Tafuta

2023.12.06 Papa na Baraza la Makardinali Washauri au  C9 2023.12.06 Papa na Baraza la Makardinali Washauri au C9 

C9 inashughulikia suala la nafasi ya wanawake katika Kanisa,shida ya ulimwengu

Mkutano wa juma moja mjini Vatican,wa Baraza la Makardinali la Papa Francisko lilikubaliana juu ya haja ya kusikiliza “kipengele cha kike”katika Kanisa,hasa katika ngazi mahalia ili michakato ya kutafakari na kufanya maamuzi iweze kufaidika na isiyoweza kubadilishwa ya mchango wa wanawake.”

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Kikao cha Baraza la Makardinali washauri wa Papa (C9) kilifanyika kwa siku mbili ya tarehe 4 na 5 Desemba  2023, katika Nyumba ya Mtakatifu  Marta, mjini Vatican. Waliokuwepo, pamoja na Baba Mtakatifu, walikuwa Makardinali wote ambao ni sehemu yake  ya Ushauri na Katibu wa Baraza hilo. Katikati ya tafakari ya tukio hilo kulikuwa na mada ya jukumu la mwanamke katika Kanisa.

Wataalamu wa kitaalimungu washiriki Baraza la Makardinali washauri wa Papa

Mazungumzo hayo yalichochewa nafasi ya  Sr. Linda Pocher,  Washirika la Binti wa Maria Msaada wa Wakristo, profesa wa Ukristo na  Elimu ya Maria  katika Kitivo cha Kipapa cha Sayansi ya Elimu Auxilium jijini Roma; na  Profesa Lucia Vantini, anayefundisha Taalimungu  ya kimsingi, falsafa ya dini na falsafa ya maarifa katika Taasisi ya Sayansi ya Kidini huko Verona, na anthropolojia ya kifalsafa na kitaalimungu  katika Mafunzo ya Mtakatifu Zeno huko Verona na falsafa ya mazungumzo katika Taasisi ya Mafunzo ya Kiekumeni ya Mtakatifu  Bernardino huko Venezia; na Luca Castiglioni, Padre wa Jimbo Kuu la Milano na Profesa wa Taalimungu ya msingi katika Seminari ya Milano.

Baraza la Makardinali 9 washauri wa Papa
Baraza la Makardinali 9 washauri wa Papa

Baraza lilikubaliana juu ya haja ya kusikiliza, pia na zaidi ya yote katika jumuiya binafsi za Kikristo, kipengele cha kike katika Kanisa, ili taratibu za kutafakari na kufanya maamuzi ziweze kufaidika kutokana na mchango usioweza kubadilishwa wa wanawake. Hali ya sasa ya kijamii, kisiasa na kikanisa katika maeneo mbalimbali ya asili ya wajumbe wa Baraza ilichunguzwa, hasa kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Ukraine na hali mbaya ya Nchi Takatifu, pamoja na kazi ya Mkutano wa Nchi Wanachama katika Mkataba Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi(COP28) unaendelea Dubai hadi tarehe 12 Desemba 2023.

Taarifa kuhusu kulinda na kuzuia unyanyasaji

Kardinali Seán Patrick O'Malley, alionesha dhana mbalimbali kuhusu mpangilio wa mabaraza ya Mabaraza ya Maaskofu kwa miaka mitano baada ya Mkutano kuhusu: "Kulinda na kuzuia unyanyasaji wa Watoto na Watu wanaoishi katika mazingira magumu mwezi Februari 2019, ambao ulikuwa na mada ya majadiliano na tathmini na Wajumbe wa Baraza.

Sinodi 2023

Hatimaye kikao hicho kilitoa fursa ya kujadili kikao cha kwanza cha Baraza Kuu la Kawaida la Sinodi ya Maaskofu na kuendeleza tafakari ya utekelezaji wa roho, kanuni na vigezo vya Uinjilishaji  wa Katiba ya Kitume ya Praedicate evangelium yaani Hubirini Injili katika makanisa ya majimbo. Kikao kijacho kitakuwa mnamo Februari 2024.


Ikumbukwe Braza la Makardinali washuri wa Papa linaunda na:Kardinali Pietro Parolin,katibu wa Vaticana;  Kardinali Fernando Vérgez Alzaga,Rais wa Tume ya Kipapa ya Mji wa Vatican na Mkuu tawala wa Vatican; Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa Kinshasa(DRC); Kardinali Oswald Gracias,Askofu Mkuu wa Bombay; Kardinali Seán Patrick O'Malley, Askofu Mkuu wa Boston; Kardinalo Juan José Omella Omella, Askofu Mkuu wa Barcelona; Kardinali Gérald Lacroix, Askofu Mkuu wa Quebec; Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa Luxembourg; Kardinali Sérgio da Rocha,Askofu mkuu wa San Salvador de Bahia. Katibu ni AskofuMarco Mellino,wa Jimbo la Cresima. Mkutano wa kwanza wa Basasisho la raza Jipya la Makardinali Washauri wa Papa 9 (C9) ulifanyika mnamo tarehe 24 Aprili 2023.

06 December 2023, 17:47