Tafuta

Papa Francisko:kuwa na furaha ya imani miongoni mwa wasioamini

Katika katekesi ya Papa Jumatano 8 Novemba ameendeleza ari ya kitume na kutazama sura ya Madeleine Delbrêl wa ufaransa kama kielelezo cha shauku katika utangazaji wa Injili.Alijifananisha na mwendo wa baiskeli kwamba ni kwa kutembea na kukimbia tu inaweza kuishi uthabiti wa Imani na unapoacha unapoteza roho hiyo.Uwiano wa Mkristo upo katika msukumo wa upendo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 8 Novemba 2023 akiwa mbele ya waamini na mahujaji waliofika katika Uwanaja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican katika katekesi yake kuhusu Shauku ya uinjilishaji: ari ya kitume ya mwamini amejikita na sura nyingine ya Madeleine Delbrêl aliyekuwa na Furaha ya imani miongoni mwa wasioamini. Baba Mtakatifu akianza tafakari ya katekesi amesema miongoni mwa mashuhuda wengi wa shauku ya kutangaza Injili, waeneza Injili hao wenye shauku, leo hii nitawasilisha mwanamke Mfaransa wa karne ya ishirini, mtumishi anayeheshimika wa Mungu Madeleine Delbrêl. Alizaliwa mnamo mwaka 1904 na alikufa mwaka 1964, alikuwa mfanyakazi wa kijamii, mwandishi na mtafakari mafumbo, na aliishi kwa zaidi ya miaka thelathini katika viunga vya maskini, vya wafanyakazi wa Paris.

Papa akisalimia umati katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa akisalimia umati katika uwanja wa Mtakatifu Petro


Akiwa ameangaziwa na kukutana na Bwana, aliandika: “Tunapofikia kujua neno la Mungu, hatuna haki ya kutolipokea; mara tu tunapolikea, hatuna haki ya kutoliacha lipate mwili ndani yetu; mara linapofanyika mwili ndani yetu, hatuna haki ya kuihifadhi kwa ajili yetu wenyewe: kuanzia wakati huo na kuendelea, sisi ni wa wale wanaolingoja” (Utakatifu wa watu wa kawaida, Milano 2020, 71). Ni kitu kizuri alichokiandika, ameongeza kusema Papa. Baada ya ujana wake ambao aliushi akiwa haamini chochote akiwa na umri wa karibu ishirini Madeleine alikutana na Bwana, akashangazwa na ushuhuda wa marafiki wengine ambao walikuwa waamini. Alianza kumtafuta Mungu, akitoa sauti kwa kiu kuu ambayo alihisi ndani yake, na akaja kujifunza kwamba “utupu uliokuwa ukilia uchungu wake ndani yake” ni Mungu aliyemtafuta.

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa
Papa alilakiwa namna hii
Papa alilakiwa namna hii


Baba Mtakatifu Francisko amesesisitza kuwa Madeleine alikuwa na moyo wa kupendeza kila wakati, na alijiruhusu kupingwa na kilio cha maskini. Alihisi kwamba Mungu Aliye Hai wa Injili anapaswa kuwaka ndani yetu hadi tunalipeleka jina lake kwa wale ambao bado hawajalipata. Katika roho hiyo, iliyoelekezwa kuelekea misisimko ya ulimwengu na kilio cha maskini, Madeleine alihisi kuitwa “kuishi upendo wa Yesu kikamilifu na kwa barua, kutoka kama mafuta ya Msamaria mwema hadi siki ya Kalvari, na hivyo kumpa upendo, kwa upendo… kwa sababu, kwa kumpenda pasipo kujibakiza na kujiruhusu kupendwa kabisa, zile amri kuu mbili za mapendo zinafanyika mwili ndani yetu na kuwa moja” ( Wito wa Upendo , 138-139).

Papa akibariki wanandoa wapya
Papa akibariki wanandoa wapya


Hatimaye, Madeleine Baba Mtakatifu amsema anatufundisha jambo lingine: kwamba kwa kueneza Injili mtu huinjilishwa: kwa kuinjilisha tunainjilishwa. Kwa hivyo, alizoea kusema, akirudia Mtakatifu Paulo: "Ole wangu ikiwa ninahubiri injili, sijihubiri mwenyewe". Hakika, kueneza Injili ni kumhubiria mtu. Na hili ni fundisho zuri, Papa ameongeza, kwa njia hiyo basi tukitazama ushuhuda huu wa Injili, sisi pia tunajifunza kwamba katika kila hali ya kibinafsi au kijamii au hali ya maisha yetu, Bwana yuko na anatuita kukaa wakati wetu wenyewe, kushiriki maisha yetu na wengine, kuchanganyika na furaha na huzuni za dunia hii. Hasa, anatufundisha kwamba hata mazingira ya kidunia yanasaidia katika uongofu, kwa sababu kuwasiliana na wasioamini kunamsukuma mwamini kufanya marekebisho ya mara kwa mara ya njia yake ya kuamini na kugundua upya umuhimu wake wa imani Madeleine Delbrêl na atufundishe kuishi imani hii “katika mwendo”, kwa kusema, imani hii yenye matunda ambayo hufanya kila tendo la imani kuwa tendo la upendo katika kutangaza Injili. Papa Francisko amehitimisha.

Katika katekesi ya Papa Novemba 2023 ni sura ya mtumishi wa Mungu mfaransa
08 November 2023, 13:20