Tafuta

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kwamba, ajali za barabarani zinasababisha vifo vingi vya watoto na vijana sehemu mbalimbaliza dunia Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kwamba, ajali za barabarani zinasababisha vifo vingi vya watoto na vijana sehemu mbalimbaliza dunia  (ANSA)

Ajali Barabarani Ni Chanzo cha Vifo Vingi na Ulemavu wa Kudumu

Baba Mtakatifu Francisko ameonesha masikitiko yake makubwa kutokana na ajali ya Bus la abiria lililopinduka darajani huko Mestre, mjini Venezia tarehe 5 Oktoba 2023 na kupelekea watu 21 kupoteza maisha na wengine 15 kujeruhiwa vibaya. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuonesha mshikamano na uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake kwa wale wote waliofikwa, kuguswa na kutikiswa na ajali hii mbaya. Ajali ni chanzo kikuu cha vifo duniani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kwamba, ajali za barabarani zinasababisha vifo vingi vya watoto na vijana sehemu mbalimbaliza dunia. Ajali za barabarani zimekuwa ni chanzo cha maumivu na majonzi kwa jamii, vifo, upotevu wa mali, vyombo vya moto na ulemavu wa kudumu. Ajali zinaua na kupoteza nguvu kazi nyingi ikiwemo wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi wakati mwingine hata wanafunzi wa taaluma na makundi mbalimbali.

Watu 21 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa vibaya huko Mestre, Italia
Watu 21 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa vibaya huko Mestre, Italia

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko katika salam za rambirambi zilizoandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin Katibu mkuu wa vatican, kwenda kwa Patriaki Francesco Moraglia wa Jimbo kuu la Venezia, ameonesha masikitiko yake makubwa kutokana na ajali ya Bus la abiria lililopinduka darajani huko Mestre, mjini Venezia tarehe 5 Oktoba 2023 na kupelekea watu 21 kupoteza maisha na wengine 15 kujeruhiwa vibaya. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuonesha mshikamano na uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake kwa wale wote waliofikwa, kuguswa na kutikiswa na ajali hii mbaya. Baba Mtakatifu anawaombea marehemu wote ili wapate pumziko na maisha ya uzima wa milele. Kwa majeruhi waweze kupona haraka na kurejea katika shughuli zao za kila siku.

Ajali Venezia

 

06 October 2023, 15:00