Tafuta

2024.03.25 Jumuiya  ya Wanaigeria waishio Roma wamekutana na Papa Francisko. 2024.03.25 Jumuiya ya Wanaigeria waishio Roma wamekutana na Papa Francisko.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa,Jumuiya ya Wanaigeria Roma:shukrani,utajiri katika utofauti na mazungumzo!

Papa akikutana na jumuiya ya wanaigeria waishio Roma katika fursa ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzisha jumuiya hiyo amewakabidhi tafakari ya mambo matatu:shukrani,utajiri katika utofauti na mazungumzo.Amewahimiza wawe wanafunzi wamisionari,wenye kutoa shukrani kwa mungu na wamfuate na kutangaza imani yao kwa bidii wakichangi ujenzi wa ulimwengu wa haki na hadhi zaidi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 25 Machi 2024, amekutana karibu na wanajumuiaya 800 wa Nigeria waishio Jijini Roma  ambapo ameanza na salamu za dhati na kuwakaribisha wote  mliokusanyika hapa kusherehekea miaka ishirini na mitano ya uwepo wa jumuiya ya Kikatoliki ya Nigeria jijini  Roma. Baba Mtakatifu amesema kuwa tarehe 25 Machi inatukumbusha jambo jingine muhimu sana la kiliturujia, yaani, maadhimisho ya Kupashwa Habari kwa Bikira Maria ambapo  mwaka huu, hata hivyo, kutokana na Juma Takatifu, Maadhimishohayo yamehamishiwa siku nyingine. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo amependa kutoa mambo mawili kwamba kuhusiana na hilo;  la kwanza  ambalo linatukumbusha juu ya Umwilisho wa Bwana; na la pili linatujulisha juu ya mafumbo ya Pasaka ya wokovu, kwamba yanayotuonesha  Neno, aliyefanyika mwili na akaishi kati yetu(taz Yh 1: 14). Na Neno aliishi, akafa na kufufuka ili kuleta upatanisho na amani kati ya Mungu na wanadamu na alitupatia  maisha yake!

wanaigeria waishio ROMA
wanaigeria waishio ROMA

Katika suala hili, Baba Mtakatifu amependa kuakisi kwa kifupi vipengele vitatu ambavyo aliviona kuwa muhimu kwa maisha ya jumuiya yao: shukrani, utajiri katika utofauti na mazungumzo. Kwanza kabisa, amewashukuru kwa kila kitu ambacho wamefanya na kuendelea kufanya, wakishuhudia ujumbe wa furaha wa Injili. Baba Mtakatifu aidha anaunga nao katika kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya vijana wengi wa Nigeria ambao wamesikia wito wa Bwana kwa ukuhani na maisha ya kuweka wakfu na kuitikia kwa ukarimu, unyenyekevu na uvumilivu. Kulikuwa na baadhi  yao hapo mapadre vijana na watawa vijana. Kwa hakika, kila mfuasi wa Yesu, kulingana na wito wake hususani, amekabidhiwa daraka la kumtumikia Mungu na jirani yake kwa upendo, na kumfanya Kristo awepo katika maisha ya ndugu zake. Baba Mtakatifu amewahimiza daima kuwa, wawe wanafunzi wamisionari, wenye kushukuru kwamba Bwana amewachagua wao kumfuata na amewatuma kutangaza imani yao kwa bidii na kuchangia katika ujenzi wa ulimwengu wa haki na utu zaidi.

Wanajumuiya wanaigeria waishio Roma
Wanajumuiya wanaigeria waishio Roma

Pili, Papa amefafanua juu ya utajiri katika utofauti. Juu ya hilo alipenda kusema kwamba tofauti za makabila, mila na tamaduni katika taifa lao hazileti tatizo, bali ni zawadi inayoimarisha muundo wa Kanisa na wa jamii nzima na inaturuhusu kukuza maadili ya kuelewana na kuishi pamoja. Ni matumaini ya Papa  kwamba jumuiya yao jijini  Roma, katika kuwakaribisha na kuwasindikiza na waamini wa Nigeria na waamini wengine, daima wanafanana na familia kubwa iliyojumuika, ambapo kila mtu anaweza kutumia vipaji vyake mbalimbali, ambavyo ni matunda ya Roho Mtakatifu, ili kukusaidia na kuimarisha kila mmoja katika nyakati za furaha na huzuni, mafanikio na shida. Kwa njia hii, wataweza kupanda mbegu za urafiki wa kijamii na maelewano kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Baba Mtakatkfu aliongeza kuwa kusitiza kuwa “Na kuwa waangalifu na hatari: hatari ya kufungwa; sio kuwa wa ulimwengu wote, lakini kujifungia ndani - ikiwa mnaweza kutumia neno - kutengwa kwa kikabila. Hiyo hapana. Mizizi yenu ya ukaribu, jitenge  mbali katika mtazamo huo  wa kikabila na usio wa ulimwengu wote, usio wa jumuiya. Jumuiya ndiyo; ukabila, hapana. Na hii ni muhimu sana kufanya.Na hii inatumika kwa sisi sote, kwa kila mtu, kila mmoja, kulingana na nafasi yake. Lakini kuwa wa ulimwengu wote na sio kujifungia katika tamaduni ya mtu binafasi. Ni kweli, utamaduni wa mtu ni zawadi, lakini si kujifunga bali kujitoa. Katika ulimwengu wote”.

Papa na Jumuiya ya Wanaigeria Roma
Papa na Jumuiya ya Wanaigeria Roma

Na hatimaye, Baba Mtakatifu Francisko amefafanua kipengele cha mazungumzo. Kwa bahati mbaya, maeneo mengi ya dunia yanakabiliwa na migogoro na mateso na Nigeria pia inapitia nyakati ngumu. Akiwahakikishia maombi yake ya usalama, umoja na maendeleo ya Taifa lao kiroho na kiuchumi, amewaalika kila mmoja kuhimiza mazungumzo na kusikilizana kwa moyo wazi, bila kumtenga mtu yeyote katika ngazi ya kisiasa, kijamii na kidini. Jumuisha, mazungumzo, unganisha, kila mara [kuanzia] na  utambulisho wa mtu mwenyewe. Na wakati  huo huo, Papa amewatia moyo wawe watangazaji wa huruma kuu ya Bwana, wakifanya kazi ya upatanisho kati ya kaka zao wote na dada zao, wakichangia katika kupunguza mzigo wa maskini na wahitaji zaidi na kufanya mtindo wa Mungu kuwa wenu. Na ni mtindo gani  wa Mungu? Ukaribu, huruma na upole. Wasisahau hilo. Mtindo wa Mungu ni ukaribu, huruma na upole. Kwa njia hii Wanigeria wote wataweza kuendelea kutembea pamoja katika mshikamano na maelewano ya kindugu.

Jumuiya ya Wanaigeria Roma
Jumuiya ya Wanaigeria Roma

Papa amewashukuru kwa mara nyingine tena kwa uwepo wao  katika mji huu, katika moyo wa Kanisa. Ni neema ya majaliwa ambayo inawaptia fursa ya kukuza ufahamu wao wa wito wao wa ubatizo wa kuishi daima kama wanafunzi waaminifu wa Bwana, kujitolea kwa huduma ya Mungu na watu wake watakatifu kwa upendo ambao Yesu anatuomba, na kusherehekea utajiri wa urithi wao wa kipekee kama Wanigeria. Kuna utajiri mkubwa: kutoa. Papa amewakabidhi jumuiya yao kwa ulinzi wa upendo wa Bikira Maria, Malkia na Mlinzi wa Nigeria, na amewabariki kwa moyo wote. Na tafadhali wasisahau kumuombea.

Papa akutana na Jumuiya ya Wanaigeria waishio Roma
25 March 2024, 12:08