Tafuta

2023.11.11  Papa na wahudumy wa Madhabau waliodhuria mkutano wa kimataifa mjini Vatican 2023.11.11 Papa na wahudumy wa Madhabau waliodhuria mkutano wa kimataifa mjini Vatican   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:mapadre waungamishi katika madhabahu wasamehe daima

Papa na wahudumu wa Maeneo Matakatifu,mjini Vatican kwa ajili ya Mkutano wa Pili wa Kimataifa,amependekeza sala,kujali sakramenti na makaribisho ya mahujaji na kuabudu.Papa emekazia kuwafariji wale mahujaji kwa mizigo na matatizo na kuwa na ukaribu wa huruma."2024 ni mwaka wa sala kuelekea Jubilei ya 2025.

Na Angella rwezaula,- Vatican.

Jumamosi tarehe 11 Novemba 2023, Baba Makatifu Francisko amekutana Katika Ukumbi wa Paulo VI na Washiriki wa Mkutano wa II wa Kitaifa wa Gambera na Wasimamizi wa Madhabahu matakatifu Ulimwenguni kote walioanza mkutano huo tangu tarehe 9 Novemba. Akianza hotuba yake amewakatisha wote na kwasababu wanajua vyema umakini wake katika mahali patakatifu. Amemshukuru Askofu Mkuu Rino Fisichella kwa mpango huo na kwa kujitolea kwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji katika uchungaji wa Maeneo Matakatifu. Ni mahali pekee ambapo watakatifu, watu waaminifu wa Mungu humiminika kusali, kufarijiwa na kutazamia wakati ujao kwa uhakika zaidi. Baba Mtakatifu amesema tunafika mahali Patakatifu, kwanza kabisa kuomba. Kwa upande wetu, ni muhimu kwamba wasiwasi kwamba Mahali Patakatifu ni mahali pa pekee pa kusali na daima kunabaki hai. Baba Mtakatifu anajua jinsi ambavyo Ekaristi Takatifu inavyoadhimishwa sehemu hizo  kwa uangalifu mkubwa na jinsi juhudi nyingi zinavyowekwa kwa ajili ya Sakramenti ya Upatanisho.

Katika muktadha huo Baba Mtakatifu amependekeza kuwa katika uchaguzi wa mapadre kwa ajili ya Maungamo, pawe na utambuzi mzuri, ili wale wanaojitokeza kwenye maungamo wakivutwa na huruma ya Baba wasipate vikwazo vya kupata upatanisho kamili. Sakramenti ya Upatanisho ni kusamehe, daima, kusamehe. Haiwezi kutokea, hasa katika mahali Patakatifu, kwamba wakutane na vizuizi, kwa sababu ndani yao huruma ya Mungu inaombwa kuoneshwa kwa njia ya ajabu sana, kwa asili yake. Hivi ndivyo waamini wanavyo waona kama mahali maalum pa kukutana na neema ya Mungu, daima kusamehe kama vile Baba anavyosamehe.  Na hivyo nao wasemehe, Papa amekazia. Katika historia ya kila Madhabahu  ni rahisi kujionea moja kwa moja imani ya watu wetu waamini inayohifadhiwa hai na kulishwa kwa sala, kwanza kabisa Rozari inayosaidia kusali kwa njia ya kutafakari mafumbo ya maisha ya Yesu na Kristo na Bikira Maria. Kuingia kiroho katika mafumbo hayo, kuhisi kuwa sehemu hai ya kile kinachounda historia yetu ya wokovu, ni ahadi tamu, ambayo inatoa ladha ya Injili kwa maisha ya kila siku.

Ni muhimu kwamba umakini maalum upewe kwa kuabudu sehemu za madhabahu matakatifu. Papa Francisko amedokeza kuwa tumepoteza kidogo hisia ya kuabudu, lazima tuitafute  tena. Labda tunahitaji kuipata kutoka katika mazingira ya makanisa yetu  ambayo hayatualiki kila wakati kukusanyika na kuabudu. Kukuza uzoefu wa ukimya wa kutafakari kwa mahujaji na ambayo sio rahisi kwa kuabudu kwa ukimya, kunamaanisha kuwasaidia kutazama mambo muhimu ya imani. Ibada sio kuachana na maisha; bali ni nafasi ya kutoa maana kwa kila kitu, kupokea zawadi ya upendo wa Mungu na kuweza kuitolea ushuhuda katika mapendo ya kidugu. Papa Francisko amesisitiza kuwa katika hili tunaweza kujiuliza swali: "Na mimi, je, nimezoea sala ya kuabudu?" Ni muhimu kujibu.

Pia tunakwenda kwenye Mahali patakatifu ili kufarijiwa. Hapo kuna siri ya faraja. Ni watu wangapi wanaokwenda huko kwa sababu wamebeba mzigo, maumivu, wasiwasi katika roho na miili yao! Ugonjwa wa mpendwa, wa kupoteza mjumbe wa familia, hali nyingi za maisha mara nyingi ni sababu za upweke na huzuni, ambazo huwekwa kwenye madhabahu na kusubiri majibu. Faraja sio wazo la kufikirika, na halifanywi kwanza kabisa na maneno, bali kwa ukaribu wa huruma na upole, unaojumuisha maumivu na mateso. Huu ndiyo mtindo wa Mungu wa ukaribu, huruma, na upole. Hivi ndivyo Bwana alivyo, Papa Francisko amesisitiza. Kufariji ni sawa na kufanya huruma ya Mungu ionekane; kwa sababu hii huduma ya faraja haiwezi kukosekana katika madhabahu zetu.

Wale wanaotunza Mahali Patakatifu lazima wafanye maneno ya Mtume kuwa yao wenyewe akisema: "Yeye hutufariji katika dhiki zetu zote, ili na sisi tuweze kuwafariji wale wanaojikuta katika kila aina ya dhiki kwa faraja ambayo sisi wenyewe tunafarijiwa na Mungu” (2Kor 1:4). Mara moja, mbili, tatu, nne katika mistari miwili neno faraja au faraja: andiko hili la Paulo ni zito, Papa amekazia. Kwa hiyo amesema kuwa Ninaweza kuwa ishara yenye matokeo ya faraja kwa kadiri ambayo mimi binafsi nimepitia nikifarijiwa na mateso ya kuokoa ya Yesu na kupata kimbilio Kwake. Kwa hiyo amehimiza wasisahau. Katika historia yetu, kila mmoja wetu ana nyakati ngumu, mbaya, ambazo Bwana alitufariji. Wasisahau hilo. Kukumbuka uzoefu wetu wenyewe wa kufariji kutatusaidia kuwafariji wengine. Na uzoefu huu unapitia umama wa Maria Mfariji. Faraja na rehema zijae katika mahali Patakatifu petu!

Hatimaye, Papa amesema tunakwenda kwenye madhabahu kutazama siku zijazo kwa ujasiri zaidi. Mhujaji anahitaji matumaini. Anatafuta katika tendo lenyewe la kuhiji: anatoka kutafuta mahali salama pa kufikia. Anaomba tumaini kwa maombi yake, kwa sababu anajua kwamba ni imani rahisi na ya unyenyekevu tu inayoweza kupata neema anayohitaji. Kwa hiyo ni muhimu kwamba, anaporudi nyumbani, ajisikie ameridhika na amejaa utulivu kwa sababu ameweka tumaini lake kwa Mungu.  Katika Madhabahu zetu  Papa ameongeza kuuwa umakini mwingi hupewe kwa kuwakaribisha watu na hivyo wasisahau hili amekezia kusema hasa kwa  kuwakaribisha mahujaji vizuri na ndivyo ilivyo. Wakati huo huo, huduma ya kichungaji inapaswa kutolewa wakati mahujaji wanapoondoka mahali Patakatifu pa kurejea katika maisha yao ya kawaida: kwamba wapokee maneno na ishara za matumaini, ili hija iliyokamilika ifikie maana yake kamili.

Baba Mtakatifu amewambia alivyopendelea mwaka 2024 katika kuelekea  matarisho ya mwaka wa Jubilei ya 2025, uwe kwa ajili ya maombi kamili. Kwa hiyo maelezo na msaada vitachapishwa hivi karibuni ambayo inaweza kukusaidia kugundua tena umuhimu wa maombi. Katika hilo Papa amependekeza kuwa kutakuwa na usomaji mzuri, ambao unawachochea kuomba kwa urahisi na kulingana na moyo wa Kristo. Kila siku tutafanya upya furaha na kujitolea kuwa wanaume na wanawake wa maombi. Iwe sala kutoka moyoni, si kama kasuku. Hapana kutoka moyoni. Maneno yaliyosemwa yatoke moyoni. Wao, katika mahali Patakatifu, watafanya hivyo kupitia hali ya kiroho inayowatambulisha. Kutoka mahali Patakatifu zote, wimbo wa shukrani uinuliwe kwa Bwana kwa ajili ya maajabu anayotend hata katika siku zetu. Na tuombe maombezi ya Mama wa Mungu ili, katika kipindi hiki kigumu sana, kaka na dada zetu wengi wanaoteseka wapate amani na matumaini tena. Papa anawasindikiza kwa Baraka zake. Amewaomba tafadhali, katika Madhahabu  yao, wamkumbue kumwombea pia.

Papa na wahudumu wa Madhabahu duniani
11 November 2023, 13:16