Papa anajibu maswali ya watoto kuwa hatupaswi kujiuzulu amani inawezekana kufikiwa
Vatican News
Papa Francisko anaandika Watoto wapendwa… Papa anajibu maswali yenu. Ni kichwa cha kitabu kilichohaririwa na mwandishi wa Vatican wa Gazeti La Stampa, Domenico Agasso ambaye alikuwa na wazo la kukusanya mfululizo wa maswali kwa Papa Francisko kwa hiyo ni kitabu kilichojaa matumaini ambayo Baba Mtakatifu anasimulia kwa dhati watoto ulinwengu, kwa kujibu maswali yao kuhusu maswali madogo na makubwa ya maisha. Kwa kutazama watoto wake mwenyewe na mahojiano na Baba Mtakatifu mtaalamu wa masuala ya Vatican anaandika maswali na majibu ambayo Papa alijikita kwa upendo wake, kukabiliana na wao kwa ukweli wote wa kibinadamu iwezekanavyo: kama babu, amesimulia wao kumbukizi na uzoefu mdogo wa maisha yake ya utoto, alijibu maswali msingi ambayo kwa kila binadamu hujiuliza kama vile (nini maana ya maisha, vita visivyo na maana, thamani ya ndoto).
Papa Francisko ameeleza jinsi gani maisha ya upapa yalivyo maalum na wakati huohuo ya kawaida. Yote hayo ameyasimulia kwa lugha rahisi sana ya ulimwenguni yenye uwezo wa kueleweka kwa walio wadogo sana. Kwa hiyo Watoto wapendwa… ni kitabu ambacho kinapaswa kusomwa kwa kushirikishana ndani ya familia, katika kitabu kilichojaa ujumbe mwingi wa ambao na ni wa ubinadamu.
Ni kitabu chenye michoro kinachoitwa "Watoto wapendwa... Papa anajibu maswali yako" kilichochapishwa na Mondadori ElectaKids na kitatolewa Jumanne tarehe 17 Oktoba 2023. Gazeti la Torino limehakiki baadhi ya vifungu vyake kama vilivyochapishwa tarehe 14 Oktoba 2023.
Vifungu vya kitabu hicho
Darío, mtoto wa kiume wa miaka kumi wa Hispania, Darío anauliza Papa Francisko: “Kwa nini kuna vita?”. Naye Papa anajibu: “Kwa sababu tunapokuwa watu wazima tuna hatari ya kuanguka katika jaribu la kuwa wabinafsi, na hivyo kutaka mamlaka na pesa. Hata kwa gharama ya vita dhidi ya nchi nyingine ambayo ni kikwazo kwa lengo hili la nguvu, au ambayo ina kiongozi mwenye malengo sawa. Hata kuijua inamaanisha kuua watu wengine. Mara nyingi, katika historia, wale ambao wamekuwa viongozi wa taifa hawajaweza kuzuia tamaa yao ya kuwa na nguvu zaidi ya yote, kuamuru ulimwengu. Hii inaitwa 'imperial interest', utaisoma shuleni katika vitabu vya historia. Leo kwenye sayari kuna vita na vurugu nyingi, na hata kama kuna wale ambao wanasema kwamba wakati mwingine wako sahihi, sina shaka kwamba utaelewa kuwa wao wana makosa daima. Vita daima huwa ni kukosea kila wakati."
Isabela, mwenye umri wa miaka tisa, kutoka Panama, anamwuliza Papa Francisko hivi: “Je, unafikiri siku moja kutakuwa na amani ulimwenguni pote? Inawezaje kufanywa?". Papa anajibu-"Ndiyo, hatupaswi kujiuzulu amani inawezekana, kufikiwa. Nina matumaini kwamba punde au baadaye 'watu wazima' wataelewa kwamba katika ulimwengu wenye amani kabisa kila mtu anaishi vizuri zaidi. Hata hivyo, kila mtu lazima ajitolee kuweka chini silaha zake, ili kutuliza ghasia, na sio kuibua mivutano na mapigano. Na kuondoa kutoka moyoni mwa mtu tamaa ya kutawala wengine, kiu ya kutawala na pesa. Katika mioyo yetu lazima kuwe na upendo kwa wengine tu, yaani, watu walio karibu na walio mbali nasi, hasa wale wanaoteseka au walio katika matatizo kwa sababu fulani. Na hii inapaswa pia kutumika kati ya viongozi wa mataifa ya sayari. Ikiwa sote tungeishi kwa njia hii kungekuwa na uchokozi kidogo na pia hofu ndogo: sote tungekuwa na utulivu na furaha zaidi. Upendo hushinda vita na kukufanya uwe na furaha."
Mary, mwenye umri wa miaka tisa, kutoka Hungaria, anauliza kwa nini Papa mara nyingi anasema kwamba watu wazima wanapaswa kujifunza kutoka kwa watoto. Kwa upande wa Papa Francisko anajibu - "Kwa sababu wana hekima wana moyo safi, hawana ubaguzi. Kwa sababu wanasema uso wao unasema ukweli wao (...) Bila kutambua, wanasaidia watu wazima wanaojua jinsi ya kusikiliza, na hasa wazazi wao, kuishi kwa uaminifu na ukarimu zaidi. Ninyi watoto mnajua jinsi ya kutoa thamani ifaayo kwa nyakati za maisha: zile za masomo, za sala, za kujifurahisha, za kucheza peke yenu, na marafiki na wazazi; na ninatumaini sana kuwa wazazi wanaweza kupata wakati wa kucheza nanyi. Na kisha, wasaidie wakubwa kubaki wanyenyekevu. Kwa sababu kweny ninyi ni mama au baba, au kwa hali yoyote wanawake , watu wazima na waungwana. Na kwa hiyo 'waondoe' wale ambao ni wakorofi sana: kwa sababu kwenu ninyi wale watu wazima sio muhimu kwa nafasi ya kifahari waliyonayo au kwa sababu ni maarufu, bali kwa ajili ya jukumu walilo nalo mbele yenu."
Paul pia ana umri wa miaka tisa, wa Norway, anauliza Papa Francisko kwa nini anapaswa kutunza asili. Papa anaelezea kuwa, "Kwa sababu mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na wanadamu inaweza kusababisha kutoweka kwa ubinadamu. Kupitia matukio kama vile ongezeko la joto duniani, uharibifu wa asili, uharibifu wa mazingira, na kutoweka kwa viumbe hai. Pamoja na magonjwa mapya ya mauti. Lakini nina imani - anasema Papa Francesco - katika ufahamu wa pamoja wa vijana na watoto juu ya maswala ya mazingira: wavulana na wasichana, ambao, mara nyingi shukrani kwa shule, wameelewa kuwa siku zijazo ni zao, na kwa hivyo lazima tuchukue hatua haraka sasa ili kuokoa siku zijazo", hata ikiwa sasa "hatua za kiikolojia za mataifa zilizokubaliwa katika kiwango cha kimataifa ni muhimu, lakini pia tabia ya kila mmoja wetu kila siku:ukusanyaji wa taka kuzitofautisha, umakini na si kupoteza maji na chakula, kusoma vitabu vinavyoeleza undani wa matatizo ya Dunia yetu. Ni lazima sote kwa pamoja tusiwe tena na kazu ya Uumbaji chafu, na kuitunza, daima, tuchague matendo kwa manufaa ya makazi yetu, kwa sababu ni Nyumba yetu ya pamoja na ni jukumu la kibinadamu na pia ya Kikristo."
Kutoka Sudan, Samuel, mwenye umri wa miaka 10, anasema anaishi katika kambi ya wakimbizi miongoni mwa marafiki wenye utapiamlo na kwamba mambo yanapokwenda vizuri "tunakula mlo mmoja kwa siku". Alimweleza Papa kwamba karibu kila mara hutabasamu hata kama wakati mwingine “ghafla najisikia kulia. Kwa sababu ningependa kutoroka kwenda mbali ...". Papa Franciskoo anasema anaielewa. Kwa kumfariji anasema "Watoto wote wanapaswa kuwa na uwezo wa kwenda shule na kupata nafasi za kucheza na kujiburudisha." Anaongeza kuwa inaonekana ni jambo la kawaida kuamini kwamba Afrika "inapaswa kunyonywa tu na sio kusaidiwa". Lakini tafadhali,"msipoteze matumaini katika maisha bora yajayo. Ninaamini kwamba mapema au baadaye nchi tajiri zitaelewa kuwa haziwezi kuendelea kutumia na kuacha ardhi yenu, zitawekeza rasilimali kusaidia kutatua matatizo yenu makubwa na kuanzisha mabadiliko ya kijamii ambayo yanaruhusu kila mtu maisha ya heshima na uwezekano wa kuota wakati wa mafanikio sio mbali sana."
Alessandro, kutoka Italia, pia ana umri wa miaka kumi na anamuuliza Papa maoni yake kuhusu ukweli kwamba watu wazima anaowasikia hawataki "familia kutoka maeneo maskini" kufika nchini mwao. Na kwamba kama ingekuwa hivyo, hangekuwa “rafiki wa Momo.” Papa Francisko anakiri kwamba cha muhimu ni thamani ya “urafiki wa kijamii”: ni lazima kila mara,“tujifikirie sisi sote kaka na dada, bila kutoaminiana juu ya nchi ya asili, dini au tamaduni tofauti. Wewe ni na ni mfano kwa wale ambao wana chuki juu ya wale wanaotoka mbali, kuhusu 'wageni'.
Hakuna mtu anayepaswa kujisikia kama mgeni mahali popote tena. Na ninyi watoto ni wazuri sana katika kukaribisha marafiki wapya. Unaweza kuunganisha utambulisho wako- kwa kucheza, mazungumzo na utambulisho wa wale wanaofika kutoka nchi za mbali, mara nyingi kwa sababu wamelazimika kukimbia vita, vurugu, ukosefu wa haki, umaskini, njaa, mateso. Ninyi watoto mnatuma ujumbe muhimu sana: kujitenga ni kosa na hakuna tija. Na ujuzi wa kuheshimiana hujenga manufaa kwa pande zote mbili. Kuanza na urafiki mpya. Hata katika eneo hili, watu wazima, ikiwa ni pamoja na viongozi wa mataifa, wanapaswa kujifunza kutoka kwako: kulinda mizizi yao na wakati huo huo kufungua ulimwengu".