Tafuta

2023.11.06 Kundi la Nyumba Ndogo ya Huruma ya huko  Gela Kusini mwa Italia. 2023.11.06 Kundi la Nyumba Ndogo ya Huruma ya huko Gela Kusini mwa Italia.  (Vatican Media)

Papa na kundi la Nyumba ya huruma ya Gela:onesheni uso wa Bwana

Kutotulia kutakatifu na unyenyekevu mwingi wa kuwa tayari na dhati katika kujibu mahitaji ya ndugu na wakati huo huo kupeleka kwa wote kukutana kibinafsi uso wa huruma wa Baba,ndiyo mambo aliyowashauru Papa,Udugu wa Kitume wa Huruma na Nyumba Ndogo ya Huruma huko Gela Kusini mwa Italia.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 6 Novemba 2023 amekutana na Kundi la Nyumba ndogo ya Huruma na Udugu wa Kitume wa Huruma kutoka Gela huko Caltanisetta, Kusini mwa Italia, katika fursa ya maadhimisho ya miaka 50  na  10 tangu kuanza kwao. Amemsalimu Askofu Rosario Gisana wa Uwanja wa Armerina na kumpongeza kuwa  amefanya vizuri, Askofu huyo. Aliteswa, alisingiziwa na alikuwa thabiti, daima, mtu mwadilifu. Kwa sababu hiyo, siku ile alipokwenda Palermo, Papa Francisko alitaka kusimama kwanza Uwanja wa Armerina, ili kumsalimia; kwani ni Askofu mzuri. Papa amewasalimu Mapadre na Mashemasi waliopo, Masista wa Maria Immaculate, wanachama wa Udugu na Ushirika wa "Raphael", watu wa kujitolea na watu wanaokaribishwa, vijana na waamini wote.

Baba Mtakatfu amesema kwamba wafika hapo  kama familia kubwa, ambamo kila mmoja ana vipawa na kazi tofauti na zinazosaidiana; na aina hii tajiri inazungumza yenyewe juu ya njia ambayo, katika miaka ya hivi karibuni, umeanzisha mpango ulioelezewa na thabiti wa mema. Kuanzia hali ngumu, wamejaribu kukumbatia watu wote na mtu mzima katika upendo, kushughulikia mahitaji mengi na kukuza mipango mbalimbali: kuanzia canteen ya kila siku ya maskini hadi warsha za ufundi, kutoka huduma za uokoaji wa kielimu hadi nafasi za mazungumzo kwa familia ngumu. Wanaweza kuona kwamba kuna harakati huko, na hiyo ni nzuri; wanaweza kuona kwamba wamejiruhusu kuchokozwa na kufadhaishwa na mahitaji ya kaka na dada ambao Mungu amewaweka kwenye njia yenu, hasa wale walio wadogo na wahitaji zaidi: wako wengi! Mbele yao ‘hawakupitia juu’, lakini walisimama kidete, wakiwa karibu nao na kuwatunza (Lk 10:25-37), kwa ubunifu, ujasiri na ukarimu, kama Msamaria mwema ambaye hakwenda zaidi ya na hiyo ni nzuri, Papa amewapongeza.Na kuwahimiza kuendeleze hayo yote.

Papa amekutana na Jumuiya ndogo ya Gela
Papa amekutana na Jumuiya ndogo ya Gela

Na wakati huo huo aliwaalika kukuza na kuimarisha zaidi msingi ambao umetoa uimara na nguvu kwa kazi yao yote tangu mwanzo: kiroho kwa huruma na Mkate Mmoja. amewataka wawe wanafunzi wanyenyekevu wa Kristo wa Ekaristi na wafunuaji pamoja Naye wa uso wa Baba Yh 14:8), kama vile Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alivyopendekeza, ambaye mafundisho yake yanatia moyo (Waraka wa Dives in Misericordia, 1).Wafichue, katika huduma na zawadi zao  wenyewe, huruma ya uso wa Baba. Katika kazi nyingi ambazo wanajishughulisha nazo kila siku, wasisahau kwamba hii ndiyo maana kuu ya matendo yao na wito wao wa msingi. Waige Mungu aliye karibu, mwenye huruma na mwororo; kuwa karibu na watu pia, mwenye huruma, mwenye huruma nyingi na upole.  Kwa sababu Papa amesema kuwa tunahitaji huruma katika Kanisa.

Wafanye kila kitu kwa nia moja: kwamba watu wanaokutana nao wapate kumjua Yeye. Wajaribu, katika kutenda mema, kwa unyenyekevu, ili katika kile wanachofanya Bwana peke yake aonekane na kila mtu aje Kwake. Mtakatifu Faustina Kowalska ni  mchochezi mwingine wa kazi yao, alisema kwamba nafsi yenye unyenyekevu huathiri hatima ya ulimwengu mzima (Katika yake  daftari ya IV, 29.9.37), na hii ni kwa sababu unyenyekevu humfanya mtu kuwa karibu na Mungu na kwa ndugu zake, mwenye uwezo wa kutoa misaada, busara na kimya ambayo hufanya kutoa kwa heshima, kupokea rahisi na kushiriki asili. Kwa hiyo, sikuzote wawe na tabia ya kujikinga na ya upole kwa watu ambao Bwana amewakabidhi, na mtindo wa kujificha, kama wale wazazi, au marafiki, au ndugu wa kiume na wa kike ambao uwepo wao, palipo na uhitaji, ni wa hiari na " kawaida" kwenda karibu bila kutambuliwa.

Papa akisalimiana na mmoja wa wadogo wa Jumuiya Ndogo ya Gela, Kusini mwa Italia
Papa akisalimiana na mmoja wa wadogo wa Jumuiya Ndogo ya Gela, Kusini mwa Italia

Kuwa huko bila kuonekana: hii si rahisi, hii pia ni utakatifu. Papa amekazia kusema kuwa baada ya yote, Mungu anatupenda kwa njia hii: kwa ukuu wa unyenyekevu, wakati kwa dakika, akitupa kila kitu bila kutarajia malipo yoyote! Kwa hivyo hapa kuna mitazamo miwili muhimu ambayo Papa Francisko amewatia moyo na kuwakabidhi ili kuendelea na safari yao: kutokuwa na utulivu Mtakatifu,  kama watoto, ambao hawana utulivu kila wakati  na  pia unyenyekevu mwingi, wa kuwa tayari na thabiti katika kujibu mahitaji ya ndugu zetu na, wakati huo huo, kuwaleta wote katika mkutano wa kibinafsi na uso wa huruma wa Baba.  Papa amesisitiz waendelee,na kuhitmimisha akiomba kwamba wasimsahau katika sala zao.

Hotuba ya Papa kwa Jumuiya ya Gela
06 November 2023, 15:40