Tafuta

Papa:ukimya ni muhimu katika maisha ya mwamini,Kanisa na umoja wa kikristo

Ukimya ni muhimu katika:maisha ya mwamini,katika maisha ya Kanisa na Ukimya ni muhimu katika safari ya umoja wa Kikristo:Ndiyo vipengele vitatu ambavyo Papa amefafanua katika tafakari ya sala ya Kiekumeni ya kuombea Sinod ya XVI ya Maaskofu tarehe 30 Septemba katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika tafakari ya  mkesha  wa Kiekumeni,  Jioni tarehe 30 Septemba 2023, ambapo Uwanja ulionesha Vipande vipande vya asili vingi ili kuamsha bioanuwai ya mazingira na ikolojia na  ukijani kupamba Uwanja wa Mtakatifu Petro ulojionesha katika tukio la “Together yaani Pamoja - Kukusanyika kwa Watu wa Mungu”, katika mkesha wa maombi ya Kiekumeni kuombea Mkutano wa  XVI wa kawaida wa Sinodi ya Maaskofu. Mkesha huo ulianza mapema kwa shuhuda na nyimbo na baadaye kufuta tafakari ya papa baada ya kufika na kuwaslimia washiriki wa tukio hilo. Baba Mtakatifu Francisko katika  kukumbusha kauli mbiu iliyoongoza mkesha huo isemayo: “Together, yaani Pamoja. Kama Jumuiya ya Kikristo tangu asili yake ya siku ya Pentekoste alisema ni kama zizi moja, pendwa na lililokusanyika kwa Mchungaji mmoja Yesu. Kama umati mkubwa wa siku ya mwisho, tupo sisi kaka na dada wa taifa moja , kabila moja, watu na lugha(Uf 7,9) kutoka katika Jumuiya na nchi tofauti , wana na binti wa Baba mmoja anayeongozwa na Roho ambayo waliipokea katika ubatizo, wameitwa katika tumaini moja (Ef 4,4-5).

Viongozi wa Kiekumeni katika Mkesha wa Kuombea Sinodi 30 Septemba 2023
Viongozi wa Kiekumeni katika Mkesha wa Kuombea Sinodi 30 Septemba 2023

Baba Mtakatifu amewapongeza kwa matumaini yao. Amemshukuru mwanzilishi wa wazo hilo na Jumuiya yake ya Taizé. Amewasalimia kwa upendo wakuu wa Makanisa, viongozi na wawakilishi wa tamaduni nyingine za kikristo na wote hasa vijana. Shukrani kwa kufika kwao kusali pamoja na Papa jijini Roma, kabla ya Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, katika kesha la mafungo ya kiroho yaliyokuwa yanafuata. Papa Francisko amesema Syn-odos”: kutembea pamoja na sio kwa wakatoliki tu, lakini wakristo wote, watu wote waliobatizwa, watu wote wa Mungu, kwa sababu,ni kwa pamoja tu inawezekana kuwa na umoja wa wote. Kama inavyoonesha umati katika katika kitabu cha Ufunuo, Papa Francisko alibanisha jinsi ambavyo walisali pamoja kwa kimya, wasilikiliza kwa ukimya mkubwa (Uf 8,1). Na ukimya ni muhimu, ni wa nguvu, unaweza kujieleza uchungu usioelezeka mbele ya mikasa, lakini hata katika wakati wa furaha, na wa shangwe inayoleta maneno. Kwa njia hiyo Papa Francisko amependa kutafakari pamoja nao kuhusu umuhimu wa maisha ya waamini, maisha ya Kanisa na maisha ya umoja wa wakristo.

Papa alisema Kwanza kabisa, ukimya ni muhimu, katika maisha ya mwamini. Hiki ni chanzo na mwisho wa maisha ya hapa duniani ya Kristo. Neno, la Baba lilifanyika katika ukimya katika holi la wanyama na juu ya msalaba. Katika usiku wa kuzaliwa na ule wa Pasaka.  Papa Francisko aliongeza kusema kuwa usiku ule ambao walisikiliza kwa kimya mbele ya Msalaba wa Mtakatifu Damiano, kama wafuasi wanaosikiliza mbele ya msalaba, Meza kuu ya Mwalimu. Kukaa hapo Papa alisema hakukuwa nikunyamaza utupu, lakini ulikuwa ni muda uliojaa matarajio na wa uwezekano. Katika ulimwengu uliojaa kelele hatukuzoea kimya na badala yake inakuwa ngumu kweli kuvumilia, kwa sababu, kimya kinatuweka mbele ya kubiliana na hali halisi yetu. Licha ya hayo msingi wake ni neno na maisha. Mtakatifu Paulo anasema kuwa huduma ya Neno lililofanyika mwili, lilikuwa limezungushwa na ukimya milele (Rm 16, 25) likitufundisha kuwa ukimya unahifadhi huduma, kama Ibrahimu alivyokuwa anahifadhi Agano, kama Maria alivyohifadhi katika umbu lake na kutafakari katika moyo maisha ya mwanae ( Lk 1,31: 2,19.51). Ili kufikia moyo wa waamini, ukweli hauna haja ya kupiga kelele kwa nguvu, kwa sababu  Mungu hapendi tangazo na kelele, gumzo na kelele; Yeye  anapendelea, kama alivyofanya kwa Eliya akizungumza katika upepo mwanana(1Waf 19, 12) kwa maana nyingine kwa ukimya. Na kwa hiyo Baba Mtakatifu alisema kama Ibrahim na Elia na kama Maria wao wanahitaji kujikomboa dhidi ya kelele nyingi ili kusikiliza sauti. Kwa sababu ni kwa ukumya tu inawezekana kusikiliza neno lake.

Mkesha wa Kiekuemeni
Mkesha wa Kiekuemeni

Pili Baba Mtakatifu ameeleza kuwa ukimya ni muhimu katika maisha ya Kanisa. Katika kitabu cha matendo ya mitume kinasema kuwa baada ya Hotuba ya Petro katika Mtaguso wa Yerusalemu, Mkutano wote ulikaa kimya( Mdo 15,12), kwa kijiandalia kusikiliza ushuhuda wa Paulo na Barnaba  karibu ishara na miujiza ambayo Mungu alikuwa ametimiza kati ya mataifa. Hii inatukumbusha kwamba ukimya, katika jumuiya ya kikanisa, huwezesha mawasiliano ya kidugu, ambapo Roho Mtakatifu anapatanisha maoni. Kuwa sinodi ina maana ya kukaribishana sisi kwa sisi kwa njia hii, kwa kufahamu kwamba sisi sote tuna jambo la kushuhudia na kujifunza, tukijiweka pamoja ili kumsikiliza “Roho wa kweli”(Yn 14:17) ili kujua “anachosema kwa Makanisa”(Uf 2:7). Na ukimya huruhusu utambuzi, kwa kusikiliza kwa makini “kuhumia kusikoweza kutamkwa” (Rum 8:26) kwa Roho ambaye mara nyingi hufichwa ndani ya Watu wa Mungu. Kwa hiyo na tumwombe Roho kipaji cha kusikiliza kwa washiriki katika Sinodi: "kumsikiliza Mungu, hata kusikia kilio cha watu pamoja naye; kuwasikiliza watu, hadi kufikia hatua ya kupumua ndani yao mapenzi ambayo Mungu anatuitia.

Sala ya Kiekuemeni ikiwa ikiwa na tamasha la vijana
Sala ya Kiekuemeni ikiwa ikiwa na tamasha la vijana

Ukimya ni muhimu katika safari ya umoja wa Kikristo ambapo Baba Mtakatifu katika kipengele cha tatu amekazia kusema kuwa kwa hakika ni jambo la msingi kwa maombi, ambapo uekumeni huanza na bila hiyo ni tasa. Yesu kwa hakika, aliomba kwamba wanafunzi wake “wawe kitu kimoja”(Yn 17:21). Ukimya unaofanywa maombi huturuhusu kukaribisha zawadi ya umoja "kama Kristo anavyotaka", "kwa njia anayotaka" sio kama matunda ya uhuru wa juhudi zetu na kulingana na vigezo vya kibinadamu tu. Kadiri tunavyomgeukia Bwana pamoja katika maombi, ndivyo tunavyohisi kwamba ni Yeye anayetutakasa na kutuunganisha zaidi ya tofauti zetu. Umoja wa Kikristo unakua katika ukimya mbele ya msalaba , na hasa kama mbegu ambazo walikuwa wapokee kama ishara ya siku hili na ambazo zinamaanisha zawadi nyingi kutoka katika Roho Mtakatifu kwa tamaduni tofauti: kwa hiyo shughuli yao ni kizipanua, kwa uhakika kuwa Mungu tu ndiye anajalia kukua(1Kor 3,6). Hizo zitakuwa ishara kwa ajili yetu, walioalikwa kwa mara nyingine kukaa kimya cha binafsi ili kwa njia ya roho mtakatifu waweze kukua katika umoja na Mungu na katika udugu kati yetu.

Uwanja waulipendeza sana
Uwanja waulipendeza sana

Baba Mtakatifu Francisko alibainisha kuwa "tuombe katika sala ya pamoja ili kujifunza kwa upya kufanya ukimya wa  kusikiliza sauti ya Baba, wito wa Yesu na kilio cha Roho. Tuombe kwamba Sinodi iwe Kairos ya udugu mahali ambapo Roho Mtakatifu anasafisha Kanisa na minong’ono, itikadi na kutojali".  Na “Wakati tukielekea katika maadhimisho muhimu ya Mtaguso wa Nikea, Papa amesema "tuombe ili kujua namna ya kuabudu tukiwa pamoja na kwa ukimya kama Mamajusi Fumbo la Mungu aliyefanyika mwanadamu, kwa uhakika kuwa tutakuwa katibu na Kristo na tutakuwa na umoja kati yetu. Na kama wenye hekima kutoka Mashariki walivyofika huko Bethlehemu wakiongozwa na nyota kuu, ndivyo nuru ya mbingu itatuongoze katika umoja wetu kwa Bwana, katika umoja ambao Yeye mwenyewe aliomba. Tujiweke katika safari ya pamoja kwa sahuku ya kukutana naye, kumwabudu na kumtangaza kwa sababu ulimwengu uweze kuamini". Alihitimisha.

Nia za Papa za Maombi Oktoba 2023

 

30 September 2023, 18:30