Papa kwa Wascalabrini-Uhamiaji ni janga leo hii tunahitaji kutoa ukaribu na huduma
Na Angella Rwezaula, Vatican
Baba Mtakatifu Francisko alikutana mjini Vatican, Jumamosi tarehe 14 Oktoba 2023, wanaume na wanawake wa Shirika lililoanzishwa na Mtakatifu Yohane Mbatizaji Scalabrini aliyekuwa Askofu wa Piacenza Nchini Italia na aliyeishi kati ya karne ya 19 na 20, ambaye aliwafundisha watawa wa mashirika hayo mawili kuwatunza wale waliokuwa wakioondoka kutoka nchi yao ili kutafuta maisha bora ya baadaye, wawaone kama kaka dada katika njia ya kuelekea umoja. Kwa hiyo Baba Mtakatifu katika hotuba hiyo amewasalimia huku akifurahi kukutana nao mara baada ya mkutano wao wa tasaufi ya Wascalabrini. Wao walitafakari juu ya kifungi cha Biblia: "Nitakuja kuwakusanya watu wote" kutoka (Isa 66:18), ambayo ni mada muhimu sana kwa karama yao.
Kiukweli, Papaamesema Mtakatifu Yohane Mbatizaji Scalabrini, aliyeanzisha wao kama wamisionari kwa ajili ya wahamiaji, aliwafundisha, katika kuwatunza, kujiona kama kaka na dada katika safari ya kuelekea umoja, kulingana na maneno ya dhati ya sala ya kikuhani ya Yesu ( taz. Yoh 17:20-23). Kwa hiyo Papa ameomba kuwa wazi kuwa: kuhama si kutangatanga katika ushirika; mara nyingi ni janga. Na, kama vile kila mtu alivyo na haki ya kuhama, hata zaidi wana haki ya kubaki katika ardhi yao wenyewe na kuishi huko kwa njia ya amani na ya heshima. Hata hivyo, janga la uhamiaji unaosababishwa na vita, njaa, umaskini na matatizo ya mazingira ni wazi kwa wote kuyaona leo hii. Na hapa ndipo hasa hali yao ya kiroho au tasaufi inapohusika kujiuliza je: wanawezaje kuelekeza moyo wao kwa kaka na dada hawa? Kwa njia ya msaada gani wa kiroho?
Scalabrini Papa amesema anatusaidia, hasa kwa kuwatazama wamisionari wahamiaji kama washiriki wa Roho Mtakatifu katika umoja. Maono yake yenye nuru na asilia ya jambo la uhamaji, linaloonekana kama mwito wa kuunda ushirika katika upendo. Bado akiwa paroko kijana, yeye mwenyewe alisema kuwa alijikuta, katika Kituo Kikuu cha Milano, mbele ya umati wa wahamiaji wa Italia waliokuwa wanakwenda Amerika. Alisema kuwa aliona "watu mia tatu au nne waliovaa vibaya, wamegawanywa katika vikundi tofauti. Wenye nyuso [...] zilizokunjamana na makunyanzi ya mapema ambayo yalikuwa kwa hiyo hayavuti, msukosuko wa upendo ambao uliisumbua mioyo yao wakati huo ungeweza kuonekana. [...] Walikuwa wahamiaji [...] Walikuwa wakijiandaa kuacha nchi yao" yaani (uhamiaji wa Italia kwenda Amerika, 1888).
Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa huu kwa bahati mbaya, ndizo picha za kawaida kwetu pia. Na Mtakatifu huyo, alivutiwa na taabu hiyo kubwa, na alielewa kwamba kulikuwa na ishara kutoka kwa Mungu kwa ajili yake, ambayo ilikuwa ni wito wa kuwasaidia watu hao kwa mali na kiroho, ili kwamba pasiwepo hata mmoja wao, aliyeachwa peke yake, apotee, na has hasipoteze imani yake. Na ili waweze kuufikia, kama nabii Isaya asemavyo, mlima mtakatifu wa Yerusalemu “kutoka kwa mataifa yote kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na juu ya magari, na juu ya viti vya wanyama wote, na juu ya nyumbu, na juu ya ngamia” (66,20). .. Farasi, mikokoteni, viti vya,nyumbu ambavyo tunaweza leo hii kuongeza kuwa ni majahazi, lori na mikokoteni ya baharini; lakini marudio yanabaki pale pale, Yerusalemu, mji wa amani (rej Zab 122:3-9), Kanisa, nyumba ya watu wote (rej Isa 56:7), ambapo maisha ya kila mtu ni matakatifu na ya thamani. Ndiyo, kwa Upande wa Mtakatifu Scalabrini, Yerusalemu hii ni Kanisa Katoliki, yaani, la ulimwengu wote, na vile vile kwa sababu ni "mama", kwa sababu ni jiji lililo wazi kwa mtu yeyote anayetafuta nyumba na kimbilio salama.
Na hapo kuna ombi la kwanza kwetu, Papa Francisko amehimiza kwamba ni la kuhamasisha mioyo iliyojaa ukatoliki, ambayo ni ile inayotamani ulimwengu wote na umoja, kukutana na ushirika. Kwa hiyo ni mwaliko wa kueneza mawazo ya ukaribu na "ukaribu" ni neno muhimu... ni mtindo wa Mungu, ambaye daima huwa karibu, ni hali ya kiroho, mawazo ya kujali na kukaribishwa, na kusaidia kukua katika ulimwengu, kwa maneno ya Mtakatifu Paulo VI, alisema ni "ustaarabu wa upendo" (Mahubiri kwa ibada kuu ya kufunga Mwaka Mtakatifu, 25 Desemba 1975). Hata hivyo, itakuwa ni jambo ambalo si la busara kujifanya kuwa haya yote yanaweza kupatikana kwa nguvu za binadamu pekee. Badala yake, ni suala la kushirikiana katika utendaji wa Roho, na kwa hiyo kutenda katika historia chini ya uongozi na nguvu zinazotoka kwa Mungu tu ambao ni kujiruhusu sisi wenyewe tuongozwe na huruma yake isiyo na kikomo ya kuhisi na kutenda kulingana na yeye na hivyo ni njia, ambazo si zetu sikuzote (taz. Isa 55:8), kumtambua katika wale ambao ni wageni (rej. Mt 25:35) na kupata ndani yake nguvu za kupenda kwa uhuru huyo mgeni.
Baba Mtakatifu Francisko amekazia kusema kwamba Tusisahau maneno haya matatu kutoka katika Agano la Kale: mjane, yatima, na mgeni. Na hili ni jambo muhimu katika Agano la Kale kuhusu mgeni. Na hapa kuna ombi la pili ambalo Askofu Mtakatifu wa Piacenza anatuelekeza, anaposisitiza haja ya mmisionari kuwa na uhusiano wa upendo na Yesu, Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili, na kuukuza hasa kwa njia ya Ekaristi, inayoadhimishwa na kuadhimishwa. kuabudiwa. Hapa Papa Francisko amependa kukazia neno la “kuabudu”. Na hii amebainisha kuwa anafikiri tumepoteza hisia ya kuabudu. Na tuna maombi ya kufanya jambo fulani au... maombi mazuri, lakini… katika ukimya, na ibada. Mawazo ya kisasa yameondoa hisia hii ya kuabudu kutoka kwetu kidogo. Kwa hiyo ameomba kwamba - Irudisheni, tafadhali, irudisheni.
Tunajua ni kiasi gani Scalabrini alipenda Kuabudu, na ambaye alijitolea hata usiku, licha ya uchovu wa ratiba yake ya kazi yenye uchovu, na ambayo hakukata tamaa wakati wa mchana, hata wakati wa shughuli kubwa zaidi. Hakujidanganya na akatualika tusijidanganye: kwa sababu bila maombi hakuna utume! Alisema: “[Msipotoshwe] na tamaa fulani ya ukichaa isiyozuiliwa ya kuwasaidia wengine, mkijisahau […]. Ni sawa kwamba unafanya kila kitu kwa kila mtu; lakini [...] kumbuka Malaika waliopaa kwa Mungu na kushuka duniani kwenye Ngazi ya Yakobo [...]. Hakika ninyi pia ni Malaika wa Bwana." Kupaa kwa Mungu ni muhimu ili basi namna kujua jinsi ya kushuka duniani, kuwa "malaika kutoka chini", ni karibu na kuwa na mdogo kabis. Hiyo sio bahati kwamba ngazi ya Yakobo (rej. Mwa 28:10-22) imewekwa moja kwa moja ndani ya katikati ya nembo ya kiaskofu ya Scalabrini.
Kwa hiyo, Papa Francisko amebainisha kwamba , huo ni mwaliko wa kufanya upya ahadi yao kwa wahamiaji, na kuitia mizizi zaidi katika maisha ya kiroho yenye bidii, kwa kufuata mfano wa Mwanzilishi wao. Pamoja na hilo, hata hivyo, alitaka kusema asante kubwa, asante kubwa kwa kazi nyingi wanayofanya ulimwenguni kote! Tangu siku za Buenos Aires Papa ameshuhudia kazi hiyo, na wao wanaifanya vizuri sana. Jwa njia hiyo amesahuruku sana na kuwaomba wasonge mbele na Mungu awabariki. Kama kawaida yake pia amewaomba wasali kwa ajili yake na kwamba ni kazi hiyo ambayo siyo rahisi. Kabla ya kuhitimisha wamesali pamoja sala ya Salamu Maria.