Tafuta

Hii ni picha ya Jorge Mario Bergoglio akiwa kijana yaani Papa Francisko wakati akiwa kijana. Hii ni picha ya Jorge Mario Bergoglio akiwa kijana yaani Papa Francisko wakati akiwa kijana. 

"Life.Historia yangu katika Historia"ni kitabu cha Papa katika majira ya vuli

Kitabu kilichochapishwa na HarperCollins,ambacho kitatolewa katika nchi mbalimbali za Ulaya na Amerika kinafungamana na matukio ya kibinafsi ya Papa Francisko na matukio makubwa ambayo yameadhimisha karne ya ishirini hadi leo hii:"Tunapofikia umri fulani ni muhimu,kwetu sisi tukumbuke. Ni zoezi la utambuzi tunalopaswa kufanya kabla hatujachelewa."

Vatican News

"Life yaani Maisha. Historia yangu katika Historia,"  ndicho kichwa cha kitabu kipya cha Papa Francisko ambamo anasimulia kwa mara ya kwanza historia ya maisha yake kupitia matukio ambayo yameweka alama ya ubinadamu, tangu kuzuka kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mnamo mwaka 1939 alipokuwa karibu ana miaka mitatu, hadi leo hii. Kitabu hicho  kitachapishwa na Nyumba ya Vitabu ya HarperCollins kama walivyotangaza. Kwa mujibu wa HarperCollins Italia, wanawakilisha mpango wa kimataifa kwa uchapishaji ambao utachapishwa katika majira ya vuli 2024 nchini Italia, Marekani, Uingereza, Canada, Brazil, Ufaransa, Ujerumani, Mexico, Poland, Ureno, Hispania na Amerika Kusini.

Jinsi Papa Francisko alivyoona matukio ambayo yalibadilisha ulimwengu

Ni kwa mara ya kwanza kwa HarperCollins, shirika la uchapishaji lililo mjini New York, Marekani litachapisha kitabu kuhusu Papa Francisko. Maisha. Historia yangu katika Historia  kwa mujibu wa  taarifa kwa vyombo vya habar, Vaticani kwamba  "ni safari isiyo ya kawaida kwa miongo kadhaa ya kurejea hatua muhimu zaidi za nyakati zetu, kupitia kumbukumbu za Papa. Miongoni mwa hizi: kuanguka kwa Ukuta wa Berlin, mapinduzi ya Videla d'état huko Argentina, kutoa katika mwezi mnamo 1969 na pia Kombe la Dunia la 1986 ambapo Maradona alifunga bao ambalo liliwekwa kwenye historia. Kumbukumbu za mchungaji ambaye, kwa maoni yake ya kibinafsi, anasimulia miaka ya kuangamizwa  kwa Wayahudi mikononi mwa Wanazi, bomu la atomiki huko Hiroshima na Nagasaki, mdororo mkubwa wa kiuchumi wa 2008, kuanguka kwa Minara Miwili huko Marekani. Kujiuzulu kwa Papa Benedikto XVI na mkutano uliomchagua Papa kwa jina la Francis. Yote hayo tunasoma kwamba ni  Matukio ambayo yamefungamana na maisha ya "Papa callejero,” ambaye hufungua tena hazina ya kumbukumbu zake kusema, kwa uwazi unaomtofautisha, nyakati hizo ambazo zilibadilisha ulimwengu.

Mada motomoto zaidi ya mambo ya sasa

Wakati huo huo, Papa Francisko anazindua baadhi ya ujumbe muhimu kuhusu masuala motomoto zaidi ya sasa: kukosekana kwa usawa wa kijamii, mgogoro wa hali ya hewa, vita, silaha za atomiki, ubaguzi wa rangi, vita vya kupendelea maisha. Sauti ya Papa inapishana na ya msimulizi, Fabio Marchese Ragona, mwandishi wa Vatican wa kikundi cha televisheni cha Mediaset, ambaye katika kila sura anaelezea mazingira ya kihistoria ambayo Papa aliishi.

Kukumbuka ili usirudie kufanya makosa

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inaripoti maoni ya Papa kuhusu kitabu hicho kuwa: "Katika kitabu hiki tunasimulia historia ile ya maisha yangu, kupitia matukio muhimu na ya kushangaza ambayo ubinadamu umepitia katika miaka themanini iliyopita. Ni kitabu kinachoona mwanga ili hasa vijana waweze kusikiliza sauti ya mzee na kutafakari juu ya yale ambayo sayari yetu imepitia, ili wasirudie makosa ya zamani tena. Tufikirie kwa mfano vita ambavyo vimewahi kutokea, kusumbuliwa na kuendelea kuitesa dunia. Hebu tufikirie mauaji ya kimbari, mateso, chuki kati ya kaka na dada wa dini mbalimbali! Maumivu kiasi gani! Mara tu tunapofikia umri fulani ni muhimu, hata kwa sisi wenyewe, kufungua tena kitabu cha kumbukumbu na kukumbuka: kujifunza kwa kuangalia nyuma, kwa wakati, na kupata mambo mabaya, yale yenye sumu ambayo tumepatia pamoja na dhambi zilizofanywa, lakini pia kuhuishia kila kitu kizuri ambacho Mungu ametutuma. Ni zoezi la utambuzi ambalo sote tunapaswa kufanya, kabla hatujachelewa!"

Kitabu kipya Papa cha Life,Maisha yangu 2024

 

08 November 2023, 16:40