Tafuta

Wanachama wa Chama Cha Msalaba Mwekundu nchini Italia, Jumamosi tarehe 6 Aprili 2024 wamekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko kama sehemu ya Jubilei ya Miaka 160 tangu kuanzishwa kwake. Wanachama wa Chama Cha Msalaba Mwekundu nchini Italia, Jumamosi tarehe 6 Aprili 2024 wamekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko kama sehemu ya Jubilei ya Miaka 160 tangu kuanzishwa kwake.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Jubilei ya Miaka 160 ya Chama Cha Msalaba Mwekundu Italia: Huduma Katika Dharura

Majitoleo yao yanachochewa na kanuni za ubinadamu, kutopendelea wala kuegemea upande wowote; uhuru, kujitolea, umoja na mshikamano na kwamba, hii ni ishara inayoonekana kwamba, ujenzi wa udugu wa kibinadamu ni jambo linalowezekana. Mwanadamu akipewa kipaumbele cha kwanza kuna uwezekano mkubwa wa kufanya kazi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, tayari kuvunjilia mbali kuta za uadui na kuthamini utakatifu wa maisha ya watu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Italia kiliundwa rasmi tarehe 15 Juni 1864 huko Milano kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa vita na mapigano, ambayo hata leo hii vita bado inaendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Chama cha Msalaba Mwekundu kikawa ni faraja kwa ajili ya huduma kwa waathirika wa vita bila ubaguzi wa utaifa, hali ya kijamii, dini, imani na mitazamo ya kisiasa. Hata leo hii, huduma ya Chama cha Msalaba Mwekundu ni muhimu sana kutokana na vita inayoendelea kusababisha mateso na mahangaiko ya watu; watu wanaotamani amani ya kudumu. Wanachama wa Chama Cha Msalaba Mwekundu nchini Italia, Jumamosi tarehe 6 Aprili 2024 wamekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko, ambaye amewapongeza kwa huduma makini kutokana na dharura mbalimbali zinazomwandama mwanadamu katika ulimwengu mamboleo.

Jubilei ya Miaka 160 ya Chama cha Msalaba Mwekundu Italia
Jubilei ya Miaka 160 ya Chama cha Msalaba Mwekundu Italia

Majitoleo yao yanachochewa na kanuni za ubinadamu, kutopendelea wala kuegemea upande wowote; uhuru, kujitolea, umoja na mshikamano na kwamba, hii ni ishara inayoonekana kwamba, ujenzi wa udugu wa kibinadamu ni jambo linalowezekana. Mwanadamu akipewa kipaumbele cha kwanza kuna uwezekano mkubwa wa kufanya kazi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Hii inawezekana kwenda zaidi ya migawanyiko na mipasuko, ili hatimaye, kuvunja kuta za uadui, kwa kushinda mantiki ya masilahi na nguvu ambayo hupofusha na kumfanya mwingine kuwa ni adui. Kwa mwamini kila mtu ni mtakatifu na kwamba, Mwenyezi Mungu anawapenda watoto wake wote na kwamba, kila mwanadamu ana haki zake msingi ambazo haziwezi kuondosheka. Wakihusishwa na imani hii, watu wengi na wema watakautana, wakitambua thamani kuu ya maisha na changamoto ya kuwatetea hasa zaidi walioko hatarini zaidi. Baba Mtakatifu anasikitika kusema kwamba, watoto walioathirika kwa vita kutoka Ukrain hawana tabasamu midomoni mwao kutokana na madhara ya vita.

Miaka 160 ya Huduma ya Dharura kwa Binadamu
Miaka 160 ya Huduma ya Dharura kwa Binadamu

Chama cha Msalaba Mwekundu katika maeneo ya vita kinatoa msaada mkubwa katika kudhibiti uharibifu unaosababishwa na majanga asilia kwa njia ya majiundo makini, huduma bora za afya sanjari na huduma kwa wakimbizi na wahamiaji. Hii ni kazi kubwa inayofanywa kwa upendo kwa watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, Chama cha Msalaba Mwekundu kitaendelea kuwa ni alama ya upendo kwa ndugu; upendo ambao hauna mipaka kwani unavuka mipaka ya kijiografia, kitamaduni, kijamii au kidini. Chama cha Msalaba Mwekundu kinafanya kazi sehemu mbalimbali za dunia. Hii ni dhamana na mtindo wa maisha. Kumbe kuna haja ya kumwilisha mshikamano wa kiulimwengu kwa kufanya kazi Kitaifa na Kimataifa na hivyo kuwafanya binadamu kutambulishana kama ndugu. Ili kufikia hali kama hii, ni vyema watu wakatambua kwamba wote ni ndugu wamoja pamoja na kuwa na mwono wa pamoja. Ni katika muktadha huu, kuna haja kwa Chama cha Msalaba Mwekundu kujikita katika mchakato wa ujenzi wa watu kukuna ili kuwawezesha watu kufahamiana zaidi.

Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Italia 1864-2024
Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Italia 1864-2024

Baba Mtakatifu anakaza kusema mwanadamu na utu, heshima na haki zake msingi na kwamba, hii ni changamoto ya kuendelea kukaa pamoja na maskini, wanaohitaji kuonjeshwa: weledi, ukarimu, majitoleo na sadaka hasa katika jamii ambamo ubaguzi wa rangi pamoja na tabia ya kutowathimini watu wengine inaendelea kwa kasi kubwa. Ujenzi wa urafiki wa kijamii ni sawa na udugu wa kibinadamu wote. Mtakatifu Paulo anasema “Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.” 1 Kor 9:22. Huu ni muhtasari wa utume wa Mtakatifu Paulo, Mwalimu wa Mataifa, ili aweze kushuhudia na kuwatangazia watu ile furana ya Injili. Huu ndio mtindo wa maisha unaotekelezwa na Chama cha Msalaba Mwekundu, kwa kujikita katika roho ya udugu ili kuwapunguzia watu mateso. Katika kipindi hiki cha Pasaka, Baba Mtakatifu anawaalika wajumbe wa Chama cha Msalaba Mwekundu kuomba neema ya kuwa ni mashuhuda na vyombo vya udugu wa kibinadamu na wajenzi wa amani; wadau katika kudumisha upendo na wajenzi wa ulimwengu unaosimikwa katika udugu na mshikamano.

Msalaba Mwekundu
06 April 2024, 15:00