Tafuta

Umaskini ni mwingi hata wasio kuwa na mahali pa kulala. Umaskini ni mwingi hata wasio kuwa na mahali pa kulala. 

Wito wa Papa:Dharura ya uchumi katika changamoto ya umaskini na tabianchi!

Katika Ujumbe wa Papa Francisko kwa wawakilishi wa Uchumi na biashara,taasisi na vyama waliokusanyika huko Firenze nchini Italia katika toleo la tano la Tamasha la Kitaifa la Uchumi wa Kiraia amewaalika kwamba:“Tazameni ulimwengu kupitia macho ya waliokataliwa.Fanyeni kazi nao na kwa ajili yao.”Kuna ukosefu wa usawa.

Vatican News

Leo hii kuna dharura ya kuwa na  uchumi mpya na wenye nuru ili kukabiliana na mabadiliko ya zama na changamoto za kutisha tunazokabiliana nazo, kuanzia umaskini na mazingira. Ndivyo amebainisha  Papa Francisko katika ujumbe uliotumwa kwa washiriki wa Tamasha la V la  Kitaifa  la Uchumi wa Kiraia, waliokusanyika huko Firenze nchini Italia katika siku za hivi karibuni. Kwa wananchi, wanachama wa vyama, maprofesa, wawakilishi wa taasisi na wahusika wakuu wa matendo mema ya ujasiriamali na ushirika, Baba Mtakatifu amewaonesha matatizo mawili ambayo hasa yanaashiria dunia ya sasa kwamba: “Hilo la umaskini, yaani, ukosefu wa usawa katika mtindo wa kiuchumi unaozalisha takataka na kutupwa na dharura ya hali ya tabianchi ambayo inaweka mustakabali wetu kwenye sayari hatarini.

Vitendo zaidi kuliko maneno

"Maono ya kina, yaliyochochewa na ikolojia fungamani, yanatufanya tuelewe kwamba katika mzizi wa machafuko haya ambayo hudhoofisha kuishi pamoja katika hali zote kuna shida ya umaskini wa maana ya maisha," anaandika Papa Francisko. Aidha anabainisha kuwa "Kumbuka kwamba uchumi wa raia una zana nyingi za kushughulikia shida hizi, ili kuziweka kwa njia sahihi na kutoa njia za kujibu. Lakini ili hili lizidi kuwa la kawaida na la ufanisi ni lazima tushinde upunguzaji  maneno  matupu bali kuwa na vitendo."

Lazima tukue katika uchumi usio tazama faida tu

Papa Francisko kwa kuzama katika anthropolojia ambapo mtu ana uwezo wa kutoa na aina hiyo bora ya busara ambayo ni akili ya kijamii, inayoundwa na uaminifu na ushirikiano, alisema tutaweza kufikia aina nyingi za biashara na kuona idadi ya wajasiriamali hao wanakua wenye shauku zaidi, ambayo haiangalii faida tu, bali pia athari za kijamii na mazingira. Huu ndio uchumi uliotiwa nuru  ambao unahitajika leo hii. Inahitaji maelekezo mapana, ambayo yanasaidia jamii yetu kufuata njia ya maisha bora na uzalishaji, na ya sera, ikiwa ni pamoja na kiuchumi, iliyoboreshwa na ushiriki, uraia hai na uchaguzi wa uwajibikaji wa raia, kwa mantiki ambayo ni msingi wa demokrasia.

Mwaliko wa Baba Mtakatifu  ni ule wa kukuza nadharia katika mwelekeo wa vitendo,  lakini pia na zaidi ya yote kufanya utume wao wa kuwaunganisha watu wote wenye mapenzi mema. Wanapaswa kujua jinsi ya kutazama uchumi na dunia kwa macho ya maskini zaidi  wa waliotengwa na  waliotupwa. Wafanye kazi nao na kwa ajili yao. Papa amewaomba wajitume kwa ujasiri na shauku  na ndilo tumaini la mwisho  ambalo zaidi ya yote waungane, kufanya kile kinachounganisha kutawala tofauti nyingi ambazo wakati mwingine kwa nia nzuri zaidi hudhoofisha nguvu ya wema.

Ujumbe wa Papa
30 September 2023, 18:13