Tafuta

2023.11.09 Wajume washauri wa Shirika la  Kaburi Takatifu la Yerusalemu walikutana na Papa mjini Vatican. 2023.11.09 Wajume washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu walikutana na Papa mjini Vatican.   (Vatican Media)

Papa kwa washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu,Elimu ni kwa maisha yote!

Kwa bahati mbaya tupo tunashuhudia janga ambalo linamaliza hasa katika maneno ambayo Bwana aliishi,mahali ambapo alitufundisha kwa njia ya ubinadamu wake kupenda,kusamehe na kufanya wema kwa wote.Ni maneno ya Papa aliyowalekea Novemba 9,Wajumbe Washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 9 Novemba 2023  amekutana na Wajumbe washiriki katika Mashauri ya Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu. Katika hotuba yake ameanza na salamu kwa Mkuu wa Kikanisa anayewakilisha Shirika hilo na pia kwa namna ya pekee kwa Kardinali Fernando Filoni Mkuu Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalemu, amemshukuru na kwa shirika zima lililoenea ulimwenguni pote. Papa amebainisha jinsi ambavyo wamekusanyika jijini Roma kwa ajili ya Ushauri, ambao unajumuisha mkutano wa Luteni, Wajumbe wa shirika ambapo  mwaka huu pia Maaskofu Wakuu wastaafu, kujadili mada ya malezi. Mafunzo ya lazima kwa wagombea wanaotaka kuingia katika Shirika; malezi endelevu kwa wale ambao tayari wanashiriki katika maisha na utume wake; na pia mafunzo ya wale walioitwa kushika nyadhifa za wajibu, pamoja na mambo mawili: ya kiroho, katika ufahamu wa ahadi ya juu ya maadili inayofanywa mbele ya Altare; na ile inayohusiana na mpangilio wa shughuli na usimamizi wa kiutawala wa rasilimali, kuendelea na kukidhi mahitaji ya Nchi Takatifu.

Wajumbe washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu na Papa
Wajumbe washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu na Papa

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amekazia kuwa mafunzo ya awali na yanayoendelea, ya vitendo na ya kiroho: hii ni miongozo minne ambayo tunaweza kuona ikiwakilishwa katika ishara ya Msalaba, ambayo inaonekana wazi kwenye nguo zao na ambayo uhuisha hali yao ya kiroho. Kwa mkono wake mlalo unakukumbusha kujitolea ili kuhakikisha kwamba kujitolea kwa Kristo aliyesulubiwa na kufufuka kunakumbatia maisha yao yote na katika upendo huwafanya wawe karibu na kila kaka na dada; huku ikiwa na ule wa wima, uliopandwa vyema ardhini na ukitazama anga, ambao unakukumbusha juu ya ukamilishano wa lazima, katika safari yao, kati ya maisha ya sala na huduma ya ndugu zao, wasikivu, wenye sifa, wenye kukita mizizi katika ukweli ambao ndani yao  wanaofanya kazi, inayolenga manufaa kamili ya mtu.

Papa na wajumbe washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu
Papa na wajumbe washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu

Kwa mantiki hiyo, Sheria  ambapo Papa Francisko aliidhinisha  kuhusu shirika hilo  amesema zinaunda njia kuu ya kuhamia kama Shirika la  Walei, kwa madhumuni ambayo tayari yalieleweka vyema na Mwenyeheri Papa Pio IX na kisha kuthibitishwa na warithi wake: kuwashirikisha wanaume na wanawake ambao wamejitolea kushiriki kikamilifu kwa maisha ya Kanisa, kuanzia yale ya Kanisa  “Mama” la Yerusalemu, kulingana na mafundisho ya mtume Paulo(rej. 1 Cor 16,3), na kuufungua ulimwengu wote. Katika pumzi hiyo ya ulimwengu Papa amesema wao wameitwa kuwa Shirika ambalo likiwa na nguvu katika utambulisho,linashiriki fumbo la upendo kwa namna nzuri zaidi, lililo wazi na linalowezekana, tayari kuchukua wajibu wa huduma zile ambazo Bwana anaomba kupitia mahitaji ya ndugu, kuanzia elimu ya awali katika mashule hadi mshimakamo wa dhati na aina nyinghine dhaifu zaidi, kama vile wazee, wagonjwa na wakimbizi.  Papa Francisko amewahimiza kwamba hapo wakumbuke daima kwania itakua kama kiitikio chaka ambacho Bwana alifanya wasmea kwa wote manabii wa Agano la kale: wajane, yatima, na mgeni. Ndiyo wajibu wetu tulio nao.

Papa amekutana na wajumbe washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu
Papa amekutana na wajumbe washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu

Baba Mtakatifu Francisko amesema, Kaburi wazi, ambamo wito wao kwa karne nyingi wanajikita nayo kuwa walinzi maalum ni kwa maana hiyo hasa ishra ya upendo usi ona vizinginta vya Msalaba, ambao kwayo hauchukui lolote na kwa hiyo hauweze kufungwa na kamba za kifo, ni shara ya ushindi wa Mfufuka ambaye hata sisi tunapata maisha (Rm 6,8-9) na nguvu ya Fumbo la Mwili wake na Daamu yake ambayo inatuunganisha wote kama wajumbe wake (rej.1 Cor 10,17). Mafunzo na kujifunza, mwanzoni mwa safari ya nadhiri na katika maisha yote. Elimu ni kwa maisha yote.  Kufunda na kujifunza kutoa msaada wa ulimwengu na jumuishi. Kusoma historia ya Shirika  lao kwa mtazamo huo na, katika muktadha wa kusikiliza na maombi, kujishughulisha mwenyewe kupata ujuzi wa kujibu mahitaji ya wengine: hii ndiyo huduma kubwa ambayo wanaweza kufanya leo  hii kwa Kanisa na kwa ulimwengu. Katika kila zama, hata katika zama zetu zilizo na dhana ya kiteknolojia, kuna hitaji kubwa la watu wanaotumia hisani kwa akili na mawazo. Kwa hiyo Papa Francisko amewaomba waendelee na kazi zao kwa mtindo huu na kuusambaza kwa uaminifu katika awamu mbalimbali za malezi.

Papa ameomba zawadi ya amani kwa ajili ya nchi Takatifu

Kabla ya kuhitimisha, Papa Francisko amependa kuwalekeza wao pamoja wazo la Nchi Takatifu. Kwa bahati mbaya tupo tunashuhudia janga ambalo linamaliza hasa katika maneno ambayo Bwana aliishi, mahali ambapo alitufundisha kwa njia ya ubinadamu wake kupenda, kusamehe na kufanya wema kwa wote. Na kinyume chake tunaona mateso yalyotapaa ya ajabu ambayo yanawakumba hasa wengi wasio na hatia. Kwa njia hiyo niko kiroho na ninyi ambao kwa hakika mnaishi mkutano wa ushauri, mkishirikishana kwa uchungu muuu wa Mama Kanisa la Yerusalmea na kuomba zawadi ya amani. Na Bikira maria ambaye wao wanamuomba kwa jina la Malkia wa Palestina, awasaidiea daima katika utume wao. Kwa moyo wote, Baba Mtakatifu amewabariki na wajumbe wote wa shirika pamoja na familia zao. Amewahimiza nao wasisahau kusali kwa ajili yake.

Papa na wajumbe washauri wa Shirika la Kaburi Takatifu la Yerusalemu
09 November 2023, 14:52