Tafuta

Papa Francisko alikuwa anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 huko Dubai, kwa Mwaka 2023, lakini kutokana na changamoto za kiafya, hija hii ya kitume kwa sasa imefutwa Papa Francisko alikuwa anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 huko Dubai, kwa Mwaka 2023, lakini kutokana na changamoto za kiafya, hija hii ya kitume kwa sasa imefutwa  (AFP or licensors)

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Dubai, COP28 Imefutwa

Baba Mtakatifu Francisko, kuanzia tarehe 1 Desemba hadi tarehe 3 Desemba alitarajia kwenda Dubai, Falme za Kiarabu ili kushirikishi katika Mkutano wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 huko Dubai, kwa Mwaka 2023, lakini kutokana na changamoto za kiafya, hija hii ya kitume kwa sasa imefutwa. Utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote, amani na maskini ni kati ya vipaumbele vya maisha na utume wa Papa Francisko kwa sasa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Vita na athari za mabadiliko ya tabianchi ni kati ya mambo yanayohatarisha maisha ya viumbe hai duniani na hasa kwa vizazi vijavyo. Hali hii ni kinyume cha mpango wa Mungu ambaye aliumba kila kitu kwa ajili ya kuenzi Injili ya uhai. Baba Mtakatifu Francisko, kuanzia tarehe 1 Desemba hadi tarehe 3 Desemba alitarajia kwenda Dubai, Falme za Kiarabu ili kushirikishi katika Mkutano wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 huko Dubai, kwa Mwaka 2023, lakini kutokana na changamoto za kiafya, hija hii ya kitume kwa sasa imefutwa. Baba Mtakatifu Francisko ameupokea ushauri wa madaktari kwa moyo wa unyenyekevu na uchungu mkubwa, ingawa afya yake kwa sasa inaendelea kuimarika.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Dubai COP28 imefutwa
Hija ya Kitume ya Papa Francisko Dubai COP28 imefutwa

Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake, ameendelea kutoa kipaumbele cha kwanza kwa amani, maskini sanjari na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote ni kati ya mambo ambayo ameyapatia kipaumbele cha pekee na ndiyo maana alikuwa amekubali mwaliko kutoka Falme za Kiarabu kushiriki katika Mkutano wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 huko Dubai, kwa Mwaka 2023. Kwa sasa Baba Mtakatifu na Vatican katika ujumla wake, wanaangalia namna bora zaidi ya kushiriki katika mkutano huu.

Mkutano wa COP28: 30 Septemba hadi 12 Desemba 2023.
Mkutano wa COP28: 30 Septemba hadi 12 Desemba 2023.

Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa kitume wa “Laudate Deum” yaani “Asifiwe Mungu Kwa Ajili ya Viumbe Vyake Vyote” anachambua kuhusu: Matarajio ya Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, huko Dubai, Falme za Kiarabu kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023. COP28 ilete mabadiliko makubwa katika kipindi hiki cha mpito, mabadiliko ya kudumu kwa kujikita katika matumizi ya nishati ya upepo na jua ili hatimaye, kuachana na matumizi ya nishati ya mafuta. Huu ni uwajibikaji wa pamoja, utakaoirejeshea tena Jumuiya ya Kimataifa uwezo wa kuaminika tena katika maamuzi yake; kwa kujikita katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Papa Dubai COP28
29 November 2023, 15:07