye tumaini la maisha yao.  (Vatican Media)

Kanuni ya Imani: Yesu Aliteswa, Akafa na Kufufuka Kwa Wafu

Baba Mtakatifu amewakumbusha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kwamba, Kristo Yesu ndiye tumaini la maisha yao, kwa mateso na kifo chake, ameweza kuzama katika kaburi ya dhambi zao na hivyo kuwakirimia maisha mapya, tayari kutembea katika mwanga wa Kristo aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu. Sherehe ya Pasaka inawakirimia waamini na walimwengu matumaini na maisha ya uzima wa milele, mwaliko ni kumtangaza na kumshuhudia Kristo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Kuna matukio makubwa mawili ambayo yako mbele ya Wakristo wote. Mosi, Makanisa na Madhehebu mbalimbali ya Kikristo yanajiandaa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 1, 700 tangu Mtaguso wa Nicea ulipoadhimishwa kunako mwaka 325 na kilele cha maadhimisho haya ni mwaka 2025, tukio la pekee na muhimu sana. Mwaka huo Wakristo wote wataadhimisha Pasaka ya Bwana siku moja, matendo makuu ya Mungu kwa waja wake. Kanuni ya Imani ya Nicea-Constantinopoli ni formula rasmi ambayo ilipitishwa na Mababa wa Mtaguso wa Kwanza wa Nicea (325) ikakamilishwa na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381) ili kubainisha imani sahihi ya Kanisa Katoliki dhidi ya uzushi, hasa wa Ario na wafuasi wake. Katika mazingira hayo, lengo kuu lilikuwa kwanza kabisa ni kumkiri Kristo Yesu “Mungu kweli kwa Mungu kweli” yaani Mungu kweli sawa na Baba, halafu kwamba Roho Mtakatifu anastahili kuabudiwa pamoja na Baba na Mwana (Fumbo la Utatu Mtakatifu).

Ufufuko wa Kristo Yesu ni kilele cha ukweli wa imani
Ufufuko wa Kristo Yesu ni kilele cha ukweli wa imani

Wakristo wanataka kutembea pamoja na Kristo ambaye ni njia, ukweli na uzima. Watu wanamtafuta Kristo Yesu hata bila ya kutambua. Kristo Yesu aliteswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, akasulubiwa, akafa na kuzikwa. Kristo Yesu alishuka kuzimu na siku ya tatu alifufuka kutoka wafu. Ufufuko wa Yesu ni kilele cha ukweli wa imani katika Kristo Yesu ambayo jamii ya kwanza ya Wakristo iliusadiki na kuuishi kama kiini cha ukweli; waliiendeleza kama msingi wa njia ya Mapokeo; wakaithibitisha kwa njia ya Maandiko Matakatifu ya Agano Jipya; na wakaihubiri kama sehemu muhimu sana ya Fumbo la Pasaka pamoja na Fumbo la Msalaba. Kristo amefufuka kutoka wafu, kwa kifo chake ameshinda dhambi n amauti na wafu wamepata uzima. Rej. KKK 571 – 658.

Kanuni ya imani ni muhtasari wa mafundisho makuu ya Kanisa
Kanuni ya imani ni muhtasari wa mafundisho makuu ya Kanisa

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 3 Aprili 2024, ametumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu anayewakirimia Wakristo furaha ya kuadhimisha Sherehe ya Pasaka, inayowakirimia walimwengu matumaini na maisha ya uzima wa milele. Katika kipindi hiki cha Oktava ya Pasaka, waamini waangaziwe na nuru ya Kristo Mfufuka katika maisha yao, hasa katika mchakato wa kutafuta na kuambata haki, ili kujenga ulimwengu unaosimikwa katika udugu wa kibinadamu. Baba Mtakatifu amewakumbusha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kwamba, Kristo Yesu ndiye tumaini la maisha yao, kwa mateso na kifo chake, ameweza kuzama katika kaburi ya dhambi zao na hivyo kuwakirimia maisha mapya, tayari kutembea katika mwanga wa Kristo Mfufuka. Anawaalika waamini kumtangaza na kumshuhudia Kristo Mfufuka kwa ari na moyo mkuu; kwa huruma na upendo, daima wakijitahidi kuwa waaminifu kwa Injili ya Kristo Yesu, Mwanga wa Mataifa. Amewataka vijana, wagonjwa, wazee na wanandoa wapya kukumbatia na kuambata ile furaha na amani ya Kristo Mfufuka kutoka katika sakafu ya nyoyo zao.

Kanuni ya Imani
03 April 2024, 14:04