Papa atoa wito wa kuacha vita.Kuna mateso makubwa!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mara baada ya tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko, Jumatano tarehe 8 Novemba 2023, ametoa mwaliko wake tena, wakati akisalimia waamini kwa lugha ya kitaaliano baada ya tafakari yake iliyojikita katika sura ya Madeleine Delbrêl, Mfaransa mtafakari fumbo, mfanyakazi wa kijamii, mwandishi wa insha na mshairi na kusema kuwa, Tufikiri na kuwaombea watu wanaoteseka na vita. Tusiisahau Ukraine iliyoteswa na kuwafikiria Wapalestina na Waisrael: Mungu atuongoze kwenye amani ya haki. Tunateseka sana: watoto wanateseka, wagonjwa, wazee wanateseka na vijana wengi wanakufa. Vita daima ni kushindwa: tusisahau hili. Daima ni kushindwa.
Papa Francisko akiendelea amesema anavyowakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano, hasa kwa wamini wa Altamura, Mtakatifu Salvatore Telesino na Petronà. Amewakaribisha kikundi cha kujitolea cha Unitalsi cha Emilia-Romagna, kikundi kutoka Hospitali kuu ya Milano na Sanaa ya Muziki Mtakatifu kwa upendo maalum. Na kama kawaidia amewasalimia vijana, wazee, wagonjwa na wanandoa wapya .
Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha hata hivyo litutujia ya Kanisa kuhusu Kutabaruku Basilika ya Mtakatifu Yohane , Laterano ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 9 Novemba ya kila mwaka na ambalo ni Kanisa kuu la Roma, Kanisa kuu la Papa, kama askofu wa Roma. Kwa hiyo Papa ameongeza kusema kuwa Tukio hili na liamshe kwa kila mtu hamu ya kuwa mawe yaliyo hai katika utumishi wa Bwana.
Baba Mtakatifu akiendelea katika salamu zake kwa lugha mbali mbali zaidi ya hayo, baraza ziliwaendea wanaozungumza Kiarabu, ambapo Papa ameomba ulinzi dhidi ya uovu wote na amemwomba Bwana Yesu hasa kwa zawadi ya Ujasiri wa kufanya kazi pamoja na wale wote wanaofanya kazi duniani ili kuikomboa dunia dhidi ya uovu na kuirudisha kwenye wema wake wa awali.
Papa Francisko akiwageukia kati ya vikundi vingine vya mahujaji, wanaozungumza Kifaransa, aliwasalimia washiriki wa Jumuiya ya Kitaifa ya Jumuiya za Familia za Kikatoliki. Kisha aliongeza kutoa mwaliko kuwa: Tukiwa tunakabiliana na ulimwengu wetu wa kiulimwengu, tusilalamike, bali tuone ndani yake wito wa kuthibitisha imani yetu na mwaliko wa kuwasilisha furaha ya Injili kwa wale wote wenye kiu ya Mungu. Tumwombe Bwana neema ya kushuhudia kwa imani yetu kila siku na udugu na urafiki wa uzoefu na kila mmoja.
Hatimaye, Mrithi wa Petro hakukosa kutaja, katika salamu zake kwa mahujaji wa Kipoland, kumbukumbu ya karibu ya kurudiwa kwa uhuru wa Poland, ambayo itaadhimishwa tarehe 11 Novemba. Baba Mtakatifu amesema Sikukuu hii inawahimiza kuwa na shukrani kwa Mungu, na kuongeza kusema hasa kwa: kurithisha historia yao kwa vizazi vipya.