Papa Francisko,kuna uhusiano kati:sanaa,historia na utamaduni
Na Angella Rwezaula, Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Walinzi wa Sanaa za Majumba ya Makumbusho mjini Vatican, Alhamisi tarehe 9 Novemba 2023. Katika hotuba yake amewashukuru kwa mara nyingine tena kwa ushirikiano wao katika umuhimu wa kazi ya kuhifadhi na kukarabati urithi wa kisanaa na kiutamaduni wa Majumba ya Makumbusho mjini Vatican. Shughuli yao ni ishara ya dhati ya kupongezwa kwa ajili ya nguvu ambayo inahusiana na usanii katika mitindo yake mingi, kufungua akili na mioyo kwa uzuri wa uumbaji na utajiri wa fumbo wa maisha yetu na wito wetu wa kibinadamu. Kazi ya kuhifadhi ambayo ni muhimu katika urithi wa thamani wa wakati uliopita, inaalika hata vizazi vipya kutafakari juu ya msukano huo kati ya sanaa, historia, utamaduni na imani. Papa ameongeza tena kusema kuwa kuna msukamo kati ya mambo hayo ya: sanaa, historia, utamaduni na imani.
Baba Mtakatifu Francisko amesema wao kama Walinzi wa Sanaa wa Makumbusho ya Vatican ni kuhakikisha kwamba hazina za kisanii za makusanyo ya Vatican, ambayo yanaakisi utofauti mkubwa wa tamaduni, mila na usemi wa ubunifu unaorutubisha ulimwengu, unaweza kuendelea "kuhamasisha, kuinua na kufichua" matumaini na matarajio ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu. Sanaa, na sanaa ya kidini hasa, inaweza kuleta ujumbe wa huruma, kujali na kutia moyo sio tu kwa waamini, lakini pia kwa wale wanaotilia shaka, wanaohisi kupotea, kutokuwa na uhakika au labda wako peke yao. Kwa sababu sanaa daima inazungumza na roho. Ina uwezo wa kukuza utambuzi wa ubinadamu wetu wa pamoja, kujenga madaraja kati ya tamaduni na watu, na kuunda hisia ya mshikamano tunaohitaji katika ulimwengu wetu uliogawanyika kwa huzuni na ulioharibiwa na vita. Sanaa hutengeneza upya roho ya mwanadamu, kama vile maji yanavyotengeneza upya jangwa kavu na kame.
Historia ya miaka arobaini ya Walinzi imechochewa sio tu upendo wa sanaa, lakini pia na imani kwamba kila kizazi kina jukumu la pamoja la kulinda na kuhifadhi urithi wa thamani ambao umekabidhiwa kwetu. Ufahamu huu umezaa matunda katika kazi muhimu za urejeshaji zilizofanywa katika miongo minne iliyopita na, hasa, wakati wa miaka ya kufungwa kwa sababu ya janga la uviko. Kwa hisia hizo, Baba Mtakatifu Francisko, amerudia kutoa shukrani zake tena kwa msaada wao kwa ajili ya utume wa Makumbusho ya Vatican na amewahimiza kudumu katika kazi hiyo nzuri. Juu yao familia zao na wale wote wanaohusishwa na kazi ya Ulinzi wa Sanaa, amewaombea kwa moyo mkunjufu baraka za Mwenyezi Mungu, chanzo cha milele cha uzuri wote, ukweli na wema.
Walinzi wa sanaa za Makumbusho ya Vatican: Miaka 40 ya huduma ya sanaa na imani
Ikumbukwe tangu Jumatatu tarehe 6 Novemba hadi 10 Novemba 2023, imeanzishwa shughuli ya uchangiaji na ufadhili ambayo imeruhusu urithi wa thamani kuhifadhiwa na kuthaminiwa na ambayo inaadhimishwa kwa mfululizo wa mipango. Na hii ilikuwa 1983 wakati "Walinzi wa Sanaa katika Makumbusho ya Vatican" walianzishwa kati ya California na New York. Mwaka mmoja mapema Vatican ilikuwa imehamaisha maonesho ya kusafiri yenye kichwa “The Vatican Collections” nchini Marekani yaani mkusanyo wa Vatican. Upapa na Sanaa”. Maonesho hayo yaliwaamsha wageni wengi hamu ya kushiriki na kujifanya kuwa wa manufaa kwa michango ya hisani.
Wafadhili wa kisasa na wazamani
Warithi wa ulinzi wa zamani na hivi karibuni "Marafiki wa Jumba la Makumbusho la Vatican" zaidi ambao mwishoni mwa miaka ya 1960 walichangia kuunda mkusanyiko wa kipapa wa sanaa ya kisasa ya kidini, iliyoungwa mkono kwa nguvu na Paulo VI, Walinzi leo hii wako katika Amerika kadhaa, serikali na katika nchi zaidi ya tisa duniani kote, zikiwemo za Ulaya na Asia, zenye shughuli kubwa ya uchangishaji fedha.