Tafuta

Papa:Kwa kufuata mfano wa Nabii tunaweza kuwa nuru ya Yesu kwa wengine

Katika Noeli hii tushuhudie nuru ya kweli ambayo ni Kristo.Ni ushuhuda wa ujasiri wa Yohane Mbatizaji aliomshuhudia Yesu.Papa ametoa tafakari kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana kwamba katika kila enzi Bwana hutuma watu wenye nuru ambao kwa kufuata mfano wa nabii,wanatuonesha jinsi sisi pia tunaweza kuwa taa inayoangaza ili kuwasaidia wengine kutafuta njia ya kukutana na Yesu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko akiongoza tafakari yake Dominika ya Tatu ya Majilio tarehe 17 Desemba 2023 kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, kwa waamini na mahujaji wengi waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican amesema kuwa: “Leo katika Dominika ya Tatu ya Majilio, Injili inazungumza Utume wa Yohane Mbatizaji (Yh 1,6-8.19-28 ) akielekeza jinsi Nabii aliyetumwa na Mungu ili kushuhudia nuru. Kwa hiyo Papa amependa kutafakari juu ya kushuhudia mwanga. Papa ameanza na neno kushuhudia. Mbatizaji kwa hakika ni mtu wa kipekee. Watu wanamkimbilia kumsikiliza kwa kushangaa na mtindo wake wa  kuwa, madhubuti na wa dhati (Yh 1,6-7).

Wakati wa Sala ya Malika , zimaebarikia sana zitakazowekwa kwenye Pango
Wakati wa Sala ya Malika , zimaebarikia sana zitakazowekwa kwenye Pango

Ushuhuda wake unapitia ukweli wa lugha, uaminifu wa tabia, ukali wa maisha. Papa amesisitiza kwamba: “Mambo matatu: ukweli wa lugha, uaminifu wa tabia, ukali wa maisha.” Hayo yanamfanya awe tofauti na watu wengine mashuhuri na wenye nguvu wa wakati ule ambao kinyume chae walikuwa wanawekeza sana ujuujuu. Watu kama Yeye, wa moja kwa moja, walio huru na wajasri, ni watu angavu, na washangaza: wanatuchangamotisha ili kuinuka juu ya hali ya wastani na kuwa vielelezo vya maisha bora kwa wengine. Bwana anatuma kila nyakati, wanaume na wanawake wa namna hii. Je tunajua namna ya kuwajua? Tunatafuta kujifunza kutoka ushuhuda wao, hata kwa kujihoji? Au tunaacha kushangwa na watu kama hao wa  mtindo?" Papa ameongeza "tunakwenda kwenye tabia hizo za kijujuu."

Waamini wakati wa sala ya Malaika 17 Desemba 2023
Waamini wakati wa sala ya Malaika 17 Desemba 2023

Yohane ni angavu kwa sababu ya kushuhudia nuru. Lakini mwanga wake ni upi? Anatujibu yeye mwenyewe wakati anaposema wazi kwa umati uliokimbia  kumsikiliza, kwamba siyo yeye Nuru, na wala siyo yeye Masiha (Yh 1,19-20). Mwanga ni  Yesu, Mwanakondoo wa Mungu, Mungu anayeokoa. Ni Yeye tu anayekomboa, anayeleta uhuru, anaponya na kuangaza. Kwa sababu hiyo Yohane ni “sauti” inayosindikiza ndugu kwenye Neno; anatumikia, bila kutafuta heshima na umashuhuri: yeye ni taa, na mwanga ni Kristo aliye hai (Rej Yh 1, 26-27; Yn 5.35). Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa, kwa "mfano wa Yohane Mbatizaji anatufundisha angalau mambo mawili. Kwanza kwamba peke yetu hatuwezi kujiokoa, ni kwa Mungu peke yake tunapata mwanga wa maisha. Pili kwamba kila mmoja wetu katika huduma, mshikamano, unyenyekevu na ushuhuda wa maisha, kwa maana ya neema ya Mungu inawezekana kuwa taa ambayo inaangaza na kusaidia wengine kupata njia ya kukutana na Yesu.

Tafakari ya Papa 17 Desemba 2023
Tafakari ya Papa 17 Desemba 2023

Kwa hiyo tujiulize: Je ninawezaje, katika mazingira ninamoishi, si siku ya mbali lakini tayari sasa, Noeli hii, kuwa shuhuda wa mwanga, shuhuda wa Kristo? Maria, kioo cha utakatifu, a tusaidie kuwa wanaume na wanawake wanaoakisi Yesu, nuru inayokuja ulimwenguni." Baba Mtakatifu  ameomba tujiulize: je ninaweje katika mazingira ninayoishi sio siku moja ya mbali, bali kuanzia sasa, katika Noeli hii kuwa shuhuda wa nuru, kushuhudia Kristo? Ninawezaje katika mikutano mingi, katika mazungumzo, katika kusheherekea kwenye siku kuu zijazo kushuhudia mwanga wa kweli,  yaani Bwana Yesu ambaye anaangaza maisha yake ili hata wengine waweza kumjua na kufurahi pamoja naye? Maria, kioo cha Utakatifu atusaidie  kuwa wanaume na wanawake ambao wanaonesha Yesu mwanga ambao unakuja ulimwenguni.

Tafakari ya Papa 17 Desemba 2023
17 December 2023, 12:51