Tafuta

2023.09.11 Papa Francisko na  Baselios Marthoma Mathews III Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox la Kisiria huko Malankara. 2023.09.11 Papa Francisko na  Baselios Marthoma Mathews III Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox la Kisiria huko Malankara.  (Vatican Media)

Pongezi ya Papa kwa jitihada ya uekumeni wa kichungaji na Waorthodox

Papa amekutana na Baselios Marthoma Mathews III,Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox la Malankara,kwa mara ya kwanza mjini Vatican tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2021.Katika hotuba anakumbuka mageuzi ya mahusiano ya pande zote mbili,amepongeza kazi ya uekumeni wa kichungaji kutafsiriwa katika makubaliano na maamuzi ya pamoja na ushiriki wa mjumbe katikaka Sinodi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kama ilivyokuwa tayari taarifa imetolewa juu kuhusu mkutano wa Mkuu wa Kanisa la  Kiorthodox  la Kisiria  la Malankara, Baselios Marthoma Mathews III,  Baba Mtakatifu,  Jumatatu tarehe 11 Septemba 2023,  amekutana naye. Katika hotuba yake mara baada ya kusikiliza Papa ameshukuru kwanza kwa maneno yake na ziara ya kutembelea mji wa Mitume Petro na Paulo mahali ambapo yeye mwenyee tayari aliishi na kusoma na sasa amerudi akiwa kama mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Siria linaloheshimika la Malankara. Kwa hiyo Papa ameomba kusema kwa heshima yake, ajisijie  nyumbani, kama Ndugu mpendwa na aliyesubiriwa kwa muda mrefu. Pamoja naye alipenda kumshukuru Bwana kwa vifungo ambavyo wameanzisha katika miongo ya hivi karibuni.  “Kukaribiana kwa Makanisa yetu, baada ya karne nyingi za kutengana, kulianza na Mtaguso wa Pili wa Vatican, ambapo Kanisa la Kiorthodox la Malankara la Siria lilituma waangalizi fulani. Wakati huo, Mtakatifu Paulo VI alikutana na Baselios Augen I huko Bombay mnamo 1964.”

Papa alimkaribisha Kiongozi  Mkuu wa Kiorthodox wa Malankara
Papa alimkaribisha Kiongozi Mkuu wa Kiorthodox wa Malankara

Kwa njia hiyo Papa amesema kuwasili kwake sasa kunalingana na kumbukumbu ya miaka arobaini ya ziara ya kwanza ya Roma kwa Mkuu wa kanisa lao pendwa iliyofanywa mwaka 1983 kati ya  Baselios Marthoma Mathews I, ambaye Mtakatifu Yohane Paulo II alimtembelea miaka mitatu baadaye katika Kanisa Kuu la Mar Elia huko Kottayam. Baba Mtakatifu amebainisha kuwa Mwaka huu 2023 pia wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi ya kukumbatiwa na  mtangulizi wake wa karibu, Baselios Marthoma Paulose II, ambayo ni  kumbukumbu yenye baraka, ambaye alipata furaha kumpokea mwanzoni mwa Upapa wake mnamo, Septemba 2013.

Papa na wajumbe wa Kiorthodox

Baba Mtakatifu Francisko pia amesema kwamba kwa kumkaribisha yeye na na wajumbe wake ametoa salamu kwa  ndugu maaskofu, mapadre  na waamini wa Kanisa la Kiorthodox la Kisiria  la Malankara, ambapo  chimbuko lake linarejea kwenye mahubiri ya Mtume Tomasi, ambaye, mbele ya yule Mfufuka, alisema kwa mshangao: “Bwana wangu na Mungu wangu!”(Yoh 20:28). Kwa maombi na woga, taaluma hii, ambayo inatangaza Bwana wa wokovu na Umungu wa Kristo, unaweka msingi wa imani yetu ya pamoja. Papa Francisko amesema ni imani hiyo hiyo ambayo anatumaini tutasherehekea pamoja katika maadhimisho ya mwaka wa 1,700 wa Baraza la kwanza la Uekumeni la Nikea.

Wakati wa sala na kiongozi mkuu wa kiorthodox
Wakati wa sala na kiongozi mkuu wa kiorthodox

Imani ya Mtakatifu Thomasi haikutenganishwa na uzoefu wake wa majeraha ya Mwili wa Kristo (taz. Yn 20:27). Mgawanyiko ambao umetokea katika historia kati yetu sisi Wakristo umekuwa ni majeraha maumivu yanayotokana na Mwili wa Kristo yaani Kanisa. Sisi wenyewe tunaendelea kushuhudia matokeo yake. Hata hivyo tukigusa majeraha haya pamoja; ikiwa, kama Mtume, tunatangaza pamoja kwamba Yesu ni Bwana wetu na Mungu wetu; na ikiwa, kwa moyo wa unyenyekevu, tunajikabidhi kwa neema yake ya ajabu, tunaweza kuharakisha siku inayotazamiwa na watu wengi, ambapo kwa msaada wake tutaadhimisha Fumbo la Pasaka kwenye madhabahu ile ile.” Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza.

Kulikuwa na fursa ya kusali pamoja na ujumbe wake
Kulikuwa na fursa ya kusali pamoja na ujumbe wake

Papa Francisko amesema na wakati huo huo, “tusonge mbele pamoja katika sala inayotutakasa, katika upendo unaotuunganisha, na katika mazungumzo yanayotuleta karibu zaidi na zaidi. Nafikiri kwa namna ya pekee kuanzishwa kwa Tume ya Pamoja ya Kimataifa ya mazungumzo kati ya Makanisa yetu, ambayo ilisababisha makubaliano ya kihistoria ya Kikristo, yaliyochapishwa siku ya Pentekoste 1990. Hili lilikuwa ni Tamko la Pamoja linalothibitisha kwamba yaliyomo katika imani yetu katika fumbo la Ukristo. Neno lililofanyika mwili ni sawa, ingawa tofauti na  mkazo zimetokea katika uundaji wake katika historia. Azimio hilo linasema kwa kupendeza kwamba, “tofauti hizi ni kama vile zinaweza kuwepo pamoja katika ushirika uleule na kwa hiyo hazihitaji na hazipaswi kutugawanya, hasa tunapomtangaza Kristo kwa kaka na dada zetu ulimwenguni pote kwa maneno ambayo wanaweza kuelewa kwa urahisi Zaidi.” Kumtangaza Kristo kunaunganisha badala ya kugawanya; tangazo la pamoja la Bwana wetu linainjilisha safari yenyewe ya kiekumeni.

Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema kufuatia Azimio la Pamoja, Tume imekutana huko Kerala karibu kila mwaka na imezaa matunda mazuri, ikikuza ushirikiano wa kichungaji kwa manufaa ya kiroho ya Watu wa Mungu. Nakumbuka kwa shukrani hasa mikataba ya mwaka 2010 juu ya matumizi ya pamoja ya maeneo ya ibada na madhabahu na juu ya uwezekano kwamba, katika mazingira fulani, waamini wa Kanisa lolote wanaweza kupokea upako wa wagonjwa. Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya kazi ya Utume huu, unaolenga zaidi maisha ya kichungaji, kwani uekumene wa kichungaji ndiyo njia ya asili ya umoja kamili. Kama vile Baba Mtakatifu alivyopata nafasi ya kusema kwa Tume ya Pamoja ya Kimataifa ya Mazungumzo ya Kitaalimungu kati ya Kanisa Katoliki na Makanisa ya Kiorthodox ya Mashariki, ambayo Kanisa lake  limekuwa muumini wake tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka wa 2003, "Uekumeni daima una tabia ya kichungaji’.

Ni kwa kusonga mbele kidugu katika kuhubiri Injili na utunzaji madhubuti wa waamini tunajikubali sisi wenyewe kuwa ni kundi moja la mahujaji wa Kristo. Kwa maana hiyo, ni matumaini ya Baba Mtakatifu  kwamba, mikataba ya kichungaji kati ya Makanisa yetu yanayoshiriki urithi mmoja wa kitume, inaweza kuenea na kustawi hasa katika maeneo ambayo waamini wake wachache au wanaishi nje ya nchi. Pia Papa amefurahishwa na ushiriki wao wa dhati katika ziara za mafunzo kwa mapadre na watawa vijana zinazoandaliwa kila mwaka na Baraza la Kipapa la kuhamasisha Umoja wa Kristo, na ambazo zinazochangia uelewano bora kati ya wachungaji.

Hata wakati wa kubariki kwa Pamoja
Hata wakati wa kubariki kwa Pamoja

Katika mchakato wa safari ya pamoja kuelekea umoja kamili, njia nyingine muhimu ni ile ya sinodi. Miaka kumi iliyopita, jijini Roma, Mtangulizi wake alitangaza kuwa: “Ushiriki wa wawakilishi wa Kanisa la Kiorthodox la Malankara katika mchakato wa maridhiano wa Kanisa Katoliki tangu Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ambao umekuwa wa umuhimu kwa ukuaji wa maelewano. Ni furaha ya Papa kwamba ndugu mjumbe kutoka Kanisa lake atashiriki katika kikao kijacho cha Baraza la Sinodi ya Maaskofu inayokaribia. Papa anao uhakika kwamba ‘tunaweza kujifunza mengi kutokana na uzoefu wa zamani wa sinodi la Kanisa lao. Kwa maana fulani, Harakati la kiekumeni inachangia katika mchakato unaoendelea wa sinodi ya Kanisa Katoliki, na ni matumaini ya Papa. Sinodi na uekumeni kiukweli ni njia mbili zinazoendelea pamoja, zikiunganishwa na lengo moja, lile la ushirika, ambalo linamaanisha ushuhuda wenye ufanisi zaidi wa Wakristo “ili ulimwengu upate kuamini” (Yn 17:21).

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi

"Ilikuwa ni kwa ajili ya hili kwamba Bwana aliomba kabla ya Pasaka, na hivyo ni sawa kwamba mkutano wa leo utaendelea na maombi. Mtakatifu Thomasi Mtume atuombee kwa ajili ya safari yetu ya umoja na ushuhuda. Masalia yake yanatunzwa katika Jimbo Kuu la Lanciano-Ortona, linalowakilishwa hapa na Askofu Mkuu Emidio Cipollone. Asante kwa uwepo wako." Wakati Bwana alipomwonesha majeraha yake, Mtakatifu Thomas alipita kutoka upagani hadi kwenye imani kwa kile alichokiona. Tafakari yetu ya pamoja ya Bwana aliyesulubiwa na kufufuka iongoze kwenye uponyaji kamili wa majeraha yetu ya zamani, ili, mbele ya macho yetu, kupita umbali wote na kutokuelewana, aonekane, “Bwana wetu na Mungu wetu” (taz. Yn 20; 28), ambaye anatuita kumtambua na kumwabudu katika altare  moja ya Ekaristi.

Papa alikutana na kusali na Kiongozi wa kiordhodox wa Malankara
11 September 2023, 16:34