Tafuta

2023.09.21  Papa alikutana na washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Amerika Kusini na Carribean. 2023.09.21 Papa alikutana na washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Amerika Kusini na Carribean.  (Vatican Media)

Papa akutana na wakuu wa Vyuo Vikuu vya Amerika Kusini na Carribean

Jina la Waraka Mpya wa kitume wa Papa ni“Laudate Deum.Papa mwenyewe alisema hayo alipokuwa akihutubia washiriki wa mkutano wa wakuu wa vyuo vikuu vya Amerika ya Kusini siku ya Alhamisi 21 Septemba 2023 ambapo alitafakari mada mbalimbali kama vile uhamiaji,mabadiliko ya tabianchi na kutengwa kwa watu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Siku ya Alhamisi, tarehe 21 Septemba, Baba Mtakatifu Francisko alikutana katika ukumbi wa  Clementina, mjini Vatican, takriban na washiriki 200 katika mkutano wa wakuu wa Vyuo Vikuu vya umma na binafsi vya Amerika ya Kusini na Karibiani, uliohamaishwa na Chuo Kikuu cha Red  cha Ulinzi wa Kazi ya Uumbaji (RUC) na Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini (Pcal) tarehe 20 na 21 Septemba katika Chuo Kikuu cha Baba wa Kanisa cha Agostino yenye mada “Kuandaa Tumaini” kwa kushirikisha baadhi ya wakuu na makatibu wa Mabaraza ya Kipapa.

Akitafakari masuala mbalimbali yanayotolewa na waelimishaji yakiwemo mabadiliko ya tabia nchi, uhamiaji, utamaduni wa upotevu, Baba Mtakatifu amewataka kuwa wabunifu katika kuwafunza vijana kuanzia hali halisi na changamoto za sasa. Rectors waliuliza Papa maswali juu ya masuala ya mazingira na hali ya hewa ambayo yeye alijibu kwa kusisitiza kusikitisha "utamaduni wa kutupa au utamaduni wa kutelekezwa". Alieleza kuwa ni "utamaduni wa matumizi yasiyofaa ya maliasili, ambayo haiambatani na asili kwa maendeleo kamili na hairuhusu kuishi. Utamaduni huu wa kuachwa - alisema - unatudhuru sisi sote". Papa alitoa hata jina la Waraka Mpya wa kitume kuwa ni “Laudate Deum. 

Papa na ikolojia
26 September 2023, 13:10