Tafuta

2024.03.27 Papa alitume ujumbe mfupi kwa njia ya video kwa wafungwa wa Barcellona-Hispania 2024.03.27 Papa alitume ujumbe mfupi kwa njia ya video kwa wafungwa wa Barcellona-Hispania 

Papa kwa wafungwa wa Barcellona:msiogope,tembea kuelekea upeo wa Yesu

Papa Francisko alituma ujumbe mfupi kwa njia ya video kwa wafungwa wa Gereza la Quatre Camins,huku akiwaalika kuwa na subira katika kutatua matatizo yao,kujumuika kwa furaha katika jamii na daima kumwangalia Yesu ambaye anajihatarisha ili kutuokoa.

Sebastián Sansón Ferrari  na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko alitoa maneno yake kwa wafungwa wa Kituo cha Magereza cha Quatre Camins huko Barcellona Hispania, katika ujumbe kwa njia ya video uliorekodiwa wakati wa mkutano mjini Vatican na Kadinali Juan José Omella na kuchapishwa tarehe 25 Machi 2024  na jarida la Catalunya la Kikristo ambalo lilizindua upya njia za kijamii. Katika ujumbe huo Papa anasema: “Nataka mjue kuwa niko karibu na nyiny, kwamba ninawaombea, lakini ninataka mjue kuwa mnaye mtu ambaye alijiweka katikati ya  kila mtu, na ambaye alichukua hatari ya kujihatarishwa kwa kila mtu.”

Kwa njia hiyo katika ujumbe huo mfupi Papa alibainisha kwamba aliguswa kusikia wafungwa wakizungumza na alisisitza kuwa na  usikivu wake maalum kwa watu wanaojikuta gerezani. Kwa hakika, tangu mwanzo wa upapa wake, amechagua maeneo yaliyo katika kile anachokiita pembezoni mwa  kuwepo katika kuadhimisha Misa ya  Alhamisi Kuu, akianza na taasisi za magereza. Pia hata mwaka huu 2024, Baba Mtakatifru Francisko anatazamia kwenda  katika gereza la wanawake la Rebibbia jijini Roma.

Msalaba unaoonesha Yesu akija kututafuta

Katika video hiyo, Papa Francisko aliwaonesha wafungwa msalaba mzuri wa mbao ambao ndani yake Yesu anaonekana akiwa amepiga magoti, huku mkono mmoja ukinyooshwa kuelekea kwa Baba na mwingine akiwa amemshika mtu, akiwanyooshea ili kuwaleta karibu na Mungu, alisema Papa, huku  akionesha kile ambacho Bwana ametufanyia na kwamba   anatualika kukizingatia kuwa: “Yesu anajihatarisha na kwenda kututafuta na kutuondoa katika shida yetu, nje ya ukweli wetu. Yesu ndiye anayejihatarisha: akishika mkono wa Baba, anajihatarisha kutuokoa”, alisisitiza Askofu wa Roma. Kwa hiyo alihimiza:“mssiogope, muwe na subira na kusonga mbele, msipoteze upeo wenu” na “kusuluhisha polepole matatizo ya kila mtu na kufaa katika jamii kwa furaha.” Kisha aliwahakikishia sala zake na kuwaomba wamwombee.

Kama ilivyoripotiwa, kutoka huko Katalonya ni kwamba Kadinali Omella alieleza kwamba vijana waliokuwa gerezani walishiriki katika mafungo ya kiroho ya Effetà ambayo yaliwaruhusu kukutana na Yesu na kuomba.  Kardinali pia alisema alishangazwa na msalaba uliowasilishwa na Papa: “Picha nzuri kama nini! Kristo, akijua jinsi ya kubeba maumivu yake, huwafikia maskini, kuwaleta kwa Baba!”

Ujumbe wa Papa kwa wafungwa wa Barcellona
27 March 2024, 16:37