Tafuta

2023.09.14 Papa amekutana na washiriki wa Mkutano wa kiekumeni kuhusu barua za Mtume Paulo. 2023.09.14 Papa amekutana na washiriki wa Mkutano wa kiekumeni kuhusu barua za Mtume Paulo.  (Vatican Media)

Papa:ndani ya Uekumeni kuna Ujasiri wa kinabii na ujasiri wa kushinda vizingiti

Papa akikutana washiriki wa Kongamano la 26 la Kiekumeni la Paulo amesisitizia juu ya kubadili dira ya mgawanyiko na kuelekea katika umoja.Mpango huo,unawaleta pamoja wasomi wa madhehebu na tamaduni tofauti za Kikristo,zinawezesha kushinda vikwazo vya kutoaminiana katika kukutana na wengine hivyo kukuza mazungumzo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa XXVI wa Mazungumzo ya Kiekumeni kuhusu Barua za Mtakatifu Paulo Mtume, tarehe 14 Septemba 2023 mjini Vatican. Amewashukuru kwa kufika kwao ambao wameunganika huko mjini Roma na katika Kanisa Kuu zuri la Mtakatifu Paulo nje ya Ukuta kwa ajili ya Mazungumzo ya Kiekumeni ya mafunzo ya Paulo. Mpango  huo ulizaliwa kidogo baada ya Mtaguso wa Pili wa Vatican na kikundi cha wasomi waliokuwa wanatoka nchi kumi na zenye tamaduni mbali mbali za kikristo, na hivyo imefikia toleo la 26.

Papa amekutana na washiriki wa mazungumzo ya kiekumeni
Papa amekutana na washiriki wa mazungumzo ya kiekumeni

Baba Mtakatifu amebainisa kuwa wao wanaweza kujivunia shauku yao ambayo imechangia utambuzi wa kibiblia na kiroho  wa  Barua za Mtume wa watu. Hili ni tukio ambalo bado ni muhimu kwa kile ambacho mazungumzo yanakuja kati ya madhehebu ya kikristo tofauti na wao wenyewe  wakiwa na shauku ya mafunzo ya Paulo kutoka katika mataifa mbali mbali, kwa kuleta pamoja sio tu umaalum wa mafunzo, lakini hata asili ya utamaduni na maisha ya imani katika jumuiya ya kikristo wanayotokea.

Baba  Mtakatifu amependa kusema kuwa ni mchango mkubwa wa mazungumzo, mkutano kati ya wakristo wengine kati ya na zaidi kuungana katika neema  ya mafundisho ya Paulo; mazungumzo kati ya mambo ambayo yanagusa sehemu tofauti na ambayo yanatafuta ardhi ya pamoja kuanzia na Maandiko; ulinganisho wa ufafanuzi wa kina na wa kisayansi unaopata chimbuko lake muhimu katika muktadha wa sala na hali ya kiroho, ili uzuri wa barua za Mtume na umuhimu wake kwa maisha ya Kikristo na kikanisa uonekane.

Mkutano wa kiekumeni
Mkutano wa kiekumeni

Kuna jambo ambalo ni la ujasiri na kinabii katika mpango wao. Kuna ujasiri wa kushinda vizingiti vya tofauti ambazo mara nyingi zinaibuka hasa tunapata fursa ya kukutana na mwingine. Na baadaye kuna unabii wa kiekumeni, ule mzuri , wa uvumilivu wa Kiroho, ambamo wakristo wote tunaitwa, kwa sababu safari iendelee kuelekea muungano kamili na wala jitihada katika uhuhuda zisikosekane. Ikiwa katika mchakato wa historia, migawanyiko, imekuwa sababu ya mateso, leo hii ni kujibidisha kubadilisha dira, kwa kutazamia mchakato wa umoja na wa udugu ambao unaanza hasa kwa kusali, kujifunza na kufanya kazi pamoja. Shauku yao ya kina katika Barua za Mtume , zilizo kiini cha mafunzo, thamani ya mchango ambao wako wanabadilishana na ambao baadaye watachapisha, mwaka huu inajikita katika sura kuanzia 9-11 za Barua kwa Warumi, Papa amesisitiza.

Mkutano wa Papa na washiriki wa kiekumeni
Mkutano wa Papa na washiriki wa kiekumeni

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amebainisha kuwa ni ufafanuzi wa ajabu wa fumbo la wokovu, ambalo linaleta pamoja na kwa hiyo katika mazungumzo,  karama na wito wa Mungu kwa Israeli, ambao Mtume anafafanua kuwa ‘usioweza kubatilishwa.’(Rm 11,29) na tumaini la Injili. Mtume anatukabidhi ujumbe wa msingi ambao unawakilisha bado ule ambao sio tu wa kufakari katika mafunzo ya kibiblia lakini hata kuendelea kukuza majadiliano ya kiekumeni; Mungu hakawii katika ahadi zake za wokovu na kupelekea mbele kwa uvumilivu, hata kupitia njia zisizofikiria na za kushangaza. Lakini uhakika wa kina ni kwamba waamini wanaweza kuamini juu ya huruma na juu ya ahadi za Mungu. Haya katika udhaifu wao, na katika hatari nyingi zinazowekwa katika imani yao, wanaweza kuhesabu hata katika nguvu za kifo na katika ufufuko wa Kristo, juu ya hahadi muafaka za neema ya Mingu.

Hotuba ya Papa kwa washiriki wa kongamano la 26 la barua za Paulo
14 September 2023, 16:45