Tafuta

2023.10.04 Kifuniko cha Ujumbe wa Papa Francisko wa Laudate Deum. 2023.10.04 Kifuniko cha Ujumbe wa Papa Francisko wa Laudate Deum.  Tahariri

Pande nyingi kuanzia chini ili kuthibiti maadiliko ya tabia nchi

Katika tahariri ya Mwariri wetu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican,Dk. Andrea Tornielli kuhusu Hati mpya ya Papa anabainisha kuwa katika Waraka mpya wa Papa Francisko anaelekeza umuhimu kwa mamlaka duniani wa kuwa na uwezo wa kuheshimu jitihada na ulazima wa ushiriki kwa wote.

Andrea Tornielli

Pamoja na Waraka wa Laudate Deum Papa Francisko hakuelezea tu kwa kina na kutimiza ujumbe wa Waraka wa Laudato Si uliochapishwa miaka 8 iliyopita. Na Hati hii yenye utajiri mkubwa wa takwimu na idadi ya maandishi mengi yaliyochukuliwa kutoka katika fasihi ya hivi karibuni ya kisayansi ambayo haipo nje ya hofu zaidi kuhusu matokeo yanayoongezeka kila mara na daima yanazaidi kuwa mabaya ya mabadiliko ya tabianchi, kwa matumaini kuwa COP28  ya Dubai inaweza hatimaye kubadilisha mwenendo kabla haijachelewa. Laudate Deum ina mengi zaidi na katika sehemu ya kwanza inajikita na udhaifu wa kisiasa kimataifa na kuweka kidole katika donda la wakati wetu ule wa udhaifu wa  kitaasisi na mashirika makuu ya kimataifa katika kuwa na  uwezo wa kuheshimu jitihada zilizochukuliwa na  kutatua migogoro.

Ni maelekezo ambayo Mfuasi wa Petro anabainisha katika muktadha wa mgogoro wa tabianchi na ulinzi wa kupunguza hewa chafuzi kwa njia ya Uongofu wa kweli wa kiikolojia, lakini kwa kutazama wakati wetu ujao  na sio tu katika uhusiano na ulinzi wa kazi ya uumbaji. Ni mambo ambayo yanawezekana katika mantiki nyingine, kwani inatosha kufikiria vita, tuseme vita vingi ambavyo kwa wakati huu, vinaendelea kupigana, katika ulimwengu, vimekusuka kama onesho la umbo ambalo Papa Francisko mara kadhaa amelielezea kuwa vita ya Tatu ya Dunia vilivyomegeka vipande vipande

Kwa hiyo mtazamo ambao Papa anapendekeza ni ule wa  kuongeza zaidi Ushirikiano na mahsikamo wa pande nyingi na kusisitiza juu ya haja ya kupendelea mikataba ya kimataifa kati ya mataifa na uwezekano wa kuwa na mtindo fulani wa mamlaka ya kidunia wenye kuwa na kanuni ya kisheria yaani wa mashirika ya kimataifa yenye muafaka zaidi, kuwa na mamlaka ya kuhakikisha manufaa ya wote duniani, kutokomeza njaa na umaskini na utetezi fulani wa haki msingi za binadamu. Mashirika yenye uwezo wa kuhakikisha utimizaji wa baadhi ya malengo yasiyoweza kuachwa kamwe.

Kama ilivyo katika vita vinavyoendelea nchini Ukraine, Matarajio ya Baba Mtakatifu ni uwezo wa Roho ya Helsinki, ambao kama ulivyokuwa na dhamiri ya Mkutano  kuhusu usalama na ushirikiano katika Bara la Ulaya wa 1975 na kwa njia hiyo hata leo hii ingekuwa ni vema kurudia mshikamano  na hivyo katika mapendekezo ya mgogoro wa mazingira Papa anaandika  kuwa zaidi ya kuokoa ushirikiano wa pande nyingi za zamani, utafikiri kwamba leo hii changamoto ni ile  ya kuundwa kwa upya katika nuru ya jamii ya kiraia ili kutimiza  kwa kufikiria udhaifu wa Jumuiya ya Kimataifa. Kuna  maana kwa mtazamo huo ambao Papa anataja mchakato wa Ottawa dhidi ya uzalishaji na mtumimizi ya mabomu ya kulipuka, mfano ambao unajionesha kama jamii ya raia na mashirika yake ambayo yanakuwa na uwezo wa kuunda mwendelezo muafaka ambao Umoja wa Mataifa hauwezi kufikia.

Katika Waraka wa Kitume wa Askofu wa Roma anapendekeza kuwa na pande nyingi kama njia hisiyozuilika, yaani pande nyingi kuanzia chini na sio maamuzi rahisi tu kutoka kwa wasomo wa madaraka.  Kwa kutambua umuhimu wa nguvu mpya zilizojitokeza ambazo daima  ziko zinageuka kuwa za juu zaidi. Ili kuweza kutimiza hili la kuwa pande nyingi mpya, inahitajika mchakato mpya wa maamuzi, inahitajika nafasi za uongofu, mashauriano, usuluhishi, utatuzi wa migogoro, usimamizi, kwa kifupi aina fulani ya udemokrasia katika mzunguko wa sayari ili kuelezea na kuunganisha hali tofauti.

Papa Francisko anahitimisha akisema kuwa kwa sababu haitakuwa na maana tena kusaidia taasisi ambayo inahifadhi haki za walio na nguvu zaidi bila kushughulika haki za wote.  Iwe ni kukabiliana na mgogoro wa tabianchi na uhamiaji, na iwe ni kuzungumzia migogoro ambayo inasababisha Sayari kumwaga damu au ambayo inashughulika hatimaye kashfa ya njaa na kiu ya ulimwengu na mapendekezo ya kubadili k mfumo wa sasa wa uchumi wa kifedha ambao uzalishe usawa. Yote hayo ni matukio yanayosukana kama alivyokuwa tayari ameonesha katika Waraka Laudato si’.

04 October 2023, 12:00