Tafuta

Nchi Takatifu, mtazamo wa mbali wa mji wa Yerusalemu. Nchi Takatifu, mtazamo wa mbali wa mji wa Yerusalemu. 

Ujumbe wa Papa kwa wakatoliki wa Nchi Takatifu na kuwashukuru kwa kutumainia

Katika barua ya Baba Mtakatifu aliyowalekeza waamini wote wa Nchi Takatifu katika fursa ya maadhimisho ya Pasaka,anaonesha ukaribu,upendo na kuwatia moyo kutokama na kuteteseka zaidi kwa uchungu katika vita hivi vya kipuuzi.”Utufanye tusichoke kuthibitisha hadhi ya kila mtu,bila ubaguzi wa dini,kabila au utaifa kuanzia wale walio dhaifu zaidi hasa kuanzia na wanawake,wazee,wadogo na maskini.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 27 Machi 2024 ametuma barua yake aliyowaelekeza   waamini Wakatoliki na wengine wa  Nchi Takatifu  ambao wanajiandaa kuadhimisha Pasaka ya Bwana. Katika ujumbe huo anawalezea kuwa  amekuwa akiwawazia kwa muda na kuwaombea kila siku. Lakini sasa, katika mkesha wa Pasaka hii, ambayo kwao wanajua mengi kuhusu Mateso na bado machache kuhusu Ufufuko, amehisi haja ya kuwaandikia wao kuwaambia kwamba anawabeba moyoni mwake. “Niko karibu nanyi nyote, katika ibada zenu mbalimbali, wapenzi waaminifu Wakatoliki waliotawanyika katika eneo lote la Nchi Takatifu: hasa kwa wale ambao, katika hali hizi, wanateseka sana kutokana na  vita vya  kipuuzi, kwa watoto wananyimwa wakati ujao, kwa wale wanaolia na katika maumivu, kwa wale wanaohisi uchungu na kufadhaika.  

Pasaka ni moyo wa imani yetu

Pasaka, ambayo ni moyo wa imani yetu, ni muhimu zaidi kwenu ninyi mnaoiadhimisha a mahali ambapo Bwana aliishi, akafa na kufufuka tena: sio historia tu, lakini hata jiografia ya wokovu ingekuwepo bila Dunia ambayo mmeishi kwa karne nyingi, ambapo mnataka kukaa na ambapo ni bora kwenu kukaa. Papa amewashukuru kwa ushuhuda wao  wa imani, “ asante kwa upendo uliopo kati yenu, asante kwa sababu mnajua jinsi ya kutumaini dhidi ya matumaini yote. Ninapenda kila mmoja wenu ahisi mapenzi yangu kama baba, ambaye anajua mateso na shida zenu, hasa zile za miezi hii ya mwisho.” Aidha kwa kuongeza katika barua hiyo Papa anabinisha kuwa “Pamoja na mapenzi yangu, ninaomba muhisi yale ya Wakatoliki wote ulimwenguni! Bwana Yesu, Maisha yetu, kama Msamaria Mwema, anamimina mafuta ya faraja na divai ya matumaini kwenye majeraha ya mwili na roho zenu.”

Kuendelea kwa mivutano bila hatua ya amani ni hatari

Baba Mtakatifu Francisko akifiria juu ya hilo, amesema  kuwa:“hija niliyoifanya kati yenu miaka kumi iliyopita inakuja akilini; na ninajitengenezea maneno ambayo Mtakatifu Paulo VI, Mtangulizi wangu na mrithi wa  Petro kama mwanahija  katika Nchi Takatifu, aliwaambia waamini wote miaka hamsini iliyopita kuwa: “Kuendelea kwa hali ya mvutano katika Mashariki ya Kati, bila hatua madhubuti za kuelekea amani kuchukuliwa, ni hatari kubwa na ya mara kwa mara, ambayo inatishia sio tu utulivu na usalama wa watu hao - na amani ya ulimwengu wote - lakini pia. maadili fulani ambayo ni ya thamani sana, kwa sababu mbalimbali, kwa wanadamu wengi" (Waraka wa Kitume wa Nobis in Animo). Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa “, Jumuiya ya Kikristo ya Nchi Takatifu, si kwa karne nyingi tu, imekuwa walinzi wa Mahali pa Wokovu, bali imeshuhudia mara kwa mara, kwa njia ya mateso yake, fumbo la Mateso ya Bwana. Na, kwa uwezo wake wa kuinuka na kusonga mbele, ilitangaza na inaendelea kutangaza kwamba Msulubiwa amefufuka, kwamba kwa ishara za Mateso aliwatokea wanafunzi na kupaa mbinguni, akileta ubinadamu wetu unaoteswa lakini uliokombolewa na Baba.

Bwana uliye amani yetu utukomboe

Katika nyakati hizi za giza, ambazo inaonekana kwamba giza la Ijumaa Kuu linafunika Dunia yao  na sehemu nyingi za ulimwengu zilizoharibiwa na wazimu usio na maana wa vita, ambayo daima na kwa kila mtu ni kushindwa kwa umwagaji damu, wao ni mienge inayowashwa usiku. Wao  ni mbegu za wema katika nchi iliyojaa migogoro. Kwa ajili yao na pamoja nao Papa anaomba  “Bwana, wewe uliye amani yetu (rej. Efe 2:14-22), wewe uliyewatangaza wapatanishi kuwa heri (rej. Mt 5:9), ukomboe moyo wa mwanadamu kutoka katika chuki, kutokana na vurugu na kulipiza kisasi. Tunakutazama na kukufuata wewe, ambaye husamehe, ambaye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo (taza Mt 11:29). Ufanye kuwa hakuna mtu anayetubia mioyoni mwetu tumaini la kuinuka na kufufuka tena pamoja nawe, utufanye tusichoke kuthibitisha hadhi ya kila mtu, bila ubaguzi wa dini, kabila au utaifa, kuanzia wale walio dhaifu zaidi, hasa kuanzia na wanawake, wazee, wadogo na maskini.”

Hamko peke yenu tutawaacha

Papa Francisko aidha amependa kuwambia kuwa wa hawako peke yao na hawatawaaacha peke yao, lakini watabaki katika mshikamano na wao kupitia sala na upendo wa bidii, kwa kutumiania kuwa na uwezo wa kurudi hivi karibuni kwa mahujaji, kwa kutawazama machoni na kukukumbatiana, ili kuumega mkate wa udugu na kutafakari yale machipukizi ya matumaini yaliyoota kutokana na mbegu zao , yaliyotawanywa kwa uchungu na kukuzwa kwa subira. “Ninajua kwamba Wachungaji wenu, watawa wa kiume na kike kidini wako karibu nanyi: Ninawashukuru kutoka ndani ya moyo wangu kwa yale ambayo wamefanya na wanaendelea kufanya. Dhahabu ya umoja na ikue na kung'aa, katika lindi la mateso, pia pamoja na kaka na dada wa Madhehebu mengine ya Kikristo, ambao ningependa pia kuwaelezea ukaribu wangu wa kiroho na kuelezea faraja yangu. Ninawaweka  kila mtu katika maombi.” Papa Mtakatifu kwa njia hiyo amewabariki na kuwaombea ulinzi wa Bikira Maria, binti wa Ardhi yao. Amerudia kutoa mwaliko wangu kwa Wakristo wote ulimwenguni kuwafanya wahisi msaada wao thabiti na kusali bila kuchoka, ili watu wote wa Dunia yao pendwa hatimaye iwe na amani.

Barua ya Papa kwa waamini wa Nchi Takatifu
27 March 2024, 16:18