Tafuta

Papa Francisko:Sura ya mtu ina chapa ya Mungu hakuna anayeweza kuifuta

Wazalendo wenye uwajibikaji wanaochangia jamii,wakijitolea kwa manufaa ya wote,lakini wakijua kwamba kila kitu ni cha Bwana:Haya ni maisha ya Wakristo.Papa amekumbusha katika tafakari Dominika tarehe 22 Oktoba 2023,katika maneno ya Yesu:“Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu”.Maneno hayo lazima yaeleweke kwa usahihi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Dominika ya 29 ya Mwaka A wa Kanisa, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu  Petro mjini Vatican tarehe 22 Oktoba 2023. Akianza tafakari hiyo Papa Francisko amesema: “ Katika Injili ya Liturujia  ya  leo inasimulia kuwa baadhi ya mafarisayo walivyokwenda wakafanya shauri  pamoja na Maherodi jinsi ya kumtega Yesu kwa maneno. Na walikwenda kwake wakamuuliza, je ni halali kumpatia Kaisari kodi ama sivyo? (Mt 22,17) Ni ulaghai: Ikiwa yuko halali kulipa kodi, anaweka pembeni uwezo wa kisiasa, ambao ulikuwa hauvumiliki kwa watu, wakati ikiwa anatesema hawezi kulipa inawezekana kushitakiwa kuwa amekuwa mgumu dhidi ya Mamlaka. Lakini yeye alikwepa ulaghai huo. Aliwaomba wamuonesha sarafu ya kodi, ambayo ilikuwa na chapa ya picha ya Kaisari na kusema “Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakajibu  ya Kaisari, naye akawambia, Basi mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu”(Mt 22, 21).

Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana mvua kubwa ilinyesha
Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana mvua kubwa ilinyesha

Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema je ina maana Akiendelea na tafakari hiyo amesema maneno haya ya Yesu yamegeuka kuwa matumizi ya kawaida, lakini wakati mwingine yametumiwa vibaya, au hata kuyapunguza kwa namna ya kuzungumzia uhusiano kati ya Kanisa na Serikali, kati ya wakristo na Siasa; mara nyingi yamekuja kueleweka kama kwamba Yesu anataka kutengenisha  kati ya ‘Kaisari’ na ‘Mungu’ yaani ukweli wa kidunia na ule wa kiroho. Na wakati mwingine hata sisi tunaweza kufikiria hivyo: kwamba jambo hilo ni la imani na mazoezi yake na jambo jingine la  maisha ya kila siku. Lakini siyo hivyo. Hii ni tabia ya kuganda, utafikiri imani haina lolote katika maisha ya dhati, na changamoto za kijamii na haki kijamii na sera za kisiasa na mengine.

Umati wa mahujaji na waamini hawakukosa katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Umati wa mahujaji na waamini hawakukosa katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa kiukweli, Yesu anataka kutufundisha kutambua “Kaisari” na “Mungu”  katika kila mmoja umuhimu wake. Kwa Kaisari ikiwa na maana katika sera za kisiasa, za kitaasisi za kiraia, katika michakato ya kijamii na kisheria, ambayo inaendeshwa na sheria za kidunia, ujumla masuala ya siasa; na sisi katika hali halisi hiyo tumo ndani, ambapo tunapaswa kurudisha katika jamii kile ambacho tunapewa kwa njia ya mchango wetu wa uwajibikaji kizalendo, kwa kuwa na umakini kwa kile ambacho tunakabidhiwa, kama vile kuhamasisha sheria na haki katika ulimwengu wa kazi, kwa kulipa kodi kwa uaminifu, na  kujikita kwa ajili ya wema wa kawaida  wa pamoja.

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana

Na kwa wakati huo huo lakini, Yesu anathibitisha uhalisia msingi kuwa  Mungu anapatikana kwa  binadamu, ‘kwa mtu na kila mwanadamu’. Hii ina maana kuwa sisi hatupo katika hali halisi ya kidunia, kwa yeyote katika ‘Kaisari.’ Kwa sababu Sisi ni wa Bwana na hatupaswi kuwa watumwa kwa yeyote yule katika mamlaka ya kidunia. Kuhusu sarafu kwa njia hiyo kuna picha  ya mfalme, lakini Yesu anatukumbusha kuwa katika maisha yetu, yametiwa chapa ya muhuri na sura ya Mungu, na ambayo hakuna chochote na hakuna mtu anayeweza kuificha. Kwa Kaisari kuna mambo ambayo yanahusu dunia hii, lakini kwa mtu na dunia hii yenyewe ni vya Mungu. Na hivyo “Tusisahau hili,” Papa amekazia.

Kikundi cha Udugu wa Bwana wa Miujiza cha Wanajumuiya Waperu, Roma
Kikundi cha Udugu wa Bwana wa Miujiza cha Wanajumuiya Waperu, Roma

Kwa hiyo, ndiyo maana tunaweza kuelewa kwamba Yesu yupo  na anarudisha kwa kila mmoja wetu  katika utambulisho wake binafsi: juu ya safari ya dunia hii kuna picha ya Kaisari, lakini je  wewe unabeba sura gani ndani mwako? Maisha yako ni ya picha gani? Je tuakumbuka kuwa yanahusiana na Bwana au tunajiachia kupakwa na mantiki za ulimwengu  na kufanya kazi, katika siasa, katika fedha za kuabudu miungu yetu? Bikira Mtakatifu atusaidie kujitambua na kuheshimu hadhi yetu na ile ya kila binadamu.

Tafakari ya Papa wakati wa Angelus 22 Oktoba 2023
22 October 2023, 13:22