Tafuta

Papa apokea matunda ya kazi ya mikono ya wanawake wafungwa!

Papa aliongoza misa ya Alhamisi Kuu katika Gereza la Wanawake la Rebibbia,Roma mbele ya washiriki 200 wafungwa wa hali miongoni hata mwanamke mwenye mtoto wa miaka 3.Ni wa rika tofauti na madhehebu tofauti.Walimzawadia kikapu cha mboga wanazozalisha katika bustani zao pia rosari na stola mbili kutoka maabara mbili za ushonaji na ufundi wa kazi za mikono.

Na Angella Rwezaula – Vatican

Chini ya muundo wa mvutano wa Gereza la wanawake la Rebibbia, nje kidogo ya mji wa Roma, ndipo Baba Mtakatifu Francisko alichagua  mwaka huu 2024  kuadhimisha Misa ya Coena Domini, yaani Karamu Kuu, katika siku ya Alhamisi kuu, tarehe 28 Maachi 2024 na wafungwa. Kwa njia hiyo alasiri Papa alipowasili alipokelewa na wafungwa hao pamoja na walinzi, watu wajitolea na watawa waliokuwa wamevaa alama ya “Ibara ya 17” (WafransikanI na wadominikani waliowekwa wakfu, wa Ordo Virginum) ambao wanatekeleza utume wao ndani ya kuta hizo, wakisambaza vijitabu, kupanga viti na kikapu chenye bidhaa za kutoa zawadi za mboga ambazo wao wenyewe wanalima katika bustani yao ndani ya Gereza.

Papa na wafungwa
Papa na wafungwa

Mara baada ya Misa, Mkuu wa Gereza la Wanawake, Nadia Fontana alimsalimia Baba Mtakatifu, kwa furaha na hisia kuchukua nafasi ya kueleza na kumpatia sio hata moja, lakini shukrani nyingi: “kwanza kabisa, asante iliyozidishwa na idadi ya wale wanaoishi mahali hapa na ambao wanateseka kwa kunyimwa uhuru. Kuna wafungwa 360 na mtoto mmoja.” Uwepo wake hapa, leo, ni kwa kila mmoja wao miale ya jua ambayo inachangamsha moyo na kufufua matumaini ya kuweza kuanza tena, hata wanapojikuta wanaanza kutoka mwanzo. Asante, Baba Mtakatifu, kwa niaba ya wale wote - wanaume na wanawake - ambao katika nyadhifa tofauti na kwa kazi tofauti wanafanya kazi katika Taasisi hii, wakiwekeza sadaka na taaluma.”

Picha aliyowazawadia
Picha aliyowazawadia

Mkuu wa Gereza la Wanawake hao, aliendelea kusisitiza kuwa “Asante kwa niaba ya watu wote wenye mapenzi mema ambao, bila malipo, wanafanya kazi mahali hapa ili kuweka matumaini, ubunifu na kuleta upendo wa Kanisa linalotaka kuwa Mama. Aidha alisema wanahimiza jamii ambayo bado inathubutu kuweka dau kwa mtu zaidi ya makosa na maigizo ya maisha.” Asante yangu sio tofauti lakini imeunganishwa na kila moja ya haya "asante": kwa kila neno na ishara ambayo umetupatia. Ni kwa mara ya kwanza kwa Papa kuingia kwenye milango ya nyumba hii ya Gereza: inaitwa nyumba ambayo umeingia leo kama mhujaji wa matumaini kwa kuleta ujumbe wa amani.” Kwa hivyo tunakuomba usisite kuja kututembelea na kutusalimia wakati wowote unapotaka: kila wakati utakuta mlango wazi na sote tuko tayari kukukaribisha kama ulivyotukaribisha leo, na kutufanya tujisikie nyumbani. Heri ya Pasaka, Baba Mtakatifu.                                                  

Mara baada ya hotuba yake Mkuu wa Gereza hilo alimwambia Baba Mtakatifu jinsi ambavyo wafungwa wao walivyokuwa na zawadi ya kumpatia ambayo angeweza kuendelea kuwakumbuka. Hicho kilikuwa ni kikapu cha bidhaa wanazozalisha hapo, kwenye shamba lao wanaofanya kazi katika bustani hiyo. Kwa hiyo Papa alipokea matunda yote ya kwanza ya wakati huu. Vile vile wanayo maabara ya kutengeneza vitu kama mikufu na hivyo wanatengeneza rozari za rangi ya upinde wa mvua ilyotenenezwa na nido ya mkono na lulu. Walitaka kwamba liwe wazo la asili kabisa.  Na pia pamoja na wafungwa wa kile wanaofanya kazi katika maabara ya kushona na hizo ziko mbili moja ambapo kuna mwalimu anayefundisha kushona na nyingine kiukweli wanashona na walimtengenezea stola mbili zenye sura ya mikono miwili ya kukaribisha, na alizeti kuelekea jua na pia mbegu, ili kutofautisha kuwa wao ni Taasisi ya Rebibbia ya kike.

Baada ya kumkabidhi hizo zawadia Papa Francsiko naye alisema: Ninataka kuwaachia katika nyumba hii zawadi ya picha ya Mama ambayo walinizawadia iliyochorwa na haraka nimefikiria ninyi. Ninawachia ninyi.

Kama tulivyosema hapo awali, wafungwa wa kike wa Rebibbia ni karibi 200 kati ya 300 wanaondelea kulipa adhabu yao ya mwisho(wengine ni wazee au wagonjwa sana hata kukosa kushiriki) miongoni mwao ni mama kijana na mtoto anaitwa Jairo Massimo wa miaka 3 ( Yeye kwa yupo Magereza ya Rebibbia kwa miezi 9). Walifika mmoja baada ya mwingine katika mstari kumsalimia Papa Francisko.  Hawa ni Wanigeria, Waperu, Wafilipino, Wasri Lanka, Waethiopia, Wabulgaria, Wakiukraine, Waitaliano Warusi na hata Mchina mmoja. Wengi wa wanawake hawa ni wa kabila la Waromania.

Stola ya pili
Stola ya pili

Na wamegawanywa katika majina ya sehemu kwa mfano za  usalama wa kati, kwa uhalifu kama vile wizi, ujambazi au biashara ya dawa za kulevya; usalama wa hali ya juu, kama vile  viongozi wanaokuza vyama kihalifu vya mafia, wakiwemo baadhi ya watu wa ukoo maarufu unaojulikana. Na hatimaye chumba  kingne cha wagonjwa, chenye wafungwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya akili. Nyuso zote tofauti: vijana, wazee, dhaifu na wanyonge. Walionekana watafuna gum, wamengine wamevaa suti za rangi, viatu au hata slippers. Baadhi ya vijana wadogo wamesuka nywele kwa ajili ya hafla hiyo, wengine wamevalia fulana nyeupe yenye uso wa Papa, karibu wote wakiwa na rozari ya plastiki shingoni mwao.

Papa limfariji mama anayelia
Papa limfariji mama anayelia

Kabla ya kuingia katika chumba cha wagonjwa, jambo lisilotarajiwa lilitokea: mwanamke mmoja  pia wa asili ya Kiafrika, akiungwa mkono na wasaidizi wawili, alipiga kelele na kulia sana machozi yasiyoweza kudhibitiwa. Tayari alikuwa ameshaeleza usumbufu wake wakati wa Misa kwamba: “Ninateseka sana, siwezi kuvumilia tena, ninateseka sana, alisema katikati ya kwikwi kwa Papa Francisko ambaye alimbembeleza na kujaribu kumtuliza, kisha kumwekea mkono kwenye paji la uso na kumhakikishia maombi, kuwaalika yeye pia kuomba.

Papa alpokea zwadi kutoka kwa wafungwa wa kike
29 March 2024, 11:30