Tafuta

2023.12.07 Papa amekutana na Wajumbe wa Chama cha Kitaifa cha Mtakatifu Paulo (Anspi). 2023.12.07 Papa amekutana na Wajumbe wa Chama cha Kitaifa cha Mtakatifu Paulo (Anspi).  (Vatican Media)

Papa kwa ANSPI:Injili ni furaha,tumaini,nuru na tangazo la wokovu

Papa amewashukuru Chama cha Kiataifa cha Mtakatifu Paulo,Italia(ANSPI)kwa sababu wanazingatia ufunguzi wa nafasi wazi na furaha.Furaha ni dawa kubwa zaidi.Mtu anapopoteza furaha na kupoteza uwezo wa kufurahi kuna kitu kibaya ndani mwake.Ni katika fursa ya maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko alhamisi tarehe 7 Desemba 2023 amekutana na Wajumbe wa Chama cha Kitaifa cha Mtakatifu Paolo Italia (ANSPI) ambao amewakaribisha wakiwa katika fursa ya maadhimisho ya miaka 60 ya chama hicho . Ni fursa nzuri inayosadia kujikita katika mizizi ya kiini cha maisha ili kundelea na jitihada, kwa ari , ili kujiunda kibinadamu, na kikristo vijana kwa njia ya shughuli za vituo na mikutaniko ya vijana katika maparokia. Mtindo wao ulizaliwa katika Muktadha wa Mtaguso kwa utashi wa Monsinyo Battista Belloli, kwa kusaidia na Askofu Mkuu Montini, ambaye alikuwa anaunganishwa na chaka cha utume wa Paulo kwa hakika mnamo 1963 alipochaguliwa kuwa Papa. Miaka hiyo ya upyaisho wa katekesi, Monsinyo Belloli alikuwa na furaha ya kuanzisha chama chenye nia ya kichungaji katika nuru ya mafundisho ya mtaguso, kwa kuthamanisha uhusiano wa Walei na kutoa mtindo na roho ya elimu fungamani.

Papa amekutana na Wajumbe wa Chama cha Kitaifa cha Mtakatifu Paulo Italia
Papa amekutana na Wajumbe wa Chama cha Kitaifa cha Mtakatifu Paulo Italia


Mapendekezo yao ya ubunifu, utamaduni na sanaa daima vina mtazamo wa elimu fungamani ya binadamu kwa watoto wote kike na kiume. Baba Mtakatifu amesema. "Lazima tujali mtu mzima, vipimo vyake vyote: kihisia, kisaikolojia, kiroho, kiakili, kimwili. Mtakatifu Yohane Bosco alisema kwamba lazima tufunze "Wakristo wema na raia waaminifu",tukijua wazi kwamba haiwezekani kuelimisha katika vyumba visivyo na maji na kwamba mustakabali mzuri au mbaya wa jamii unategemea kwa usahihi elimu chanya au hasi ya vijana.

Wajumbe wa Anspi
Wajumbe wa Anspi


Mtindo wa Kikanisa na kiraia ni sura mbili zilizo kwenye medali moja sawa, na haziwezi kuwa tofauti kwa sababu zote mbili zinachangia wema wa kuaminika na kwa pamoja. Papa Francisko amethibitisha jinsi ambavyo anapenda methali ya Kiafrika ambayo inafungamanisha ukweli mkubwa kuwa: “ili kukuza mttoto inahitaji kijiji kizima”. Kwa hiyo amesema “Leo hii kuliko hapo awali kuna haja ya kuunda mshikamano ili kuunda mtu mkomavu, mwenye uwezo wa kushinda mpasuko na kinzani ili kujenga kiini cha mahusiano kwa ajili ya ubinadamu wa kidugu zaidi (rej. Uzinduzi wa Mkataba wa Elimu, 12 Septemba 2019).

Papa na wajumbe wa Chama cha Anspi
Papa na wajumbe wa Chama cha Anspi


Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru Chama cha Kiataifa cha Mtakatifu Paulo Italia ANSPI) kwa sababu wanazingatia ufunguzi wa nafasi wazi na furaha. Papa amesema kuwa Furaha ni dawa kubwa zaidi. Mtu anapopoteza furaha anapoteza uwezo wa kufurahi kuna kitu kibaya ndani mwake. Katika furaha kwa mfano Mtakatifu Philipo Neri alipenda kurudia kusema kuwa "changamka, uwe na moyo mkunjufu". Wakristo hawawezi kuwa na huzuni, Injili ni furaha, tumaini, nuru, tangazo la wokovu. Na hii inahusishwa na uzoefu wa bure, yaani wa bure, ambao unahusishwa na zawadi ya kujitolea. Msimamizi wao Mtakatifu Paulo aliandika kuwa “mueni na furaha daima katika Bwana, ninarudia furahini (rej. fil 4,4).” Kwa hiyo amemakabidhi Yeye na Bikira Maria chama chao , vijana wao, wanaowasimamia na familia. Amewashukuru kufika kwao, kazi zao katika huduma ya Kanisa na Jumuiya. Amewabariki kwa Moyo na kuwaomba wasishau kusali kwa ajili yake.

Hotuba ya Papa kwa Wajumbe wa Chama cha Anspi
07 December 2023, 13:43