Tafuta

Padre Luis Pascual DRI, OFM Cap ni mmoja wa makardinali wateule mwenye umri miaka 96 Muungamishi katika madhabahu ya‘’Nueva Pompeya’ nchini Argentina. Padre Luis Pascual DRI, OFM Cap ni mmoja wa makardinali wateule mwenye umri miaka 96 Muungamishi katika madhabahu ya‘’Nueva Pompeya’ nchini Argentina. 

Papa:Septemba 30,Papa anasimika makardinali wapya 21 akiwepo Padre Dri

Papa anatarajia kuwasimika makardinali 21 mjini Vatican walitoteuliwa mnamo 9 Julai 2023.Miongoni mwao makardinali wateule kuna Padre Dri mwenye umri wa miaka 96 kutoka Argentina na watatu kutoka Afrika:Askofu mkuu mwandamizi Rugambwa,Tanzania,Askofu mkuu Martin MULLA,Sudan ya Kusini Askofu mkuu Stephen Brislin wa Jimbo kuu la Cape Town,Afrika Kusini.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Manmo Dominika tarehe 9 Julai 2023 Baba Mtakatifu Francisko aliwateua Makardinali wapya 21 ambao watasimikwa rasmi katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Makardinali utakaoadhimishwa Jumamosi tarehe 30 Septemba 2023 mjini Vatican. Makardinali hao wanatoka katika mabara matano ya ulimwengu ili kuwakilisha umoja wa Kanisa na Kharifa wa mtume Petro.

Padre Luis Pascual Dri, mwenye umri wa miaka 96, anaendelea kuungamisha waamini wanaomiminika kila siku katika madhabahu ya Mama Yetu wa Pompei Nchini Argentina hata tangu Dominika ya tarehe 9 Julai 2023, wakati  Baba Mtakatifu Francisko alitaja jina lake katika orodha ya makadinali wapya 21. Zaidi ya hayo, chaguo la Baba Mtakatifu lilimwangukia kutokana na utendaji wake yaani  shughuli hii isiyochoka kama muungamishi, kwa uwezo wake wa kuudhihirisha uso wa ukaribishaji na huruma ya Mungu, unaojulikana sana na Askofu Mkuu Jorge Mario Bergoglio (Papa Francisko), alipokuwa huko Buenos Aires kabla ya kuwa Papa. Papa  pia kwa wakati mwingine aliweza kumfafanua kama  sura muhimu ya muungamishi na kwa sababu hiyo atapokea kikofia chekundu  Jumamosi  tarehe 30 Septemba 2023  licha ya kutokuwa askofu, bali kutunukiwa  heshima hiyo kwa uwajibikaji wake bila kuchoka.

Padre huyo alizaliwa mnamo  tarehe 17 Aprili 1927 huko Federación, jimbo la Entre Ríos (Argentina), katika familia ambayo watoto wote, isipokuwa yeye tu, aliitwa na  Mungu katika maisha ya kitawa. Alijiunga na Seminari ya Wakapuchini mnamo Januari 1938, akiwa na umri wa miaka 11 tu, na akamaliza masomo yake ya msingi na sekondari. Katika kitongoji cha Montevidea cha Nuevo París, Uruguay, aliingia novisi. Alifunga nadhiri za kitawa kwa  Wakapuchini mnamo 21 Februari 1945. Mnamo 1949 alifunga nadhiri za daima. Tarehe 29 Machi 1952 alipewa daraja la Upadre katika kanisa kuu la Montevideo. Tangu wakati huo, nafasi nyingi, imekuwa  kama mkurugenzi wa semina,  mwalimu, katika sehemu nyingi huko Argentina, sehemu nyingine za Ulaya ambapo mnamo 1961, alikuja kwenye mafunzo ya utaalamu kama mkufunzi wa unovisi. Alikuwa paroko mara kadhaa,na mwanzoni mwa 2000 alihamishwa na kuwa na jukumu hili la kuungamisha kwenye madhabahu ya Mama Yetu wa Pompeya, huko Buenos Aires, ambako alikaa miaka mitatu; kisha, uhamishohuko Mar del Plata na, kuanzia 2007, kurudi kwa uhakika kwenye Madhabahu hiyo ya  Buenos Aires.

Leo hii akiwa na umri wa miaka 96, bado  anaendelea kumtumikia Bwana  kwa kutumia masaa mengi kuungamisha kila siku akitoa Sakramenti ya kitubio na upatanisho. Katika mahojiano  na shirika la habari za Kidini la Baraza la Maaskofu Italia (SIR) Padre Dri kama angekuja Roma alisema: “Hapana, sitakuwa Roma, ingawa ningemkumbatia kwa furaha Papa Francisko. Hali yangu ya afya hainiruhusu kufanya hivyo. Nembo italetwa kwangu hapa Buenos Aires, askofu mkuu aliniita na kunielezea na kutakuwa na sherehe. Hata hivyo Mtawa huyo Mkapuchini kwa sasa anatembelea kiti cha magurudumu, lakini sauti yake ni safi kabisa, mawazo yake ni ya busara, pamoja na dozi kubwa ya vichekezo vikichanganyika  na huruma na upole.

Hebu turejee tarehe 9 Julai 2023, Ulijisikiaje uliposikia habari hizo?

Nilishikwa na mshangao kabisa. Walianza kuniambia jambo hilo, na nilifikiri walikuwa wananichezea utani tu. Kisha, nilipotambua kwamba yote ni kweli, nililia kwa muda mrefu, sikujua la kusema au la kufanya! Sasa nimetulia, ninatambua kwamba Bwana alinihurumia, kwa utambuzi huu.”

Je siri yako kama muungamishi ni ipi?

Ninajiona kama muungamishi asiyechoka. Kuna hitaji kubwa sana leo hii, katika ulimwengu uliojaa hali nyingi ngumu, ambazo huzidisha na kuhusisha watu.

Wanasema wewe ni mtu  mzuri sana, kwamba unasamehe kila mtu ...

Sikatai, lakini daima ninamwambia Yesu: “Wewe ndiye uliyesamehe sana, ambaye amesamehe kila mtu! Ninajaribu kufanya kama yeye. Kwa sababu Yesu hakumnyima mtu yeyote msamaha. Nilimjua Askofu Mkuu Bergoglio vizuri, na yeye pia, kwa kusema, ‘alinisamehe’ kwa hili.

Je unaweza kusema nini juu ya  maisha yako leo hii?

Ndiyo, tuseme ni kazi yangu, kuanzia asubuhi na mapema. Ninajaribu kuwakaribisha watu, kusikiliza. Tunaishi katika miaka iliyo na mashaka makubwa, ukosefu wa amani na utulivu. Ni muhimu kufikisha upendo wa Yesu Yeye ndiye kitovu cha kila kitu! Nilijifunza nikiwa mtoto, kutoka kwa mama yangu, ambaye alinifundisha kuwa mwamini. Baba yangu alikufa nilipokuwa na umri wa miaka minne.

Unatumia maneno gani kuwasilisha kipaumbele hiki?

Ninajaribu kuweka utulivu na amani ya ndani. Ni muhimu kwamba unatoa chuki au chuki katika nafsi. Msamaha unahitaji msamaha, na hii ndiyo suluhisho pekee, hata unapokabiliwa na hali ambayo hewa imechafuliwa na chuki, kama inavyotokea pia katika Argentina yetu. Katika jamii, lakini pia katika Kanisa, kuna migawanyiko mingi, lazima tubadilike. Na uwongofu una jina moja tu: Nafsi ya Yesu. Uhusiano na Yesu ni jambo la msingi, zaidi la dini kuliko yaliyomo katika katekesi. Yote huanza kutoka hapo, kuwa mmoja naye. Ni lazima tumtumaini yeye, yeye ni amani, maisha yetu.

Je, ni kweli kwamba unawathamini sana watakatifu wengine Wakapuchini, waamini wakuu, kama vile Mtakatifu Leopoldo Mandic na  Padre Pio wa  Pietrelcina?

Kwa hakika! Nilitembelea maeneo  Mtakatifu Leopoldo, huko Padova. Alikufa wakati wa vita, lakini alikuwa mtu mkuu wa amani na umoja. Alijitolea kuungama na kwa unyenyekevu aliendeleza upatanisho. Nilikutana na Padre Pio kibinafsi huko Mtakatifu Giovanni Rotondo. Mnamo mwaka 1961 niliungama kwake, nilizungumza naye, na kisha tena mnamo  1968. Wote wawili wananitia moyo kuungamisha.

Papa alikwambia nini?

Nilipomwambia kwamba nisingeweza kuja Roma, lakini alisema usijali! Zaidi ya  yote, niliwahi kukaa naye, huko Mtakatifu  Marta, mnamo 2018, kwa siku chache. Nilimwona, hata katika tukio hilo, kama baba anayekumbatia na kubariki, lakini zaidi ya yote kama kaka.

Je, unatuachia wazo la mwisho?

Kupitia sisi ulimwengu lazima ujue kwamba Mungu ni mwema, na kwamba yeye husamehe daima, hatupaswi kuogopa.

Maaskofu wakuu kutoka Afrika ni Askofu mkuu mwandamizi Protase Rugambwa wa Jimbo kuu la Tabora, Tanzania, Askofu mkuu Stephen Ameyu Martin MULLA, Jimbo kuu la Juba, Sudan ya Kusini pamoja na Askofu mkuu Stephen Brislin wa Jimbo kuu la Cape Town, Afrika Kusini. Makardinali wapya hao  watasimikwa rasmi katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Makardinali utakaoadhimishwa Jumamosi tarehe 30 Septemba 2023 mjini Vatican.

Makardinali wengine kutoka mabara mengine

Makardinali wateule wengine ni  Askofu mkuu Robert Francis PREVOST, O.S.A., Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa; Askofu mkuu Claudio GUGEROTTI, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki; Askofu mkuu Víctor Manuel FERNÁNDEZ, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Askofu mkuu Emil Paul TSCHERRIG, Balozi, Askofu mkuu Christophe Louis Yves Georges PIERRE, Balozi, Askofu mkuu Pierbattista PIZZABALLA, Patriaki wa Madhehebu ya Kilatini mjini YerusalemuAskofu mkuu Ángel Sixto ROSSI, S.J., wa Jimbo kuu la Córdoba; Askofu mkuu Luis José RUEDA APARICIO, wa Jimbo kuu la Bogotá; Askofu mkuu Grzegorz RYŚ, wa Jimbo kuu la Łódź,; Askofu mkuu José COBO CANO, wa Jimbo kuu la Madrid,;  Askofu mkuu Sebastian FRANCIS, wa Jimbo kuu la Penang; Askofu Stephen CHOW SAU-YAN, S.J., Askofu wa Hong Kong: Askofu François-Xavier BUSTILLO, O.F.M. Conv., wa Jimbo la Ajaccio, Askofu msaidizi Américo Manuel ALVES AGUIAR, wa Jimbo kuu la Lisbon, Ureno pamoja na Padre Ángel FERNÁNDEZ ARTIME, s.d.b., Mkuu wa Shirika la Wasalesian wa Don Bosco. Askofu mkuu Agostino MARCHETTO, Balozi; Askofu mkuu mstaafu Diego Rafael PADRÓN SÁNCHEZ, wa Jimbo Cumaná;

Padre Luis Pascual DRI, OFM Cap., ambaye ni Muungamishi wa Madhabahu ya Mama Yetu wa Pompei, Buenos Aires nchini Argentina.

Padre Dri wa miaka 96 atapewa kofia ya ukardinali
29 September 2023, 17:32