Tafuta

Papa:kuna haja ya kujifunza kutoka kwa watoto

Maisha ni zawadi!Mungu anatupenda!Sisi sote ni ndugu!Mmekuja hapa kutoka ulimwenguni pote kama vile ndugu katika nyumba kubwa ambayo Yesu alitupatia,familia kubwa ya kike na kiume.

Na Angella Rwezaula,- Vatican

Tunahitaji kujifunza kutoka kwa watoto. Ninafurahi kila wakati ninapokutana na ninyi kwa sababu mnanifundisha kitu kipya kila wakati. Kwa mfano, mnanikumbusha jinsi ambavyo maisha ni mazuri katika unyenyekevu wake, na jinsi ilivyo vizuri kuwa pamoja! Ni zawadi kuu mbili ambazo Mungu ametupatia ya  kuishi na kuweza kuwa pamoja." Baba Mtakatifu Francisko amesema hayo Jumatatu alasiri  tarehe 6 Novemba 2023 alipokutana na watoto kutoka nchi 84 duniani katika maadhimisho ya hafla iliyofadhiliwa na Baraza la Kipapa la  Utamaduni na Elimu, "Watoto wakutane na Papa", kwa kaulimbiu "Tujifunze kutoka kwa  watoto wavulana na wasichana".  Kwa hiyo katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican mkutano huo uliotanguliwa na shamra shamra za Watoto nyimbo na magizo na ambazo zimehitishwa kwa Watoto kuuliza maswali na majibu. Hakika Watoto walichangamka sana kukutana na Papa ambaye kati kati yao alikuwa kama babu yao.

Papa amekutana na watoto elfu 6 kutoka pande za dunia
Papa amekutana na watoto elfu 6 kutoka pande za dunia

Kwa njia hiyo Hotuba ya Papa imesema Asante kutoka moyoni mwangu kwa nyinyi nyote kwa kuja,  wachungaji wenu, na kwa waandaaji wa mkutano huu: kwa Kardinali José Tolentino, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, kwa Padre Enzo Fortunato, kwa familia zenu, na kwa watu na vyama vyote ambavyo vimechangia kutupatia furaha kubwa ya kuwa hapa! Mada ya mkutano wetu ni "Tujifunze kutoka kwa  watoto Wavulana na Wasichana." Hili linaweza kuonekana kama jina geni kwa mtu kusika: “Jifunze kutoka kwa watoto? na kwamba Je! watoto si ndio wanaohitaji kujifunza?” Ndiyo, bila shaka, na bado, hii ndiyo njia: tunahitaji kujifunza kutoka kwao, Papa amekazia kusema.

Watoto kutoka Ulimwenguni wakutana na Papa
Watoto kutoka Ulimwenguni wakutana na Papa

Akirejea juu ya “milipuko ya shangwe kubwa” ambayo washiriki wote walimkaribisha kwayo, Baba Mtakatifu alisema: “Hizi ndizo kelele tunazotaka kuijaza dunia: si zile za mabomu, bali zile za furaha zenu na vicheko vyenu vya furaha, zinatukumbusha sote kwamba uhai ni zawadi nzuri sana, kwamba Mungu anatupenda na kwamba tunataka kushiriki shangwe yake tukiwa kaka na dada. Papa amesema anavyoona hayo machoni pao na tabasamu lao, amesikia kwa sauti zao za kufoka, katika nyimbo walizoimba, na katika milipuko ya shangwe inayotetemeka katika ukumbi huo mkubwa! Hizi ndizo shangwe tunazotaka kuujaza ulimwengu: sio zile za mabomu, lakini zile za furaha yao na kicheko chao cha furaha. Hili ndilo tunalotaka kuuambia ulimwengu. Kwa hivyo Papa amesema tuseme pamoja sasa. Na ameomba warudie pamoja naye kwa sauti kubwa: "Maisha ni zawadi! “Mungu anatupenda!” “Sisi sote ni kaka na dada!” atoto walirudia.

Papa katikati ya watoto alikuwa kama babu yao
Papa katikati ya watoto alikuwa kama babu yao

Papa akiendelea na hotuba amesema, Kiukweli, mmekuja hapa kutoka ulimwenguni pote, kama kaka  na dada tu wengi wanaokutana pamoja katika nyumba kubwa. Ni nyumba kubwa ambayo Yesu ametupatia, familia kubwa ya Kanisa, iliyo wazi kwa watoto wote wa ulimwengu. Kwa sababu ndivyo inavyopaswa kuwa: popote wanapokwenda, kila mtoto duniani lazima ajisikie nyumbani daima, akikaribishwa kila mara kwa upendo mwingi, kwa tabasamu nzuri, kwa kukumbatia, na kubembeleza. Papa amesema anatamani angewakaribisha wote mmoja baada ya mwingine. Kwa kuwa kuna wengi wao, pamoja na kupitia kwao aliowahutubia, wavulana na wasichana wote katika ulimwengu mzima, kuwapatia kumbatio la Mungu, kumbatio la Kanisa, na kumbatio la kila mtu mwema, kwa kumbatio lake.

Ulimwengu wa amani
Ulimwengu wa amani

Hasa kwa wale watoto ambao, kama tujuavyo, kwa bahati mbaya sasa hivi wanateseka kutokana na vita, njaa, magonjwa, majanga ya hali ya tabianchi, na umaskini. Kwa watoto ambao wako hatarini kwa sababu watu wabaya hata huweka silaha mikononi mwao! Watoto hawana haja ya kuwa na silaha mikononi mwao, Papa amesema. Wanahitaji kuwa na vitu vya kuchezea, vitabu, madaftari, na mambo mengine mengi mazuri lakini si silaha! Na pamoja nao , P`apa amesema , ningependa kuwaambia watoto wote wanaoteseka, kwamba hawako peke yao, tuwaweke mioyoni mwetu, tunawaombea, na tunajitolea kufanya kila tuwezalo ili waweze kupata matumaini na utulivu tena hivi karibuni, na ili tabasamu lirudi kwenye nyuso zao. Tabasamu lirudi kwenye uso wa kila mtoto duniani!

Afla ya Watoto katika Ukumbi wa Paulo VI
Afla ya Watoto katika Ukumbi wa Paulo VI

Baba Mtakatifu aidha amesema uwepo wa watoto wapendwa hapo ilikuwa ni ishara inayoingia moja kwa moja kwenye mioyo yetu sisi watu wazima. Ni sauti ya kutokuwa na hatia ambayo inatuhoji na kutufanya tufikirie, ambayo inatulazimisha kujiuliza: Tunafanya nini na ulimwengu wetu, sayari yetu, jamii yetu? Je, ni mustakabali gani tunwaandalia? Haya ni maswali muhimu ambayo hutusaidia kutafakari kwa urahisi wao. Kwa furaha ambayo wanakubali kila kitu kama zawadi, kama zawadi mbele ambayo wanafungua macho yao juu yake, wanashangaa, na kucheka kwa furaha. Kwa hamu yao ya kuwasiliana, kusikiliza, na kusema. Na katika suala hilo, Papa alipendekeza kwamba wasikilize kwa uangalifu wazazi wao na babu na bibi. Wao wanajua, kuwa ni muhimu kuwasikiliza babu na bibi kwa sababu wameishi kwa muda mrefu na wanaweza kuwafundisha mambo mengi.

Hakika ukumbi ulipendeza na watoto wa mataifa 84
Hakika ukumbi ulipendeza na watoto wa mataifa 84

Kwa kuongeza Papa Francisko amebainisha kuwa na kisha, waulize maswali mengi, na kila siku nyumbani, waambie kila kitu kinachotokea kwao. Kwa sababu mawasiliano ni mazuri kwetu sote! Pia wanatusaidia kwa hamu yao ya kucheza pamoja, kuwa pamoja, kushirikisha kile tulicho nacho na wengine. Na wakati mwingine wanatushangaza kwa vitendo vyao, kama wanapotoa busu, kukumbatia mdoli, kipande cha vitafunio vyao na tabasamu. Ni mambo mangapi tunaweza kujifunza ikiwa tutasimama kwa muda kuwa nao! Kwa hivyo kwa mara nyingine tena Papa amewashukuru watoto wapendwa! Na amewambia wakumbuke: kwamba maisha ni zawadi ya ajabu sana, kwamba Mungu anatupenda sana, na kwamba inapendeza kuwa pamoja, kuwasiliana, kushiriki, na kutoa.  Wafanye hivyo kila  kila wakati! Mama yetu atawasaidia. Na amewahimiza kila wakati kumwomba Mama Yetu. Yeye ni Mama yetu. Na mwombee pia. Amehitimisha akisema Asante.

HOTBU YA PAPA KWA WATOTO
06 November 2023, 16:08