Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amewaandikia Barua Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Uchumi mjini Vatican kumbukizi ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko amewaandikia Barua Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Uchumi mjini Vatican kumbukizi ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi mjini Vatican.   (Vatican Media)

Barua ya Papa Kwa Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Uchumi ya Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amewaandikia Barua Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Uchumi mjini Vatican akirejea kuhusu; Historia ya mageuzi ya kiuchumi mjini Vatican, Sekretarieti ya Uchumi ni kwa ajili ya utume wa Kanisa, Wanapaswa kuwa ni Mawakili waaminifu na wenye busara; umuhimu wa mafunzo kazini; Utekelezaji wa Bajeti ya Vatican ni wajibu wa wote kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Sekretarieti ya Uchumi ni kwa ajili ya maisha na utume wa Kanisa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 24 Februari 2014 alichapisha Barua Binafsi ijulikanayo kama “Fidelis dispensator et prudens” yaani “Wakili Mwaminifu na Mwenye Busara” Lk 12:42, iliyoanzisha kitengo cha Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Vatican kinachoratibu mambo ya uchumi na utawala mjini Vatican kama sehemu ya mageuzi makubwa yaliyokua yameanzishwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI na hatimaye kufanyiwa marekebisho na Katiba mpya ya Kitume inayojulikana kama “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili” Juu ya Sekretarieti kuu “Curia Romana” na Huduma Yake Kwa Kanisa na Kwa Ulimwengu.” Baba Mtakatifu Jumatatu tarehe 11 Desemba 2023 amekutana na kuzungumza na wafanyakazi kutoka Ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Vatican na kukazia mambo makuu mtatatu: Uhuru wa ofisi, sheria na kanuni za Kimataifa pamoja na taaluma. Baba Mtakatifu Francisko anasema, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Vatican inajitegemea, kumbe inapaswa kuwajibika kwa kunogeshwa na karama ya upendo; kwa kusahihishana, kukosoana na kurekebishana kidugu, hata kama wanapaswa kutoa taarifa kwa matukio ya fedha na mambo ambayo yanakwenda kinyume cha sheria, taratibu na kanuni. Baba Mtakatifu Francisko amewaandikia Barua Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Uchumi mjini Vatican akirejea kuhusu; Historia ya mageuzi ya kiuchumi mjini Vatican, Sekretarieti ya Uchumi ni kwa ajili ya utume wa Kanisa, Wanapaswa kuwa ni Mawakili waaminifu na wenye busara; umuhimu wa mafunzo kazini; Utekelezaji wa Bajeti ya Vatican ni wajibu wa wote kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

Rasilimali, amana na utajiri wa Kanisa ni kwa ajili ya uinjilishaji
Rasilimali, amana na utajiri wa Kanisa ni kwa ajili ya uinjilishaji

Baba Mtakatifu Francisko anasema, imegota miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi mjini Vatican, ili kuhakikisha kwamba, amana na utajiri wa Vatican vinatumika kwa ajili ya utume wa Kanisa. Hii ni kazi inayotekelezwa kwa: ari, ujasiri na bila woga kama alivyofanya Hayati Kardinali George Pell, Mwenyekiti wa kwanza wa Sekretarieti ya Uchumi. Wafanyakazi hawa watambue kwamba, ni wahudumu katika utume wa Kanisa; dhamana wanayoitekeleza kwa kuwajibika pamoja na kutambua kwamba, Kanisa kwa asili ni maskini, kwani amana na utajiri wake ni kwa ajili ya kutangaza Habari Njema ya Wokovu. Barua Binafsi ijulikanayo kama “Fidelis dispensator et prudens” yaani “Wakili Mwaminifu na Mwenye Busara” Lk 12:42, iliyoanzisha kitengo cha Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Vatican inawaalika wafanyakazi katika Ofisi hii kutofanya kazi kwa mazoea. Wajenge utamaduni wa kusikiliza kwa makini, watumie akili, ujuzi, maarifa na taaluma yao kutekeleza dhamana na wajibu huu nyeti kwa maisha na utume wa Kanisa; kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya Kanisa. Wasimamie ukweli na uwazi kwa ajili ya maisha na utume wa Kanisa. Wawe na busara kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya Kanisa; busara kwa ajili ya waamini na wahitaji zaidi kwa kutambua kwamba, Sekretarieti ya uchumi ni mlinzi na mhudumu wa Kanisa; dhamana inayowataka kujisadaka bila ya kujibakiza, kwa kutumia vyema taaluma yao, ujuzi na maarifa; mambo yanayofumbatwa katika unyenyekevu, utamaduni wa kusikiliza; sheria, kanuni na taratibu; ukweli na uwazi na ujasiri wa kutoa taarifa kwa yale mambo yanayosigana na maisha na utume wa Kanisa.

Wafanyakazi wekezeni katika uaminifu, uadilifu, ukweli na haki
Wafanyakazi wekezeni katika uaminifu, uadilifu, ukweli na haki

Kwa hakika wanawajibika kufanya kazi kwa kuangalia pia na mambo ya mbeleni kwa kutambua kwamba, amana, rasilimali na fedha ya Kanisa ni kidogo sana kumbe, wanawajibika kusoma alama za nyakati, ili amana na utajiri huu visaidie hata kwa siku za usoni. Hapa kazi hii ifanyike katika misingi ya ukweli na uwazi pamoja na kujikita katika busara. Baba Mtakatifu Francisko anakaza kusema, Sekretarieti ya Uchumi inakabiliwa na changamoto zinazopaswa kufanyiwa kazi kwa kujikita katika: Utoaji wa mafunzo kazini; Mishahara ya haki na usawa kwa wote na hivyo kujenga mazingira ya upendo na ukarimu. Wazingatie kanuni maadili na utu wema, taaluma na bei nzuri zinazotolewa na mawakala wa huduma mjini Vatican. Baba Mtakatifu anawahamasisha wafanyakazi hawa kulinda na kutunza amana na utajiri wa Kanisa, kwa kuzingatia kanuni maadili, ili uwekezaji wa rasilimali ya Kanisa uweze kuzaa matunda yanayokusudiwa. Wahakikishe kwamba, wanatekeleza Bajeti ya Vatican kwa weledi kwani Kanisa ni maskini na hivyo utajiri wake unapaswa kutumiwa kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Injili; kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya Kanisa. Sekretarieti ya Uchumi ijenge utamaduni wa kusikiliza kwa makini, itekeleze dhamana na wajibu wake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu; kwa kuzingatia ukweli na uwazi, ili kwa pamoja waweze kutoa ushuhuda wa uchumi unaojikita katika huduma kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya Kanisa.

Barua kwa Wafanyakazi
13 December 2023, 15:19