Tafuta

2022.11.15 nembo ya Mpango uitwao  Uniservitate  global wa Vyuo Vikuu  kuhusu mkataba wa kimataifa wa Elimu 2022.11.15 nembo ya Mpango uitwao Uniservitate global wa Vyuo Vikuu kuhusu mkataba wa kimataifa wa Elimu 

Papa Francisko:elimu ya vijana huleta udugu,amani na haki duniani

Katika ujumbe wa Papa Francisko uliosomwa mwishoni mwa Kongamano la IV la Kimataifa la Vyuo Vikuu ambalo lilifanyika tarehe 8 na 9 Novemba 2023 huko Manila,Ufilippini, anawahimiza haja ya kukuza kwa vijana ufahamu zaidi wa uhusiano unaopaswa kuwepo kati ya lugha za akili,moyo na mikono.

Vatican News.

Katika mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko wa kujenga ulimwengu ulio bora kwa njia ya elimu inayohimiza haki na amani, Kongamano la IV la  Vyo vikuu duniani lililowaleta pamoja wataalamu wa masuala ya elimu, lilihitimishwa tarehe 9 Novemba ambalo lilikuwa la siku mbili  katika Chuo Kikuu cha La Salle, jijini Manila  nchini Ufilippini. Ni Uniservitate ambao ni mpango wa kukuza huduma ya kujifunza na mshikamano katika taasisi za Kikatoliki za elimu ya juu zinazozingatia Mkataba wa Kielimu wa Kimataifa wa Papa Francisko, unaotaka kutoa elimu muhimu kwa vizazi vipya, kuwashirikisha katika kujitolea kikamilifu kwa matatizo ya wakati wetu ili waweze kuwa wahusika wakuu wa mapendekezo ya kuleta mabadiliko na wahamasishaji wa amani na udugu kwa mabadiliko ya kijamii.

Papa Francisko:mafunzo ya dhati na sio taarifa tu

Kabla ya kufungwa  kwa siku  ya pili na ya mwisho ya Kongamano, ujumbe wa Papa Francisko ulisomwa, ambapo alisisitiza haja ya kukuza kwa vijana ufahamu zaidi wa uhusiano unaopaswa kuwepo kati ya lugha za akili, moyo na mikono. Kwa njia hiyo  Papa alisema waelimishaji wataweza kutoa mafunzo, na sio tu kuwajulisha, wale walio chini ya wajibu wao, ili kila mtu ajifunze kufikiri kulingana na kile anachohisi na kufanya; kuhisi kupatana na kile wanachofikiri na kufanya; na kufanya kupatana na yale wanayohisi na kufikiria.”

Vijana wanaweza kujenga ulimwengu bora

Ni mkataba wa  elimu ambao unahitaji mbinu bunifu, za kimfumo na zisizo na nidhamu ili kuwasaidia vijana kuwa viongozi na wahusika wakuu katika kujenga mustakabali bora wa jamii yote. Wakati huo huo, Papa anabainisha kwamba umuhimu wa mwelekeo wa kiroho katika elimu hauwezi kupuuzwa ambao unapaswa kuwasukuma vijana kutumikia manufaa ya wote kama wanafunzi wa kimisionari, wenye uwezo wa kuleta ukweli wa mabadiliko, uzuri na furaha ya Injili kwa watu wote wa familia ya binadamu, hivyo kuendeleza ufalme wa Mungu wa mshikamano wa kidugu, haki na amani".

Mwaka 2024 Kongamano litafanyika Lumsa

Matoleo mawili ya kwanza ya Kongamamo la Uniservitate ulimwenguni la Vyuo Vikuu  mnamo 2020 na 2021, yalifanyika kwa sababu ya mapungufu yaliyotokana na janga la Uviko-19. Mwaka 2022, toleo la tatu lilifanyika katika Chuo Kikuu cha LUMSA, Roma ambacho mwaka 2024 pia kitakuwa ni mwenyeji wa Kongamano la V la Global la Uniservitate. Mnamo Oktoba mwaka 2022, Papa Francisko alipokea hata wanafunzi walioshinda wa Tuzo ya Uniservitate ya 2022 na kuwahimiza kuendelea kufanya kazi katika mipango ya aina hii.

Ujumbe wa Papa kwa vijana wa Manila
10 November 2023, 16:13