Papa amekabidhiwa Tamko juu ya Udugu wa Kibinadamu na wananobel ya amani
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Jumatano tarehe 6 Desemba 2023 Mwishoni mwa Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko alisalimiana na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2021 Mwandishi wa habari wa Ufilipino Maria Ressa kutoka (Ufilipino), mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2021, mwanafizikia wa Kiitaliano Giorgio Parisi(Italia), na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 201, mwanaharakati wa Yemen Tawakkul Karman, kutoka (Yemen), katika katekesi ya Papa kwenye Ukumbi wa Paul VI, wakiambatana na Kardinali Gambetti, Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na Rais wa Mfuko wa Fratelli tutti, walimkabidhi Papa hati iliyoandikwa na kutiwa saini na washindi wengine 30 wa Tuzo ya Nobel katika hafla ya mkutano wa kwanza wa #Notalone, wa Udugu mnamo tarehe 10 Juni 2023 ambapo dhamira ya kujenga jamii za amani na kuunganisha ardhi iliyojeruhiwa na chuki na vurugu ilisisitizwa.
Kwa njia hiyo pia Baba Mtakatifu alipokea hati hiyo ya "Tamko juu ya udugu wa binadamu", kwa niaba ya washindi zaidi ya 30 wa Tuzo ya Nobel na mashirika ya kimataifa ambao pamoja nao walitayarisha na kutia saini hati hiyo mnamo Juni 2023, wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Udugu wa Kibinadamu. Mwisho wa Mkutano huo ilipigwa picha ya pamoja na washindi watatu wa Tuzo ya Nobel pamoja na Baba Mtakatifu. Ishara hiyo inawakilisha hatua ya kwanza ambayo itaanza uwasilishaji wa hati katika maeneo mengine ya sayari.
Ni Washindi wa Tuzo ya Nobel walioshiriki katika Mkutano wa#notalone mnamo tarehe 10 Juni kwa “Tamko juu ya udugu wa kibinadamu” katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Hati hiyo, iliyoandaliwa na wao wakati wa kazi ya asubuhi katika Jumba la Kansela na ilitiwa saini Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican.
Aidha Washindi wa Tuzo ya Nobel Nadia Murad na Muhammad Yunus walisoma Tamko hilo duniani kote, likiwakilisha kila mtu ambapo wanaandika kuwa: “tunaitikia chuki kwa upendo, kwa kujitolea kuunda jamii za amani kuunganisha ardhi iliyotiwa damu ya vurugu na chuki, na ukosefu wa usawa wa kijamii na uharibifu wa moyo. Tunataka kupiga kelele kwa ulimwengu kwa jina la udugu kwa hakuna vita tena! Ni amani, haki na usawa ndio huongoza hatima ya wanadamu wote.”Unaweza kusoma tamko kuhusu Udugu wa kibinadamu na hata kutia saini na wewea katika tamko hili hapa chini:
Leggi la Dichiarazione sulla fraternità umana
Firma anche tu la Dichiarazione