Tafuta

2024.02.10 Wawakilishi wa vyama vya mafundi na wajasiriamali kutoka pande zote za Italia 2024.02.10 Wawakilishi wa vyama vya mafundi na wajasiriamali kutoka pande zote za Italia   (Vatican Media)

Papa kwa Wajasiriamali na Shirikisho la Mafundi:muwe mafundi wa amani

Mikono,macho na miguu ni vitu vitatu ambavyo Papa amefafanua kwa wajasiriamali na wawakilishi wa Shirikisho la mafundi,Februari 10.Papa amesema Mafundi watusaidie kuwa na macho tofauti juu ya ukweli,kutambua thamani na uzuri wa nyenzo ambazo Mungu ameweka mikononi mwetu.Mikono yao,macho yao,miguu yao iwe ishara ya ubinadamu wa ubunifu na ukarimu.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

 Jumamosi, tarehe 10 Februari 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na idadi kubwa ya wajasiriamali na wawakilishi  wa Shirikisho la Mafundi (Confartigianato) waliofika kutoka kila sehemu ya Italia. Amemshukuru Rais wao na wote wanaofanya sehemu  ya  Chama hicho kiitwacho Confartigianato. Shirikisho lao lilizaliwa mnamo 1946 kwenye majivu ya Vita vya Pili vya Ulimwengu, Chama chao kilichangia kuzaliwa upya na maendeleo ya uchumi wa kitaifa. Katika miongo ya hivi karibuni, ufundi umepata mabadiliko makubwa, kutoka warsha ndogo hadi makampuni ambayo yanazalisha bidhaa na huduma, hata kwa kiwango kikubwa.

Papa amekutana na wawakilishi wa  Vyama vya Mafundi
Papa amekutana na wawakilishi wa Vyama vya Mafundi

Matumizi ya teknolojia yameongeza uwezekano wa sekta, lakini ni muhimu kwamba yasiishie kuchukua nafasi ya mawazo ya mwanadamu, aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Mashine huiga, hata kwa kasi ya kipekee, huku watu wakivumbua!  Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa shughuli zao huongeza ustadi na ubunifu wa mwanadamu.  Katika hayo amependa hasa kusisitiza “ni kiasi gani kazi yao imeunganishwa na viungo vitatu vya mwili: mikono, macho na miguu.” Awali ya yote ameanza na Mikono. Kazi ya mikono humfanya fundi kushiriki katika kazi ya uumbaji ya Mungu. Kutengeneza si sawa na kuzalisha. Kunaleta aina ya  uwezo wa ubunifu unaojua jinsi ya kuleta pamoja ujuzi wa mikono, shauku ya moyo na mawazo ya akili.

Mikono yao inajua kuumba vitu vingi vinavyowafanya wawe washirika wa Mungu. Bwana asema: “Kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo ninyi mlivyo mkononi mwangu” (Yer 18:6) Bariki na kumshukuru Bwana kwa zawadi ya mikono yenu na kwa kazi inawawezesha kujieleza. Baba Mtakatifu amesema kuwa “Tunajua kwamba si kila mtu ana bahati hii: kuna wale ambao hawana kazi, na wanaotafuta kazi. Ni hali zote za kibinadamu zinazohitaji kuponywa. Wakati mwingine pia hutokea kwamba makampuni yenu yanatafuta wafanyakazi wenye ujuzi na hawawezi kuwapata: msivunjika moyo katika kutoa kazi na msiogope kujumuisha makundi tete zaidi, yaani vijana, wanawake na wahamiaji.” Papa Francisko amewashukuru “kwa mchango wao wa kubomoa kuta za kutengwa kwa wale wenye ulemavu mkubwa au walemavu labda kutokana na ajali kazini, kwa wale wanaowekwa pembeni na kunyonywa. Kila mtu lazima atambulike katika hadhi yake kama mfanyakazi kike na kiume. Tusithubutu kukata mbawa za ndoto za wale wanaonuia kuboresha ulimwengu kupitia kazi na kutumia mikono yao kujieleza.”

Wawakilishi wa vyama vya mafundi
Wawakilishi wa vyama vya mafundi

Baada ya kuelezea kuhusu Mikono, Baba Mtakatifu amefafanua kipengele cha Macho. Kwa mujibu wa Papa amesema “Fundi ana sura halisi ya ukweli. Ana uwezo wa kutambua kazi bora katika jambo lisilo na maana hata kabla ya kuunda. Kwa kila mtu  anaina ni kipande cha marumaru, kwa fundi ni kipande cha thamani; kwa kila mtu anaona ni kipande cha mbao, kwa fundi ni violin, kiti, sura! Fundi ndiye wa kwanza kuelewa hatima ya uzuri ambayo nyenzo inaweza kuwa nayo. Na hii inamleta karibu zaidi na Muumba. Katika Injili ya Marko, Yesu anafafanuliwa kama "seremala" (6.3): mwana wa Mungu alikuwa fundi, alijifunza ufundi kutoka kwa Mtakatifu Joseph katika nyumba ya  Nazareti. Aliishi kwa miaka kadhaa kati ya ndege, patasi na zana za useremala. Alijifunza thamani ya vitu na kazi. Ulaji umeeneza mawazo mabaya: mawazo “yanayoweza kutupwa”. Lakini uumbaji sio jumla ya vitu, ni zawadi, “fumbo la furaha ambalo tunalitafakari kwa furaha na sifa" (Waraka wa Laudato si', 12).” Kwa hiyo Papa Francisko amesema wao watusaidie kuwa na macho tofauti juu ya ukweli, kutambua thamani na uzuri wa nyenzo ambazo Mungu ameweka mikononi mwetu.

Umati mkubwa wa wawakilishi wa vyama vya mafundi
Umati mkubwa wa wawakilishi wa vyama vya mafundi

Baba Mtakatifu akiendelea amesema baada ya kueleza Mikono na macho amejikita kueleza miguu. Bidhaa zinazotoka kwenye shughuli zao husafiri ulimwenguni  kote na kuipamba, zikijibu mahitaji ya watu. Ufundi ni njia ya kufanya kazi, kukuza mawazo, kuboresha mazingira, hali ya maisha na uhusiano. Hii ndiyo sababu Papa anapenda pia kukufikiria kama mafundi wa udugu. Mfano wa Msamaria Mwema ( rej Luka 10:29-37) unatukumbusha ufundi huu wa mahusiano, wa kushiriki pamoja. Msamaria akawa karibu, akainama na kumwinua yule mtu aliyejeruhiwa, akamweka juu ya miguu yake na kumpaka mafuta ya heshima kupitia ishara za kumtunza. Kwa hivyo "mfano unatuonesha ni mipango gani jamii inaweza kufanywa upya kuanzia wanaume na wanawake ambao hufanya udhaifu wa wengine kuwa wao wenyewe, ambao hawaruhusu jamii ya kutengwa ili kujengwa, lakini kuwa majirani na kuinua na kumrekebisha mtu aliyeanguka ili mema yawe ya kawaida" (rej Fratelli tutti, 67).

Papa wakati anaingia kwenye ukumbi wa Paulo VI
Papa wakati anaingia kwenye ukumbi wa Paulo VI

Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa miguu yetu inaturuhusu kukutana na watu wengi ambao wameanguka njiani: kupitia kazi tunaweza kuwaruhusu kutembea nasi. Tunaweza kuwa wasindikizaji wa  wasafiri, katikati ya utamaduni wa kutojali. Kila wakati tunapochukua hatua ya kumkaribia ndugu yetu, tunakuwa mafundi wa ubinadamu mpya. Papa amewahimiza wawe mafundi wa amani katika wakati ambapo vita vinaongeza waathirika na masikini hawasikilizwi. Mikono yao, macho yao, miguu yao iwe ishara ya ubinadamu wa ubunifu na ukarimu. Na moyo wao uwe na shauku ya uzuri kila wakati. Amewashukuru kwa mema wanayofanya. Na amewakawakabidhi kwa ulinzi wa Mtakatifu Joseph, ambaye anaweza kuwalinda wao, familia zao na kazi zao. Amewabariki kutoka ndani ya moyo wake. Na ameowamba wamuombee.

Papa Francisko na wajasiriamali na shirikisho la vyama vya mafundi
10 February 2024, 11:09