Tafuta

Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya pekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi. Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya pekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi.  (AFP or licensors)

Mkutano wa Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28

huu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya pekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi. COP28 ni mahali ambako dunia itatathmini utekelezaji wa Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi, mkataba wa aina yake uliopitishwa mwaka 2015 na kuweka mwelekeo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kulinda uhai na kipato.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Siasa ni wito na si kila mwamini ana wito wa kuwa ni mwana siasa! Ikumbukwe kwamba, siasa si njia pekee inayoweza kuwahakikishia watu haki, kumbe, medani mbali mbali za maisha, ziwe ni mahali ambapo patawasaidia waamini kuweza kuyatakatifuza malimwengu, kwa kujikita katika mchakato wa kutafuta na kudumisha haki, ustawi, mafao na maendeleo ya wengi. Waamini wanahimizwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu hapa duniani! Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe kwa Siku ya Kuombea Amani Duniani kwa Mwaka 2019 anasema, upendo na fadhila za kiutu ziwe ni kwa ajili ya siasa safi inayohudumia haki msingi na amani, kila mtu akijitahidi kujikita katika mafao ya wengi, kama sehemu ya ujenzi wa mji wa Mungu hapa duniani, ili kuendeleza historia ya maisha ya familia ya binadamu.

Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi COP28-Dubai-Falme za Kiarabu
Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi COP28-Dubai-Falme za Kiarabu

Haki na usawa; tabia ya kuheshimiana na kuthaminiana kama binadamu; ukweli, uwazi na uaminifu ni tunu msingi zinazoboresha siasa safi. Papa anasema mwanasiasa bora ni yule anayetambua dhamana na wajibu wake kwa jamii; anayeaminika na kuthaminiwa na jamii; ni kiongozi anayejitaabisha kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi; mwaminifu katika ahadi zake kwa wananchi waliomchagua, daima akijitahidi kujenga na kudumisha umoja na mshikamano, tayari kuchochea mageuzi katika maisha ya watu; kwa kuwasikiliza na kutenda kwa ujasiri! Siasa safi inayojikita katika ujenzi wa amani inatambua karama za watu na inaendeleza majadiliano na watu kuaminiana na kuthaminiana badala ya kuangaliana kwa “jicho la kengeza.” Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anasema, ujumbe mahususi kwa wanasiasa ni kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma kwa jamii. Hayo yamesemwa na Kardinali Parolin alipokuwa anachangia mada kwenye Bunge la Seneti ya Italia mintarafu Askofu Luigi Secco ni mmisionari aliyefariki dunia mwaka 2017. Pamoja na mambo mengine amekazia: Utu, heshima na haki msingi za binadamu; umuhimu wa shule na elimu katika ujumla wake.

COP28 Dubai, Falme za Kiarabu kuanzia tarehe 30 Nov. Hadi 12 Desemba
COP28 Dubai, Falme za Kiarabu kuanzia tarehe 30 Nov. Hadi 12 Desemba

Vatican na COP28: Viwango vya joto duniani vikiwa vimeongezeka na kuvunja rekodi, na matukio ya kupindukia ya hali ya hewa yakileta madhara kwa binadamu duniani kote, mwaka huu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, ni fursa ya pekee ya kubadili mwelekeo na kuchochea hatua za kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi. COP28 ni mahali ambako dunia itatathmini utekelezaji wa Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi, mkataba wa aina yake uliopitishwa mwaka 2015 na kuweka mwelekeo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kulinda uhai wa binadamu na mbinu za kujipatia kipato. Wakuu wa Nchi, mawaziri na washauri na wasuluhishi, sanjari na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraia na maafisa watendaji wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023 huko Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), ili kujadili mustakabali wa mabadiliko ya tabianchi. Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anawakilisha ujumbe wa Vatican kwenye mkutano huu na anashiriki katika sehemu ya kwanza ya mkutano huu. Pamoja naye yupo Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, M.C.C.I, Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini, anayejikita zaidi katika sehemu ya majadiliano ya kidini na tarehe 3 Desemba 2023 atazindua Banda la Imani kwenye Jiji la Expo, Dubai. Baba Mtakatifu Francisko amesikitika sana kukosa fursa hii kutokana na changamoto za afya, kwani ingekuwa pia ni fursa ya kukutana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wanaohudhuria mkutano huu wa COP28.

COP28
30 November 2023, 16:01