Papa Francisko abatiza mtoto wa Kiukreni huko Mtakatifu Marta
Vatican News
Ulikuwa ni wakati wa furaha kubwa katika kipindi kigumu kweli. Hivi ndivyo wazazi vijana wa Kiukraine wa Zakhariy, mtoto wa miezi mitatu aliyebatizwa na Papa Francisko katika kikanisa cha Nyumba ya Mtakatifu Marta alasiri ya Jumatatu tarehe 6 Novemba 2023 walibainisha. Jina la kijana baba wa mtoto ni Vitaly, mwenye umri wa miaka 37, na jina lake mama wa mtoto ni Vita, mwenye umri wa miaka 35, na mtoto mdogo ni wa mwisho kati ya watoto kumi, wavulana saba na wasichana watatu. Wanaishi Kamianets-Podilskyi, magharibi mwa Ukraine, katika eneo lililo salama kutokana na vita vilivyoanzishwa na Urussi tangu mwezi Februari 2022. Wazazi hawa wako kwenye harakati ya Waneokatekumenali na katika miaka ya hivi karibuni wamepata uzoefu mkubwa wa utunzaji katikati ya shida nyingi za kifamilia, zilizozidishwa zaidi baada ya uvamizi wa Urusi.
“Tunakabili kila jambo kwa shukrani kwa Mungu, kwa sababu sikuzote Mungu huitunza familia yetu,” alisema mama wa mtoto mdogo: “Kuna vita nchini” na “ni vigumu sana. Kila mtu anasali kwamba vita hivi viishe hivi karibuni, kwamba wafungwa wote warudi nyumbani na kwamba hakutakuwa na mauaji tena. Kwa ubapande wa tukio hlo wamesema Ubatizo wa tarehe 6 Novemba ulikuwa zawadi kubwa kwa familia yao na kwamba "Sikuweza hata kuota kwamba tungeweza kuwa na Baba Mtakatifu na kwamba angeweza kumbatiza mtoto wetu. Lakini Mungu anafanya historia na sisi ya ajabu sana, ambayo bado hatuelewi kikamilifu."
Pia alikuwepo katika ibada hiyo Monsinyo Leon Dubrawski, Askofu wa Kamianets-Podilskyi ya Walatini, ambaye alikumbuka jinsi upendo wa Mungu unavyopitishwa kutoka kizazi hadi kizazi kupitia familia. Alikuwa askofu aliyewasindikiza wanandoa hao vijana hadi mjini Vatican. Papa Fransisko anaendelea kuukumbusha ulimwengu juu ya janga la watu wa Kiukreni walioteswa": Ubatizo wa Zakhariy mdogo ni tumaini jipya kwa familia hii changa na kubwa ambayo haiwezi kusahau vita lakini inaendelea kuwa na imani katika siku zijazo za amani.