Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na waandaaji wa Tamasha la Muziki kwa Ajili ya Maskini Pamoja na Maskini, Ijumaa tarehe 15 Desemba 2023. Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na waandaaji wa Tamasha la Muziki kwa Ajili ya Maskini Pamoja na Maskini, Ijumaa tarehe 15 Desemba 2023.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Tamasha la Muziki kwa Ajili Pamoja na Maskini 2023

Hii ni sherehe inayopania kujenga na kudumisha umoja na udugu wa kibinadamu kwani kimsingi muziki una nguvu ya kuwaunganisha watu na kwamba, hili ni tukio kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni katika muktadha wa tamasha hili, Awamu ya Nne kwa mwaka 2023, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na waandaaji wa Tamasha la Muziki kwa Ajili ya Maskini Pamoja na Maskini, Ijumaa tarehe 15 Desemba 2023. Ujenzi wa udugu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Amana na utajiri wa Neno la Mungu unafumbatwa katika huruma na upendo wa Mungu kwa binadamu kama inavyoshuhudiwa kwa wale wakoma kumi waliotakasika; Kristo Yesu, Siku ile ya Alhamisi kuu, walipokuwa wakila, aliwaosha Mitume wake miguu yao na kuwapatia Amri ya upendo inayomwilishwa katika huduma hasa kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Huu ni mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuwa ni mashuhuda na vyombo vya huruma na upendo wa Mungu kwa binadamu. Hayo yamesemwa na Monsinyo Marco Frisina, Mkurugenzi wa Kwaya ya Jimbo kuu la Roma inayoongozwa na Speranza Scappuci, tarehe 15 Desemba 2023 majira ya jioni wanawatumbuiza maskini wa Roma, katika Awamu ya Nne inayoongozwa na kauli mbiu “Tamasha la Muziki kwa Ajili pamoja na Maskini.

Tamasha la Muziki Kwa Ajili Pamoja na Maskini 2023
Tamasha la Muziki Kwa Ajili Pamoja na Maskini 2023

Maskini elfu tatu kutoka Roma wanashiriki katika tamasha hili kwa mwaliko wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo. Tamasha linawashirikisha pia makundi mbalimbali ya watu wa kujitolea kama sehemu ya Sherehe ya Noeli kwa Mwaka 2023. Hii ni sherehe inayopania kujenga na kudumisha umoja na udugu wa kibinadamu kwani kimsingi muziki una nguvu ya kuwaunganisha watu na kwamba, hili ni tukio kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni katika muktadha wa tamasha hili, Awamu ya Nne kwa mwaka 2023, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na waandaaji wa Tamasha la Muziki kwa Ajili ya Maskini Pamoja na Maskini, Ijumaa tarehe 15 Desemba 2023.

Ujumbe Mahususi: Ujenzi wa udugu wa kibinadamu
Ujumbe Mahususi: Ujenzi wa udugu wa kibinadamu

Baba Mtakatifu anasema tukio hili ni kielelezo cha udugu wa kibinadamu, ujumbe mahususi wa Noeli ya Bwana. Tamasha la Muziki kwa ajili pamoja na maskini ni kielelezo cha upendo na mshikamano kwa kupokea na kushirikishana; mambo yanayogeuka na kujenga urafiki. Pamoja na muziki, Baba Mtakatifu amekazia pia umuhimu wa sala pamoja na kuwakabidhi waandaaji hawa wote chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa. Mwishoni amewatakia maadhimisho mema ya Sherehe za Noeli kwa Mwaka 2023.

Tamasha la Muziki
15 December 2023, 14:11