Papa:Mama yetu wa Aparecida alinde watu wote wa Brazil
Angella Rwezaula, - Vatican.
"Ni sikukuu ya Mama yetu wa Aparecida. Nimembeba moyoni. Nakumbuka mji huu na Bikira. Atubariki sana, awatazame ninyi na watu wote wa Brazil. Ninawaombea, ninatuma baraka yangu na tafadhali mniombee! Asante." Ni katika siku ya Sikukuu ya Bikira Mlinzi wa Brazil, ambapo Baba Mtakatifu Fransisko ametaka kueleza kutoka katika Sinodi upendo wake kwa Nchi ya Brazili na Wabrazili wenyewe. Kwa upande wa Papa Francisko alikumbuka hasa ziara yake ya Aparecida miaka 10 iliyopita, ya mnamo tarehe 24 Julai 2013, wakati wa ushiriki wake katika Siku ya Vijana Duniani, WYD, huko Rio de Janeiro na alitaka kupitia mara moja kutembelea mahali patakatifu pa Maria huyo huyo wa Aparecida.
Misa katika madhabahu ya Mama yetu mnamo mwaka 2013
Katika tukio hilo, Papa Fransisko aliadhimisha Misa na katika mahubiri yake alikumbuka Mkutano Mkuu wa tano wa Maaskofu wa Amerika ya Kusini na Karibiani wa mnamo Mei 2007. "Mkutano huo alisema ulikuwa wakati mzuri wa Kanisa. Ambao ungeweza kusemwa kwamba Hati ya Aparecida ilizaliwa kwa usahihi kutokana na msuko huu kati ya kazi ya Wachungaji na imani sahili ya mahujaji, chini ya ulinzi wa kimama wa Maria. Kanisa, linapomtafuta Kristo, daima hubisha hodi kwenye nyumba ya Mama na anawalekeza kwamba : 'Mwelekee Yesu'. Ni kutoka kwake kwamba uanafunzi wa kweli unaanzia hapo na kujifunza. Na hii ndiyo sababu Kanisa daima linaendelea na utume katika nyayo za Maria
Katika bustani ya Vatican
Katika miaka hii 10 ya upapa, kumekuwa na mrejesho mwingi kuhusu Msimamizi wa Brazil. Ilikuwa mnamo tarehe 3 Septemba 2016, ambapo Papa Francisko alizindua Sanamu ya Picha ya Mama Yetu wa Aparecida katika Bustani ya Vatican na kuwaalika waamini kuwaombea “maskini zaidi, waliotupwa, wazee waliotelekezwa, watoto wa mitaani; waliotupwa na kuwekwa mikononi mwa wanyonyaji wa kila aina; ili awaokoe watu wake kwa haki ya kijamii na kwa upendo wa Yesu Kristo, Mwanae”. "Uwaombee kwa upendo, wa watu wote wa Brazili - kwamba wewe ni Mama na ubariki, ili wafanyakazi maskini, wapate leo hi ina kila mt una kwa wale wanaohitaji kazi, elimu na wale ambao hawana hadhi."