Tafuta

2023.12.06 Papa Francisko wakati wa Katekesi tarehe 6 Novemba 2023 2023.12.06 Papa Francisko wakati wa Katekesi tarehe 6 Novemba 2023  (Vatican Media)

Papa Francisko:Tangazo la Injili lifanyike katika Roho Mtakatifu

Katika tafakari ya Papa kwa waamini na mahujaji waliofika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican na ambaye amekabidhi tafakari hiyo isome na Monsinyo Ciampanelli,Afisa katika Ofisi ya Katibu wa Vatican ni mwendelezo wa ari ya kitume."ni Roho Mtakatifu anayehuisha ubunifu na urahisi wa kutangaza Injili.Utume sio maandiko ya kitaalimungu ni kazi ya Roho Mtakatifu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Ketesi ya Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 6 Desemba 2023 akiwa katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican na ambaye ametangulia kwa salam una kuwaalika waamini na mahujaji kufika kwao alisema, “Kaka na dada, habari za asubuhi, ninawakaribisha nyote!. Hata leo hii, nimeomba msaada wa Monsinyo Ciampanelli ili kusoma, kwa sababu bado nina ugumu.Nimepata hauheni, lakini ninapata ugumu ikiwa ninazungumza sana. Kwa sababu hiyo atakuwa yeye kusema kitu... Kwa njia hiyo, mara baada ya kusema hayo, aliendelea Monsinyo Filippo Ciampanelli, Afisa katika  Ofisi ya Katibu wa Vatican kusoka mkatekesi hiyo. Tafakari ya Papa inabainisha kwamba: “katika katekesi zilizopita tumeona kwamba utangazaji wa Injili ni furaha, ni kwa ajili ya kila mtu na ni lazima kujikita nayo leo. Hebu sasa tugundue tabia moja muhimu ya mwisho ya tangazo ambalo lazima lifanyike katika Roho Mtakatifu. Kiukweli "kuwasiliana na Mungu", uaminifu wa furaha wa ushuhuda, kuenea kwa tangazo na kutoa  ujumbe haitoshi. Bila Roho Mtakatifu, bidii yote ni bure na ya uwongo ya kitume na kama ingekuwa  yetu tu na isingezaa matunda.”

Picha za Watoto na Papa wakati wa katekesi ya 6 Desemba 2023
Picha za Watoto na Papa wakati wa katekesi ya 6 Desemba 2023

Baba Mtakatifu katika tafakari hiyo anakazia kusema kuwa “Katika Evangelii gaudium alikumbuka kwamba “Yesu ndiye mwinjilishaji wa kwanza na mkuu;  na kwamba “katika namna yoyote ya uinjilishaji ukuu siku zote ni wa Mungu”, ambaye“alitaka kutuita ili tushirikiane naye na kutuchochea kwa nguvu za Roho wake” (n. 12).  Na huo ndiyo ukuu wa Roho Mtakatifu! Kwa njia hiyo Bwana analinganisha nguvu ya Ufalme wa Mungu na “mtu atupaye mbegu katika udongo; akilala au anapoamka, usiku au mchana, mbegu huota na kukua; na kwa jinsi ambavyo yeye mwenyewe hajui”(Mk 4:26-27). Roho ndiye mhusika mkuu, yeye huwatangulia wamisionari na hufanya kuzaa  matunda.

Salamu za waamini kwa Papa katika Ukumbi wa Paulo VI
Salamu za waamini kwa Papa katika Ukumbi wa Paulo VI

Ufahamu huu unatufariji sana!Na unatusaidia kufafanua mwingine, na wenye uamuzi sawa na huo yaani katika ari yake ya kitume, Kanisa halijitangazi lenyewe, bali kwa neema, zawadi na Roho Mtakatifu ndiye Zawadi ya  Mungu, kama Yesu alivyo mwaambia mwanamke Msamaria(rej.Yh 4,10). Hata hivyo, ukuu wa Roho haupaswi kutuongoza kwenye uvivu. Kuaminiana hakuhalalishi kutojibidisha. Uhai wa mbegu inayoota yenyewe haidhinishi wakulima kupuuza shamba.Yesu, katika kutoa mapendekezo ya mwisho kabla ya kupaa mbinguni,alisema:“Mtapokea nguvu kutoka kwa Roho Mtakatifu atakayewashukia juu yenu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu [...] hata miisho ya dunia” (Mdo 1,8). Bwana hajatuachia kazi iliyoandikwa ya  kitaalimungu au mwongozo wa kichungaji ili tuutumie,bali ni Roho Mtakatifu ambaye anaongoza utume. Na ustadi wa ujasiri ambao Roho hutia hutuongoza kuiga mtindo wake,ambao daima una sifa mbili: ubunifu na urahisi.

Waaamini wakaitamani kumsalimia Papa
Waaamini wakaitamani kumsalimia Papa

Baba Mtakatifu anasisitiza juu ya Ubunifu, katika kumtangaza Yesu kwa furaha, kwa kila mtu na leo hii. Katika zama zetu, ambazo hazitusaidii kuwa na mtazamo wa kidini juu ya maisha na ambamo utangazaji umekuwa mgumu zaidi, wenye kuchosha na usio na matunda katika sehemu mbalimbali, kishawishi cha kuacha uchungaji kinaweza kutokea. Labda tunapata kimbilio katika maeneo ya usalama, kama vile kurudia rudia kwa kawaida kwtika mambo tunayofanya kila mara, au katika miito inayojaribu ya hali ya kiroho ya karibu, au hata kwa maana isiyoeleweka ya umuhimu wa liturujia. Ni majaribu ambayo yanajifanya kuwa mwaminifu kwa mapokeo, lakini mara nyingi, badala ya majibu ya Roho, ni miitikio ya kutoridhika kwa kibinafsi. Badala yake, ubunifu wa kichungaji, kuwa jasiri katika Roho, kuwaka moto wa kimisionari, ni uthibitisho wa kutoka kwake. Kwa hiyo Baba Mtakatifu amebainisha kuwa aliandika kwamba “Yesu Kristo pia anaweza kuvunja mamlaka ya kuchosha ambayo tunajifanya kumfunga na kutushangaza kwa mara kwa mara yake,ubunifu wa kimungu.

Hata Kundi la waamini kutoka Ukraine na Bendera zao
Hata Kundi la waamini kutoka Ukraine na Bendera zao

Kila wakati tunapojaribu kurudi kwenye chanzo na upyawa  asili ya Injili,njia mpya,mbinu za ubunifu, namna nyinginezo za kujieleza,zilizofasaha zaidi,maneno yaliyo jaa maana mpya kwa ulimwengu wa leo yanaibuka”(Evangelii gaudium,11). Ubunifu, kwa hiyo na baadaye shauku, hasa kwa sababu Roho hutupeleka kwenye chanzo, hadi kufikia "tangazo la kwanza." Kwa hakika ni "moto wa Roho ambao [...] hutufanya kumwamini Yesu Kristo, ambaye kwa kifo na ufufuko wake alifunua na kuwasiliana nasi ile huruma isiyo na kikomo ya Baba"(Eg 164). Hili ni tangazo la kwanza, ambalo "lazima likae katika kitovu cha shughuli ya uinjilishaji na kila jaribio la kufanywa upya kikanisa;" Kwa kurudia papa amebainisha: “Yesu Kristo anakupenda, alitoa maisha yake ili kukuokoa, na sasa yuko hai karibu nawe kila siku, ili kukuangazia, kukutia nguvu, kukuweka huru.”

Watoto wakisalimiana na Papa
Watoto wakisalimiana na Papa

Katika tafakari hiyo  Baba Mtakatifu anakazia kusema kuwa na tufungwe na Roho na kumwomba kila siku kwani yeye awe kanuni ya utu wetu na kazi yetu; awe mwanzoni mwa kila shughuli, mkutano, mkusanyiko na tangazo. Yeye hulihuisha na kulifufua Kanisa: pamoja naye hatuna haja ya kuogopa, kwa sababu Yeye, ambaye ni maelewano, daima anashikilia ubunifu na urahisi pamoja, huhamasisha ushirika na kutuma utume, hujifungua katika utofauti na huongoza nyuma katika umoja. Yeye ni nguvu zetu, pumzi ya tangazo letu, chanzo cha ari ya kitume. Uje, Roho Mtakatifu! Tafakari ya Papa Francisko imehitimishwa iliyosomwa kwa niaba yake na Monsinyo Filippo Ciampanelli, Afisa katika Ofisi ya Katibu wa Vatican.

Katekesi ya Papa 6 Desemba 2023
06 December 2023, 15:37