Tafuta

Kimbunga cha namna hii, hakijawahi kutokea nchini Mexico, isipokuwa kile kilichotokea mwaka 2015 mjini Patricia, kwenye Bahari ya Pacific. Kimbunga cha namna hii, hakijawahi kutokea nchini Mexico, isipokuwa kile kilichotokea mwaka 2015 mjini Patricia, kwenye Bahari ya Pacific.  

Papa Francisko Aonesha Mshikamano na Waathirika wa Kimbunga Cha Otis Nchini Mexico

Kimbunga hiki kimesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao kiasi kwamba makazi ya watu yamebomolewa kutokana na mafuriko makubwa na hivyo kuharibu kabisa mawasiliano. Kimbunga cha namna hii, hakijawahi kutokea nchini Mexico, isipokuwa kile kilichotokea mwaka 2015 mjini Patricia, kwenye Bahari ya Pacific. Papa Francisko ameonesha mshikamano wake kwa njia ya sala kwa waathirika wote wa kimbunga hiki ambacho kileta maafa makubwa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Zaidi ya watu 43 wamepoteza maisha na wengine 36 hawajulikani mahali walipo kutokana na uharibifu mkubwa uliosababishwa na kimbunga cha Otis kilichoandamana na dhoruba kali kupiga mji wa kitalii wa Acapulco nchini Mexico, tarehe 25 Oktoba 2023. Kimbunga hiki kimesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao kiasi kwamba makazi ya watu yamebomolewa kutokana na mafuriko makubwa na hivyo kuharibu kabisa mawasiliano.

Watu 43 wamefariki dunia na wengine 36 hawajulikani waliko
Watu 43 wamefariki dunia na wengine 36 hawajulikani waliko

Kimbunga cha namna hii, hakijawahi kutokea nchini Mexico, isipokuwa kile kilichotokea mwaka 2015 mjini Patricia, kwenye Bahari ya Pacific. Ni katika muktadha wa maafa haya makubwa, Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 29 Oktoba 2023 ameonesha uwepo wake wa karibu kwa watu waliokumbwa na maafa haya. Amemwomba Bikira Maria wa Guadalupe kuwa karibu na kuwatia shime watoto wake wanaokabiliwa na majaribu makubwa katika historia ya maisha yao.

Maafa Mexico
31 October 2023, 14:15