Tafuta

2023.12.05 Roselyne Hamel,katika uwakilishi wa Tuzo ya Padre Jacques Hamel 2023.12.05 Roselyne Hamel,katika uwakilishi wa Tuzo ya Padre Jacques Hamel 

Roselyne Hamel amempatia Papa mchoro na njiwa na mzeituni

Papa Francisko akikutana na Roselyne Hamel,dada yake Padre Jacques,aliyeuawa kikatili amepatia mchoro wa njiwa na mzetuni kama ishara amani na shairi ambalo alikuwa akiimba na kaka yake aliyeuwawa mnao 2016 akiwa na miaka 85 nchini Ufaransa katika Parokia ya Mtakatifu Etienne-du-Rouvray Jimbo katoliki la Rouen, na vijana wawili magaidi wenye asili ya Moroko.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Roselyne Hamel, dada yake Padre Jacques, ambaye mnamo 2016  akiwa na umri wa miaka 85 nchini Ufaransa katika parokia ya Mtakatifu Etienne-du-Rouvray, jimboni  katoliki la  Rouen, aliuawa na vijana wawili magaidi wenye asili ya Morocco ambapo  Jumatano tarehe 6 Desemba 2023 amekutana na Papa Francisko. Hata hivyo mkutano huo  sio mkutano wa mara ya kwanza na Papa kwani mnamo Septemba 2018, Papa alitaka kuadhimisha Misa katika kikanisa cha Mtakatifu Marta kwa ajili ya kumbukumbu ya kuhani  huyo – ambaye hata hivyo  mchakato wa kumtangaza mwenyeheri unaendelea, pamoja na familia yake na kikundi cha mahujaji 80 kutoka Jimbo katoliki la Rouen. Mkutano wa tarehe 6 Desemba  2023 ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Paulo VI, mbele ya hadhara kuu ulikuwa ni mkutano wa tatu kati ya Papa na Roselyne ambaye pia alitaka kuwasilisha picha ya kaka yake, yenye mandhari nyepesi mikononi mwake Papa.

Roselyne  katika Uwakilishi wa Tuzo kwa ajili ya Kaka yake
Roselyne katika Uwakilishi wa Tuzo kwa ajili ya Kaka yake

Uso wa mtu huyu, anayezingatiwa na wote kuwa mtakatifu katika maisha, anazo sifa fulani zinazofanana na zile za Mtakatifu Yohane Maria Vianney, aliyejukana kama Muuguzi wa Ars. Roselyne pia alihifadhi mahubiri kutoka kwa Padre Jacques ambayo aliyapata kutoka kwenye droo ya chumbani mwake na ambayo pia alimpatia  Papa na kumhakikishia kwamba aendelee kuomba kupitia yeye kwa ajili ya afya yake. Roselyne kwa sasa yuko Roma kuwasilisha toleo la sita la Tuzo la Uandishi wa Habari wa Padre  Jaques Hamel linalojikita katika mazungumzo ya kidini, lililopangwa kufanyika Januari huko Lourdes, na mwaka huu 2023  limefayika kwa  ajili ya maombi kwa  wanahabari kutoka ulimwenguni. Utambuzi huu ni njia ya kuendeleza kumbukumbu ya ndugu yake na pia kukuza mazungumzo na upatanisho.

Maridhiano na mama wa mmoja wa wauaji

Roselyne akifanya maridano na mmoja wa wauaji ni kwamba alichokifanya yeye mwenyewe kwa mara ya kwanza alipokutana na mama ya Adel Kermiche, mmoja wa wauaji wa kaka yake Padre akiwa na umri wa zaidi ya miaka kumi na nane, alianza njia ya uponyaji kwa pande zote. Ushuhuda huo, wa kina wa Roselyne Hamel ulishirikishwa katika maikrofoni ya Jean-Charles Putzolu, Mwandishi wa Habari wa Vatican. "Kukutana na Bi Kermiche ilikuwa njia niliyokuwa nikitafuta ili kuyapa maana maisha yangu, baada ya kuteswa na vurugu kama hizo. Sio tu kwamba Jacques amekufa, lakini alikufa na uovu huu wote wa kibinadamu. Kwa hiyo nilipokwenda kwa Bi Kermiche, jambo la kwanza alilosema, bila shaka, lilikuwa kwamba ni mwanawe aliyetenda hivyo. Aliomba msamaha. Alitaka kukutana nasi ili kuomba msamaha na kujaribu kuelewa. Mara moja tulishiriki mateso haya ambayo yalikuwa na maana tofauti. Lakini nilijiuliza 'nani anaweza kuteseka zaidi yangu?'” Alisema Bi Roselyne. “Ni kweli mama huyu aliyewalea watoto wake kama mimi na anabeba mateso makubwa sana. Alituelezea: mjue, mwanangu ni, nyama ya nyama yangu; ilibidi niwaite polisi wamfukuze na kumweka gerezani maana sikuweza kumudu tena. Na nilipogundua jinsi alivyokuwa akiishi gerezani, na karibu na mtu mzima mwenye msimamo mkali, tulimtoa nje, tukawalipa mawakili. Kwa ajili ya nini? Ili amuue mtu wa dini.”. Roselyne aliendelea, Mama huyu, mara kwa mara hubeba vazi hili la hatia, pamoja na uchungu wa kumpoteza mwanawe. Naye alitwambia: 'Tazameni niny wakristo, mna kitu maana mmekuja kunitembelea. Lakini jumuiya yangu imeniacha.”

Mkutano na dada wanne wa  mmoja wa washirika wa mauaji

Roselyne Hamel pia alieleza kuwa wakati wa kesi hiyo alifanikiwa kukaribua dada wanne wa mfungwa mwingine, aliyetuhumiwa kuwa mshiriki wa mauaji hayo. “Wakati wa mapumziko ya kesi, nilikwenda kukutana nao kwenye viti walipokuwa wameketi umma, na waliponiona nikija, walikuwa na sura ya hofu na mara moja nikasema: ‘Msiogope! Msiniogope.Nimekuja kuwaeleza huruma yangu kwa uchungu anayoipata mdogo webu. Walinishika mkono. Walinishukuru. Tulihisi amani." Siku ya mwisho ya kesi wale dada wanne walimngoja Roselyne kwenye lango la mahakama ili kumweleza zaidi kuhusu kaka yao. “Wao na mama yao hawakuweza kumtunza tangu alipokuwa mdogo sana. Tulizungumza kwa muda mrefu na, kabla ya kuondoka, niliwakumbatia na kuwaambia kwamba kaka yao mdogo sasa atakuwa amebeba mzigo mzito. ‘Muwepo kadri muwezavyo, nendeni mkamwone kwa sababu atawahitaji sana’.

Papa alikutana na Roselyne Hamel
07 December 2023, 13:34