Tafuta

Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa mwaka 2024 imeandaliwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa mara ya kwanza (Ni picha ni Magofu ya mateso ya wakristo wa kwanza jijini Roma). Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa mwaka 2024 imeandaliwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa mara ya kwanza (Ni picha ni Magofu ya mateso ya wakristo wa kwanza jijini Roma).  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kwa mara ya Kwanza tafakari ya Njia ya Msalaba imeandikwa na Papa Francisko

Katika maombi pamoja na Yesu katika njia ya Msalaba ndiyo tema ya tafakari itakayoambatana na vituo kumi na vinne vya Colosseo.Taarifa kutoka vyombo vya habari Vatican:'Ni kitendo cha kutafakari na kiroho,Yesu akiwa katikati,katika muktadha wa Mwaka wa Sala uliotangazwa na Papa.Ni rejeo la matukio ya sasa ambayo sio ya moja kwa moja lakini mapana zaidi.Kwa sasa hakuna mabadiliko kuhusiana na uwepo wa Papa,Palatina ikilinganishwa na ilivyotarajiwa.'

Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.

Baada ya maaskofu, Watawa, familia nzima, vijana, wanafunzi, wanandoa, wamisionari, wahamiaji, wakimbizi wa kivita, mwaka huu 2024 ni Papa mwenyewe anayetayarisha tafakari ya Njia ya Msalaba ya siku ya Ijumaa Kuu katika njia ya Uwanja wa Colosseum(Magofu ya kizamani ya mateso ya Wakristo wa kwanza. Hii ni kwa mara ya kwanza katika kiti cha upapa cha Jorge Mario Bergoglio(Papa Francisko). Kusali pamoja na Yesu katika njia ya Msalaba ndiyo tema iliyochaguliwa kwa ajili ya tafakari itakayoambatana na vituo kumi na vinne vinavyokumbuka njia ya  Yesu kuelekea Golgotha. Tena inayotufanya kuelewa tabia ya “kutafakari kwa kina juu ya maandiko hayo ambayo, kama vile Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican  ilivyosisitiza, kwamba  itakuwa “Kitendo cha kutafakari na kiroho, na Yesu katikati.” Yeye atembeaye katika njia ya Msalaba na anajiweka katika safari pamoja nasi. Yote yanalenga sana kile ambacho Yesu anapitia wakati huo na ni wazi kwamba inapanua mada ya mateso ....”

Marejeo mapana

Kwa njia hiyo rejeo la matukio la sasa litakuwa nalo moja kwa moja, kama katika miaka mingine  ya nyuma ambapo wakimbizi, waathirika wa biashara ya binadamu au watu kutoka nchi katika vita walihusika, au, mwaka 2023, na ushuhuda na midahalo iliyochukuliwa kutoka katika nchi walizojeruhiwa  na ambapo Papa alitembelea wakati wa ziara zake za kitume. Hata kama katika Njia hii ya msalaba,  miunganisho yake ni mipana zaidi, ikiwa ni maombi ya marejeo yanapanuka... Sala haiendi kwa kundi la watu, bali kwa hali. Kwa hakika chaguo ni kuunganishwa na Mwaka wa Sala ambao Baba Mtakatifu Francisko amechagua kuutangaza kuwa maandalizi ya Mwaka wa Jubilei 2025, katika tukio ambalo, kama alivyokuwa amesema, kwanza kabisa lina tabia ya kiroho.

Uwepo wa Papa huko Palatine

Kuhusu uwepo wa Papa Francisko kwenye Njia ya Msalaba, kwa kuzingatia hali ya afya ya Papa na kushuka kwa joto jijini  Roma, hakuna uthibitisho au kukanusha kutoka katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican: kile ambacho tayari kilitangazwa hapo awali kinabaki, ambacho ni kwamba Papa atakuwa huko Ijumaa usiku  katika Palatine. “Kwa sasa hakuna mabadiliko ikilinganishwa na yale ambayo tayari yametazamiwa.” Maandishi ya tafakari yatasambazwa siku ya Ijumaa tarehe 29 Machi 2024 na siku hiyo hiyo kutakuwa na maelezo zaidi juu ya nani atabeba Msalaba, kando ya barabara za kale karibu na Colosseum. Hakika watu wanaobeba msalaba wameunganishwa na kutafakari katika kila kituo.”

Waandishi wa tafakari kwa miaka hii kumi iliyopita

Mnamo mwaka 2013, kwa  Njia ya Msalaba ya kwanza ya upapa wake, Papa Francisko alikabidhi tafakari kwa kundi la vijana wa Lebanon chini ya uongozi wa Kardinali Béchara Boutros Raï; (un gruppo di giovani libanesi sotto la guida del cardinale Béchara Boutros Raï;) mnamo mwaka 2014 ilikuwa ni zamu ya Asofu Mkuu  Giancarlo Maria Bregantini,)wa Campobasso-Boiano; (rej. ( monsignor Giancarlo Maria Bregantini); mnamo mwaka 2015, Askofu Mstaafu Renato Corti, wa Jimbo la  Novara;(rej. monsignor Renato Corti,);  Mnamo mwaka 2016, alikuwa ni Kadinali Gualtiero Bassetti, Askofu mkuu wa Perugia-Città della Pieve,(rej. cardinale Gualtiero Bassetti,) na mwaka uliofuata alichaguliwa kuwa rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI.) Mnamo mwaka 2017, Papa Francisko alichagua msomi wa kibiblia wa Ufaransa Anne-Marie Pelletier (rej. Anne-Marie Pelletier, ),mwanamke wa kwanza kushinda Tuzo ya Ratzinger, kama mwandishi wa tafakari kumi na nne.

Wakati mnamo 2018, tafakari zilikuwa ni matokeo ya mawazo, maswali na uchunguzi wa baadhi ya vijana kati ya miaka 16 na 27 (rej. ( giovani tra i 16 e i 27 anni, )iliyoratibiwa na profesa wa wakati huo, Andrea Monda, mkurugenzi wa sasa wa Gazeti la Osservatore Romano. Maandishi ya 2019, yaliyohaririwa na (Sr. Eugenia Bonetti, (Rej. suor Eugenia Bonetti,) mmisionari wa Consolata na rais wa Chama cha Slaves no more, yote yalilenga mada ya biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo. “Pamoja na Kristo na wanawake kwenye njia ya msalaba, ilikuwa ni mada ya  tafakari katika mwaka wa janga la Uviko-19, na 2020, uliwaona wahusika wakuu wa  Njia ya Msalaba katika mazingira ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika eneo la kipekee la Uwanja wa Mtakatifu Petro  na walikuwa wafungwa wa gereza la Due Palazzi huko Padova(rej. i detenuti della Casa di reclusione “Due Palazzi” di Padova.)

Tafakari za 'Kikundi' pia za mwaka uliofuata 2021, pamoja na kikundi cha skauti cha Agesci  kutoka Foligno I, huko Umbria, na parokia ya Jiji la Roma la Mashahidi wa  Uganda kama waandishi ambao pia walikuwa wameambatanisha maandishi yao na michoro kadhaa(rej. il gruppo scout Agesci “Foligno I", in Umbria, e la parrocchia romana Santi Martiri di Uganda). Mnamo mwaka 2022 Papa Francisko alitaka familia pamoja na furaha na shida zake zote, pamoja na sura na mielekeo yake tofauti, kuwa kitovu cha Njia ya Msalaba  siku ya Ijumaa Kuu(rej. famiglia,). Kwa hiyo kila kituo kilikabidhiwa aina tofauti ya familia: wenzi wa ndoa na wenzi wazee wasio na watoto; familia kubwa na mmoja ambayo amepoteza binti; familia yenye mtoto mlemavu, mtoto aliyewekwa wakfu, mzazi mgonjwa au aliyepoteza binti; familia katika utume, familia ya kuasili, familia inayoendesha nyumba ya familia, babu na bibi wawili, mjane, wazazi wahamiaji na watoto, familia mbili, moja ya Kiukreni na moja ya Kirusi.

Hatimaye mnamo 2023,  Papa Francisko akiwa na nia ya  kuhuisha tena mlolongo wa miaka kumi ya upapa  wake iliyoadhimishwa siku chache mapema, alikuwa amechagua kuingilia kati hatua ya Njia ya Msalaba siku ya Ijumaa Kuu na maandiko yaliyochukuliwa kutoka katika ushuhuda, mazungumzo, hotuba zilizokusanywa wakati wa ziara zake nyingi za kitume katika mabara matano au katika matukio mengine. Sauti za amani katika ulimwengu wa vita (rej. “Voci di pace in un mondo di guerra”,) ndiyo ilikuwa mada; yaani sauti za wanaume na wanawake kutoka kanda mbalimbali zilizokumbwa na ghasia, umaskini na chuki za kidugu zinazoumiza dunia.

Tafakari ya Njia ya Msalaba imetayarishwa na Papa
26 March 2024, 17:44