Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa misaada inayotolewa kwa Amerika ya Kusini, Kanisa linatarajia kuona matokeo, lakini Injili inakazia kutoa bila kutarajia malipo yoyote. Rej. Lk 6:35 Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa misaada inayotolewa kwa Amerika ya Kusini, Kanisa linatarajia kuona matokeo, lakini Injili inakazia kutoa bila kutarajia malipo yoyote. Rej. Lk 6:35  (ANSA)

Ujumbe wa Papa Francisko Kwa Wadau wa Misaada Amerika ya Kusini: Sadaka na Ukarimu

Takrima: Umuhimu wa kutoa msaada kwa Makanisa bila kutarajia malipo yoyote, kwani Mungu ndiye mtoaji na binadamu ni msimamizi tu wa bidhaa inayotolewa, changamoto na mwaliko wa kujenga mahusiano na mafungamano na maskini kama Kristo Yesu alivyofanya katika sadaka yake Msalabani na katika Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu anaendelea kujitoa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wake; kielelezo cha upendo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Tume ya Kipapa kwa Ajili ya Amerika ya Kusini, “The Pontifical Commission for Latin America (CAL)” kuanzia tarehe 4 hadi 8 Machi 2024 inaendesha mkutano wa Taasisi na Mashirika ya Misaada kwa Makanisa ya Amerika ya Kusini huko Bogotà nchini Colombia. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe aliomwandikia Kardinali Robert Francis Prevost, O.S.A., Rais wa Tume ya Kipapa Kwa Ajili ya Amerika ya Kusini anakazia: Takrima: Umuhimu wa kutoa msaada kwa Makanisa bila kutarajia malipo yoyote, kwani Mungu ndiye mtoaji na binadamu ni msimamizi tu wa bidhaa inayotolewa, changamoto na mwaliko wa kujenga mahusiano na mafungamano na maskini kama Kristo Yesu alivyofanya katika sadaka yake Msalabani na katika Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu anaendelea kujitoa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wake; kielelezo cha upendo unaovumilia, hufadhili, upendo hauhusudu; upendo hautakabari wala kujivuna, bali hujenga umoja na kufanya yote kuwa ni mapya! Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa misaada inayotolewa kwa Amerika ya Kusini, Kanisa linatarajia kuona matokeo, lakini Injili inakazia kutoa bila kutarajia malipo yoyote. Rej. Lk 6:35, kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye mtoaji wa yote na mwanadamu ni msimamizi tu na wala hapaswi kujisifu, bali kujikita katika fadhila ya unyenyekevu. Mwenyezi Mungu amemkarimu mwanadamu: uhai, kazi ya uumbaji, akili na nia ya kutawala hatima ya maisha yake. Mwenyezi Mungu amejitoa kwa ajili ya binadamu wote kama inavyojidhihirisha katika historia ya ukombozi inayofikia hatima yake kwenye Fumbo la Msalaba na uwepo wake katika Sakramenti ya wokovu na katika Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na katika zawadi ya Roho Mtakatifu. Huu ndio uelewa kwamba, binadamu ni msimamizi wa bidii ya Mwenyezi Mungu na kamwe, wasiwe ni watumwa wa mali na fedha, kwa kutiishwa na woga na kuanza kuikita mioyo yao kwenye hazina na usalama wa uwongo kiuchumi; ufanisi wa kiutala, udhibiti wa maisha bila matatizo.

Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili
Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kusema kwamba, tangu mwanzo wa kazi ya uumbaji, Kristo Yesu ameendelea kujitoa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya binadamu, akichukua ndani mwake: Udhaifu na dhambi zao; hali ya kutokuwa na msimamo wa maisha; mwaliko na changomoto ni kuendelea kubaki waaminifu. Waendelee kuwabeba ndani mwao wale wanaoteleza na kuanguka kando ya njia, wanaoteseka kwa ukoma au taabu nyingine za maisha; kwa kutokuwa na msimamo thabiti wa maisha. Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mapendo, anasamehe bila kuchoka hata kidogo. Katika Fumbo la Ekaristi Takatifu, waamini wanampokea Kristo Yesu mzima. Huyu ndiye Kristo Yesu “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.” 2Kor 8:9. Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha tafakari yake kuhusu takrima kwa kusema, hizi ni jitihada za kutaka kuiga njia ya Kristo Yesu ya kujitoa na kujisadaka, kielelezo cha upendo wake usiokuwa na kifani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, upendo: “huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.” 1 Kor 13:4-7. Kwa hakika upendo ni chachu ya ushirika na hufanya mambo yote kuwa mapya. Re. Ufu 21:5.

Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao
Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao

Kristo Yesu ni kielelezo cha sadaka na majitoleo yote na kwamba, kukumbatia na kuambata Msalaba ni kujiunganisha na Kristo Yesu ili kuwatangazia na kuwashuhudia maskini Habari Njema ya Wkovu kwa kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao; na vipofu kuona na uhuru kwa wale walionewa. Na kwa maneno mengine hizi ni jitihada za kugusa jeraha za maskini wenye thamani kubwa mbele za Mungu, kwa kumpatia nuru, kuimarisha miguu yake katika njia za haki pamoja na kusafisha taabu zake, ili hatimaye, kutekeleza mradi wa upendo alionao Kristo Yesu kwa ajili ya maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Hatimaye, Baba Mtakatifu Francisko amewakabidhi wajumbe wa mkutano huu chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria ili awaongoze kama alivyofanya kwenye Arusi ya Kana ya Galilaya, ili divai mpya kutoka kwa Kristo Yesu iweze kuwafikia watu wote.

Amerika ya Kusini

 

05 March 2024, 15:00