Tafuta

Papa:kusahihishana kidugu na isiwe kikundi cha kuabisha ndugu!

Papa akfiafanua Injili ya Dominika Septemba 10,kuhusiana na kusahihishana kidugu amesema tuwe na umakini kwani siyo ule wa kufanya kikundi cha kusengenya!Yesu anasema“chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili,”akimaanisha watu ambao wanapenda kweli kusaidia kaka huyo na dada ambaye amekosea.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Dominika ya 23 ya Mwaka A tarehe 10 Septemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika dirisha la Jumba la kitume mjini Vatican ametoa mahubiri yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Akianza tafakati hiyo amesema “Leo hii Injili inatuzungumzia juu ya kusahihishana kindugu (Re. Mt 18,15-20) ambayo ni moja ya kielelezo kikuu cha upendo lakini pia kigumu kwa sababu siyo rahisi kuwasahihisha wengine.. Inapotokea kwa ndugu katika imani anatenda kosa dhidi yako, na wewe bila kuwa na kinyongo, kumsaidia kumsahihisha, msaidie na umsahihishe. Kwa bahati mbaya, kitu cha kwanza mara nyingi ni kuunda kwa yule aliyeokosea masengenyo, ambayo kila mtu hujifunza kuhusu kosa, pamoja na maelezo yote, isipokuwa mtu anayehusika! Hii si sawa na haimpendezi Mungu.”

Baba Mtakatifu kwa njia hiyo amethibitisha kuwa hatachoka kamwe kusema kuwa masengenyo ni mdudu mbaya kwa maisha ya watu na  ya jumuiya, kwa sababu yanapelekea migawanyiko, mateso na kashfa, na hayasaidii kamwe kuboresha na kukua. Mwalimu maarufi wa kiroho Mtakatifu Bernardo alikuwa akisema kuwa udadisi tasa na maneno ya kiju juu, ndiyo ngazi za kwanza za ngazi za kiburi ambazo hazipeleki juu, bali chini, kwa kumuangusha mtu kuelekea upotevu na uharibifu (I gradi dell’umiltà e della superbia). Kinyume chake Yesu anatufundisha kuenenda kwa mtindo tofauti. Na tazama anasema nini “Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu;(Rej Mt 18, 15)Kuzungumza mimi na wewe” kwa uhalisia, kwa ajili ya kumsaidia aelewe alipokosea. Ufanya kwa ajili ya wema wake, kwa kushinda ainu na kupata ujasiri wa kweli , amba osio ule wa kumsengenyea, lakini ule wa kusema mambo uso kwa uso kwa unyenyekevu na upole.

Baba Mtakatifu amesema kuwa tunaweza kujiuliza  kuwa na ikiwa haitoshi? Ikiwa haelewi? Nam kwa njia hiyo inabidi kutafuta msaada. Lakini kuwa na umakini unahitajika, kwani siyo ule wa kufanya kikundi cha kusengenya! Yesu anasema “chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili,” akimaanisha watu ambao wanapenda kweli kusaidia kaka huyo na dada ambaye amekosea. Na ikiwa haelewi bado ? Hapo Yesu anasema uhusisha Jumuiya. Lakini hata hapo Baba Mtakatifu amependa kueleza usahihi kuwa siyo kumweka mtu katika masimango, kumuabisha adharani, bali ni kuunganisha nguvu za wote ili kumsaidia abadilike. Kumnyoshea kidole dhidi yake siyo jambo zuri badala yake mara nyingi inakuwa nguvu kwa aliye kosea kujitambua makosa yake.

Zaidi ya  Jumuiya lazima ifanye ahisi kaka na dada hao, wakati wanahukumu makosa yao kuwa wako karibu nao kwa sala, na upendo daima tayari kumpatia msamaha na kuanza upya. Papa Francisko kwa njia hiyo amesema, tujiulize je mwendendo wangu hukoje kwa yule anayenikosea? Ninazingatia ndani mwangu na kukusanya kinyongo? Inakuwa sababu ya masengenyo nyuma ya mgongo? Au ninatafuta kuzungumza naye? Ninasali kwa ajili ya kaka na dada huyo kuomba msaada wa kufanya yaliyo mema? Na Jumuiya zetu zinachukua mzigo kwa anayeanguka ili kuweza kuamka na kuanza maisha mapya? Je wananyosha vidole au wanafungua mikono yao? Mama Maria ambaye anaendelea kupenda licha ya kusikia watu wanamhukumu Mwanae, atusaidie kutafuta daima njia ya wema. Papa amehitimisha tafakari yake.

Tafakari ya Papa Angelus
10 September 2023, 15:13