Tafuta

Papa:Mfano wa mwenyeheri José Gregorio Hernández,mkristo achafue mikono!

Baba Mtakatifu katika mwendelezo wa mzunguko wa Katekesi juu ya ari ya kitume amefafanua juu ya sura ya daktari wa maskini wa Venezuela José Gregorio Hernandez Cisneros kuwa ni kielelezo cha Mkristo aliyejitolea kwa wanyonge.“Papa amewapongeza wakina mama kwa kutambua kurithisha imani kupitia kilugha na wanajua kuzungumza na watoto wao.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Jumatano tarehe 13 Septemba 2023 Baba Mtakatifu Francisko ametoa katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Akianza katekesi amesema, kuwa katika kakesi zetu tuendelee kukutana na mashuhuda wenye shauku ya kutangaza Injili. Tukumbe kuwa huu ni mfululizo wa katekesi kuhusu ari ya utume, kwa utashi na hata hamu ya ndani ya kupeleka mbele Injili. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amegeukia Nchini Venezuela, barani Amerika ya Kusini, ili kujua sura ya mtu wa kawaida, Mwenyeheri José Gregory Hernández Cisneros.

Hata salamu za wanandoa wapya wakimsalimia Papa
Hata salamu za wanandoa wapya wakimsalimia Papa

Alizaliwa mnamo 1864 na kuridhishwa imani hasa na mama yake kama yeye anavyosimulia. Mama yangu alinifundisha wema toka utotoni na akanikuza katika elimu ya Mwenyezi Mungu na akanipa kutoa sadaka kama mwongozo". Tuwe makini na hilo: ni akina mama wanaopitisha imani. Imani hupitishwa katika kilugha, yaani kwa lugha ya akina mama, kilugha ambacho  akina mama wanajua kuzungumza na watoto wao. Papa amewageukia akina mama kwamba wawe makini wakati wa kusambaza imani katika lugha hiyo ya mama, na amewaomba wapigiwe makofu. Akiendelea na mwenyeheri Gregory amesema kwa "Hakika, upendo ulikuwa nyota inayoongoza  na iliyoongoza uwepo wa Mwenyeheri José Gregory kwani alikuwa ni mtu mzuri na mchangamfu, mwenye tabia ya furaha, na alijaliwa kuwa na akili nyingi; akawa daktari, profesa wa chuo kikuu na mwanasayansi. Lakini kwanza alikuwa daktari wa karibu na wanyonge, kiasi kwamba alijulikana katika nchi yake kama "daktari wa maskini". Daima aliwaangalia maskini.

Kikundi cha watoto kutoka bara la Asia katika katekesi ya Papa
Kikundi cha watoto kutoka bara la Asia katika katekesi ya Papa

Kuliko kuwa na utajiri wa pesa yeye alipendelea zaidi utajiri wa  Injili, akitumia maisha yake kuwasaidia wahitaji. Katika maskini, katika wagonjwa, katika wahamiaji, katika mateso, José Gregory alimwona Yesu. Na mafanikio ambayo hakuwahi kuyatafuta duniani aliyapokea, na anaendelea kuyapata, kutoka kwa watu, wamwitao “mtakatifu wa watu. Mtume wa upendo, mmisionari wa matumaini. Papa ameongeza kusema kuwa:  “Haya ni  majina mazuri,  ya kuwa  Mtakatifu wa watu, mtume wa upendo, mmisionari wa matumaini". Kwa hiyo José Gregory alikuwa mwanamume mnyenyekevu, mtu mwenye fadhili na wa msaada. Na wakati huo huo aliongozwa na moto wa ndani, na shauku ya kuishi katika huduma ya Mungu na wengine. Akisukumwa na bidii hiyo, alijaribu mara kadhaa kutaka kuwa mtawa na padre lakini matatizo mbalimbali ya afya yalimzuia kufanya hivyo. Hata hivyo, udhaifu wake wa kimwili haukumsababisha kujiondoa ndani yake mwenyewe, lakini kuwa daktari hata zaidi anayejali mahitaji ya wengine; aling'ang'ania mapaji ya kimungu na, akiwa na nguvu katika nafsi yake, akaenda zaidi kwa mambo muhimu.

Katika Katekesi ya Papa 13 Septemba 2023
Katika Katekesi ya Papa 13 Septemba 2023

Papa amekazia kusema kuwa hapo  ndipo bidii yake ya kitume, kwa sababu hakufuata matamanio yake mwenyewe, bali kupatikana kwake katika mipango ya Mungu. Na kwa hiyo Mwenyeheri alielewa kwamba, kwa njia ya utunzaji wa wagonjwa, ataweka mapenzi ya Mungu katika matendo, akiwasaidia wanaoteseka, akiwapa matumaini maskini, akiishuhudia imani si kwa maneno bali kwa mifano. Hivyo alifikia kwenye njia hiyo ya ndani ya kukaribisha kama ukuhani, kwa hiyo ukuhani wa dawa ya maumivu ya binadamu.” Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa ni muhimu kwa  jinsi gani kutoteseka tu, bali, kama Maandiko yanavyosema, kufanya kila kitu kwa moyo mwema,  wa kumtumikia Bwana (taz. Kol 3:23).

Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa "Lakini nasi ni vema  tujiulize:  Je! José Gregory alipata wapi shauku yote hiyo, bidii hiyo yote? Ilitoka kwa uhakika na nguvu. Hakika ilikuwa ni neema ya Mungu. Yeye mwenyewe aliandika kwamba “ikiwa kuna wema na wabaya duniani, wabaya wapo kwa sababu wao wenyewe wamekuwa wabaya: lakini wema ni wema kwa msaada wa Mungu” (27 Mei 1914). Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa naye alikuwa wa kwanza kuhisi haja ya neema, akiiomba barabarani na kuhitaji sana upendo. Na hii ndiyo nguvu aliyojiwekea ya  ukaribu na Mungu. Alikuwa mtu wa maombi  kwani  kuna neema ya Mungu na urafiki wa karibu na Bwana  ambapo alikuwa mtu wa sala  na ambaye daima alishiriki katika Misa. Na katika kuwasiliana na Yesu, ambaye anajitoa mwenyewe kwenye sadaka  kwa ajili ya kila mtu, José Gregorio alihisi kuitwa kutoa uhai wake kwa ajili ya amani.

Waamini kutoka pande za dunia katika Katekesi ya Papa
Waamini kutoka pande za dunia katika Katekesi ya Papa

Vita vya Kwanza vya Ulimwengu vilikuwa vikiendelea. Hivyo mnamo tarehe 29 Juni 1919,  rafiki mmoja alimtembelea na kumkuta  akiwa na furaha sana. José Gregory alifahamu kwamba mkataba wa kumaliza vita umetiwa saini. Toleo lake lilikuwa limekubaliwa, na ni kana kwamba alihisi kwamba kazi yake duniani imekamilika. Asubuhi hiyo, kama kawaida, alikuwa kwenye Misa na baadaye akaelekea barabarani ili kumpelekea mgonjwa dawa. Lakini, wakati anavuka barabara, aligongwa na gari; akapelekwa hospitali, ambapo alifariki akiwa anatamka jina la Maria. Safari yake ya kidunia iliishia hivyo, akiwa njiani anafanya kazi ya huruma, na akiwa hospitalini, ambako alikuwa amefanya kazi yake kuwa nzuri kama daktari.

Watawa wakiwa na picha ya pamoja na Papa
Watawa wakiwa na picha ya pamoja na Papa

Baba Mtakatifu kwa hiyo amesema mbele ya ushuhuda huo tujiulize: nifanye nini mbele ya Mungu wa sasa, aliyepo katika maskini karibu nami, katika uso wa dunia? Na mfano wa José Gregory unanihusuje? Anatuchochea kujitolea kwa masuala makubwa ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ya leo. Wengi huzungumza juu yake, wengi husengenya juu yake, wengi hukosoa na kusema kwamba kila kitu ni kibaya.  Lakini Mkristo hajaitwa kufanya hivyo, bali kushughulika nalo, kuchafua mikono yake; kwanza kabisa, kama vile Mtakatifu Paulo alivyotuambia, kusalia (taz 1Tim 2:1-4), na kisha kushiriki, si kwa mazungumzo, hapana, mazungumzo ni tauni: hapana, bali kukuza mema na kujenga amani na haki katika ukweli. Hii pia ni bidii ya kitume, ni utangazaji wa Injili, na hii ni furaha ya Kikristo: "Heri wapatanishi" (Mt 5:9). "Tuendele katika njia ya Mwenyeheri Gregory, ambaye ni mlei, daktari, mtu wa kazi ya kila siku ambaye bidii yake ya kitume ilimsukuma kuishi kwa kufanya upendo katika maisha yake yote."

Katekesi ya Papa 13 Septemba 2023
13 September 2023, 10:42