Tafuta

2024.03.25 Mkutano wa kuwasilisha zira ya kitume ya Papa huko Venezia(28 Aprili). 2024.03.25 Mkutano wa kuwasilisha zira ya kitume ya Papa huko Venezia(28 Aprili). 

Ziara ya Papa Venezia:kukutana na wafungwa,vijana na wasanii!

Katika ziara ya Papa kutakuwa na hotuba 3 na mahubiri wakati wa takriban saa 6 katika jiji la maji.Papa atatembelea kituo cha wafungwa cha wanawake kwenye Kisiwa cha Giudecca na kuwasalimia wasanii wa Biennale.Ataadhimisha Misa katika uwanja wa Mtakatifu Marko kabla ya kuingia kwenye Basilika na kuheshimu masalia ya mtakatifu mlinzi.Patriaki Moraglia:Shukrani kwa Baba Mtakatifu kwa sababu alitaka kuweka makini Veneto na Kaskazini-Mashariki,kuanzia mji wetu.

Alvise Sperandio – Venezia  na Angella Rwezaula – Vatican.

Mkutano gerezani na wafungwa na kwa ajili ya uzinduzi wa banda la Vatican la Vatican lenye kauli mbiu ya  Afya; hatimaye kupita chini ya  daraja na pantoni kwenda katika Uwanja wa Mtakatifu Marko kwa ajili ya  Misa kuu, ikifuatiwa na sala ya kibinafsi kwenye kaburi la Mtakatifu Marko Mwinjili, mtakatifu msimamizi wa  Venezia  na watu wa Venezia. Hizi ni nyakati tatu zitakazoadhimisha takriban saa sita za ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko huko Venezia, inayotarajiwa kufanyika Dominika  tarehe 28 Aprili 2024  unayoongozwa na  kauli mbiu: “Kukaa na umoja katika upendo wa Kristo” na inayohamasishwa na ukurasa wa Kiinjili kuhusu tawi na mzabibu. Mpango huo rasmi umechapishwa  tarehe 25 Machi 2024 na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican na kuwasilishwa katika Chumba cha Tintoretto cha Kasri na  Patriaki wa  Upatriaki wa Venezia, Kardinali  Francesco Moraglia  ambaye alisema kuwa katika siku ile ni ya mfano ambao unachukuliwa kuwa “siku ya kuzaliwa ya Venezia”, ambayo kwa kawaida inaaminika kuwa ilianzishwa mnamo mwaka 421.

Salamu kwa wafungwa wa Giudecca

Kulingana na mpango rasmi, Papa ataondoka saa 12.30 alfajiri kwa helicoporta ya Vatican na kutua karibu saa 2.00 kamili  asubuhi katika uwanja wa ndani wa Nyumba ya Gereza la Wanawake huko  Venezia, kwenye Kisiwa cha Giudecca, ambapo atakaribishwa na Patriaki Francesco Moraglia, msimamizi Maria Milano Franco D'Aragona, mkurugenzi Mariagrazia Felicita Bregoli na kamanda wa Polisi wa Magereza, Lara Boco. Katika ua wa ndani la gereza hilo, saa 2.15 asubuhi, Papa Francisko atakutana na wafungwa na kutoa hotuba. Wafanyakazi wa utawala, maafisa wa Polisi wa Gereza na watu wa kujitolea pia watakuwepo. Mwishoni, Papa atasalimia binafsi wafungwa takriban 80.

Mkutano na wasanii na vijana

Baada ya mkutano katika Uwanaja wa Ndani ya Gereza hilo, karibu 2.45 asubuhi, Papa atafikia Kanisa la Magdalene (Kanisa la Magereza), ambapo atakaribishwa na Kadinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, pamoja na msimamizi wa Banda la Vatican  huko Venezia katika Toleo la Kisanii la  Biennale. Kardinali De Mendonça atatambulisha kwa salamu mkutano wa Papa pamoja na wasanii wanaoshiriki katika Maonesho hayo, saa 3.00 asubuhi, katika Kanisa la Maddalena. Pia katika hafla hiyo Papa atatoa hotuba na kusalimiana na mamlaka na wasanii. Saa 3.30 asubuhi ataondoka Kisiwa cha Giudecca na kufikia Basilika ya Mtakatifu  Maria wa Afya kwa boti ya walinzi. Kwa hakika, mkutano na vijana wa Venezia na majimbo ya Mkoa wa Veneto unapangwa katika uwanja ulio mbele ya Basilika, mahali muhimu  sana kwa vijana kutokana na kwamba kila mwaka hufanya hija yaoa huko kwa ajili ya sikukuu kuu ya Novemba 21 na sala mbele ya Picha  ya Bikira inayojulikana kama Mesopanditissa (yaani mbeba amani). Papa  Francisko atahutubia hotuba yake, kisha, akifuatana na ujumbe wa vijana, atavuka daraja na pantoni linaloungana na Uwanja wa Mtakatifu Marko. Katika mlango wa Uwanja huo kutakuwa na Luca Zaia, Mkuu wa  Mkoa wa Veneto; Darco Pellos, gavana wa Venezia, na meya Luigi Brugnaro ambao walichukua nafasi kubwa katika kuandaa ziara hiyo kwa mazungumzo ya karibu na Kadinali Tolentino de Mendonca, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.

Misa katika viwanja vya Mtakatifu Marko

Ili kufunga ziara ya Papa katika mji wa maji, Misa ya saa 5.00 asubuhi katika Uwanja wa Mtakatifu Marko itafanyika lakini ikitangulia na salamu ya Papa kuwazungukia waamini watakaokuwapo na pia hatimaye baada ya misa kufuata  sala ya Malkia wa Mbingu. Takriban waamini 7,500 watakuwepo na pamoja na wengine 1,500 watakaosimama katika Uwanja wa Mtakatifu Marko: waamini wataweza kuweka nafasi bila malipo kupitia parokia na watakuwa na pasi yenye Msimbo wa QR, kidogo kama ilivyokuwa hapo awali, kwenye  tukio la Mwaka wa Imani na kutangazwa kwa mwenyeheri Monsinyo Luigi Caburlotto (upatikanaji utafanyika kupitia milango maalum).

Shughuli hiyo pia itaoneshwa moja kwa moja kwenye televisheni na kupitia skrini kubwa. Mwishoni mwa sherehe, baada ya shukrani kwa Patriaki Moraglia, Papa ataingia kwa faragha ndani ya Basilika iliyowekwa wakfu kwa Mtakatifu Msimamizi ili kuheshimu masalia yake, akifuatana na maelezo ya wimbo wa Venezia wa Ave Maris Stella na Ravetta. Kisha, akiwa kwenye boti la walinzi  atafikia katika heliport ya F. Naval College, Morosini huko Mtakatifu Elena. Hapa atawaaga viongozi wa kiraia na kidini waliomkaribisha. Kuondoka huko kumeratibiwa saa moja jioni, na kutua saa 2.30 usiku kwenye uwanja wa helikopta wa Vatikani.

Shukrani kwa Papa kutoka kwa Patriaki Moraglia

Akiwasilisha ziara hiyo, Patriaki Moraglia alimshukuru Papa Francisko “kwa sababu alitaka kutilia maanani Veneto na Kaskazini-Mashariki, kuanzia Venezia . Lakini pia kwa chaguo lililofanywa la kujiunga pamoja na Banda la Vatican, ambalo linahusu mada anayopendwa na Papa: sanaa inayoonekana kwa macho ya wale wanaobeba mabegani mwao, katika historia yao, mizigo, udhaifu, majeraha ya maisha. Na kisha kutakuwa na nyakati zingine muhimu: mkutano na wafungwa na wasanii; kisha vijana wa Upatriaki wenye uwakilishi wa majimbo 15 ya Triveneto; kisha kifungu cha Uwanja wa Mtakatifu Marko.” “

Mwishoni mwa Sherehe za Ekaristi, ambapo maaskofu wote wa Baraza la Maaskofu waJimbo la Triveneto watakuwepo, kutakuwa na wakati ambapo Baba Mtakatifu atauheshimu mwili wa Mtakatifu Marko Mwinjili, mtakatifu mlinzi wa Venice na ya watu wote wa Venezia”,  Patriaki Moraglia alisema kwamba mwishoni mwa ziara ya hivi karibuni ya ad limina na maaskofu wa Triveneto, alimwomba Papa “kusema neno hasa kwa vijana: alitabasamu na kuniambia nizungumze kuhusu hilo mara moja na shirika, kwanza kabisa nikiwa na Monsinyo Piacenza. Pia ninatumaini kwamba ujumbe mzito unatoka  Kanisa ulimwenguni kama ukweli unaotaka kujumuisha. Na shauku  ambayo  Papa Francisko alinieleza ya kuwasiliana na watu kadiri iwezekanavyo itimie. Ninawaalika Jimbo kujiandaa vyema kwa mipango  na Papa, hasa kwa sala.”

Ndoto imetimia

Diwani wa Manispaa ya Venezia, Simone Venturini, akileta salamu za Meya Brugnaro, alionesha kuridhika sana kwamba: “Kwa Venezia, kumkaribisha Baba Mtakatifu ni ndoto kubwa, wakati unaokusudiwa kuingia katika historia ya jiji: Papa alifanya hivyo. sio tu kiongozi wa Kanisa Katoliki, lakini pia ni mkuu wa nchi na mwanafikra wa ajabu ambaye anatupatia chakula kizuri cha kufikiria juu ya mada na shida za zama zete.” Mipango mingine ya Papa katika nchi ya Italia ni kwamba Baba Mtakatifu Francisko atarejea Kaskazini-Mashariki mwa Italia Dominika tarehe 18 Mei huko Verona na kisha Dominika tarehe 7 Julai 2024 huko Trieste Italia.

26 March 2024, 17:00